Serikali impe angalizo Jerry Silaa, namuona anaiingiza Serikali katika mgogoro mkubwa wa kulipa fidia!

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,662
Leo katika taarifa ya habari ya ITV nimemuona Jerry Silaa akisimamia kubomoa ghorofa, na bila shaka kwa kujifanya yeye ni hakimu au Jaji mwenye uamuzi wa mwisho, kwa nini asishauri watu wafuate mlolongo wa mahakama ambao unasikiliza pande zote na kutoa haki ya rufaa ya ngazi tofauti? Kwa nini asiache tafsiri ya mwisho ya haki ifanywe na mahakama kabla ya mtu yoyote kuingizwa kwenye hasara?

Hofu kubwa ni kwamba haya mambo anayafanya Dar es salaam kwa kusaidia watu ambao mi marafiki zake, au marafiki wa familia yake. Ukikutana na family friend wa Silaa, na kimsingi wanamzonga sana pale ofisini watumie fursa kabla hajatenguliwa, ujue lazima atavuruga kila kitu ili kwemye vikao vya ukoo au harusi akasifiwe. Imagine Waziri mzima anatembea mpaka kwako na mmoja wa watu waliolalamika, yule anayelalamikiwa yuko na nani? Na ameshamumini anayekulalamikia, kamkodia mpaka greda, sijui kwa hela za serikali au kamshawishi akodi! utamwambia nini akuelewe?

Ajiepusha kuiweka serikali mbele katika kila tukio, aache sheria ichukue mkondo, akiwa waziri wa ardhi, miaka kumi serikali italipa fidia za trilioni na zaidi.

Nina imani haya mambo ya hovyo anayafanya bila kuhusisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, angewahusisha wangemkatalia maana wao ndio wanajua vita ya mahakamani ikoje, yeye atafanya upuuzi wake, atatenguliwa, na anatuachia hasara kubwa ya kulipa fidia.

Mawaziri wapya watoto watoto wasipewe wizara nzito kama ardhi. Waziri badala ya kushughulikia sera za kitaifa, anazurura mitaani ambako tayari ana maafisa ardhi. Mchi hii ina mitaa mingapi? Kama sera ina shida kutatua migogoro ya ngazi hizo, yeye kama waziri kaliambia nini Bunge limtungie sheria kutengeneza mfumo imara wa watu wa ardhi kuwa na mawasiliano na wateja wao? Atafika lini Chankende kutatua mgogoro?

Wazara yake inatoa hati, baadae inaikataa hati moja,inaikubali nyingine, halafu yuleyule waliyempa hati na kibali cha ujenzi, wao wenyewe wanaenda kumvujia walichomruhusu ajenge!
 
Leo katika taarifa ya habari ya ITV nimemuona Jerry Silaa akisimamia kubomoa ghorofa, na bila shaka kwa kujifanya yeye ni hakimu au Jaji mwenye uamuzi wa mwisho, kwa nini asishauri watu wafuate mlolongo wa mahakama ambao unasikiliza pande zote na kutoa haki ysisia rufaa ya ngazi tofauti?
Sisi ndoo kijaaani ohhhhh ooohhh,sisi ndo kijaaaaa iohhhh🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hofu kubwa ni kwamba haya mambo anayafanya Dar es salaam kwa kusaidia watu ambao mi marafiki zake, au marafiki wa familia yake.

Ajiepusha kuiweka serikali mbele katika kila tukio, aache sheria ichukue mkondo, akiwa waziri wa ardhi, miaka kumi serikali italipa fidia za trilioni na zaidi.
Saa zingine wanaiingiza serikali mkenge ili wao wakaneemekee kwenye hiyo hasara ya serikali, kwa maneno mengine hiyo inaweza kuwa syndicate
 
Nimeona nimeshangaa sana halafu watu wapo ndani yeye anabomoa nje ingekua amri ya Mahakama watu na vitu vitolewe ndio zoezi liendelee nimeona yule mama mwenye nyumba anatia huruma sana,
Hivi viwanja ni vina migogoro kwa sababu ya madalali kufanya yao na hasara unakuja kupata wewe huhusiki na una hati toka serkalini ovyo kabisa!

sheria ya ardhi iko wazi. mwenye hati ya kwanza halali ndie mmiliki.

maafisa ardhi wahuni huwa wanatoa hati halali hata kwa watu kumi tofauti.

hapo yule wa kwanza ndie anakuwa mmiliki
 
sheria ya ardhi iko wazi. mwenye hati ya kwanza halali ndie mmiliki.

maafisa ardhi wahuni huwa wanatoa hati halali hata kwa watu kumi tofauti.

hapo yule wa kwanza ndie anakuwa mmiliki
Nani kasikiliza pande zote akajua nani ana hati halali? Na haiangaliwi hati tu, yanaangaliwa mambo mengi, huyo aliyevunjiwq anasema aliyemuuzia ardhi alimshinda huyo mama mahakama zote za nchi hii
 
Back
Top Bottom