My take
Naanza kuona kwamba Tanganyika inafaidika na huu muungano kuliko zanzibar.Kama isingekuwa inafaidika,basi wangejitokeza hadharani wanaharakati (kutoka Tanganyika wanaotambuliwa na serikali) kufanya harakati kama hizo za akina Jussa na Maalim Seif kuhusu Tanganyika huru.
zanzibar sio nchi
Wanaharakati wapo JF lakini wananishangaza kweli.
Wao wanakuja na makala na maoni kutushawishi tudai serikali moja, nchi moja, taifa moja.
Hawa wanaharakati wengi wa JF wanamawazo tofauti na yako. Wan hoja ya kuwa Zaznibar inapata umeme bure, biloni 32 kapewa Bilali nk.Mimi nakubaliana na wewe kidogo. Tanganyika kama nchi au sehemu ya Muungano inafaidika na pia Zanzibar au wananchi wazanzibari wanapata faida binafsi ya biashara na ardhi.
Lakini anaefaidika hasa na hii set up ya sasa ya Muungano ni CCM na viongozi wa CCM.
Sisi kama wadanganyika bado hatuoni faida ya kuidai Tanganyika huru lakini ujio wa Tanganyika utasawazisha dosari ya mchanganyo wa mambo mengi ambayo yanleta utata katika muungano huu.
Faida kubwa itakuwa ni kuupata utaifa wetu wa Tanganyika na wengi wetu ambao tumeambulia kujiita wabara au watanzania bara tutajitanafasi kama wanavyojivunia wazanzibari kujiita wazanzibari.Tutasema kwa vinywa vipana kuwa sisi ni watanganyika. Wenzetu wa UK wanajivunia kujiita British nawakati huo huo kujiita English ,Welsh au Scottish. Hakuna mkinzano kujiita Mtanzania na pia mtanganyika.
Faida ya pili itakayopatikana ni kumaliza ukiritimba wa CCM juu ya karata ya muungano na mfumo wake.
Tatu na muhimu zaidi kila Taifa/upande wa muungano utakuwa na uhuru wa kujiamulia mambo ya ndani kivyake bila ya siasa za sasa za" wasiokubaliana na sera ya chama ya serikali mbili waondoke au warudishe kadi". Muungano hautakuwa kiini macho tena ya kudumaza maendeleo ya pande mbili za muungano.
Ya pamoja yatajulikana haya ni ya pamoja baina ya Tanganyika na Zaznibar na ya kila upande kivyake yatajulikana bila ulalamishi au visingizio vya "upuuzi".
Tuamke tudai Tanganyika huru.
Na sisi Watanganyika tuna kero zetu za Muungano;-
- Rais wa Zanzibar ajaye naye atokee bara, maana mwinyi alishatoka zanzibar - kama urais ni kwa zamu
- Watanganyika turusiwe kununua ardhi zanzibar, ikishindikana ardhi zinazo milikiwa na wazanzibar zilizopo bara tuzitaifishe
- Sehemu ya wabunge au wabunge wote wa bara waruhusiwe kuingia katika bunge la zanzibar, ikishindikana basi wabunge kutoka zanzibar wasiingie bunge la bara.
- Bei za umeme, tutozwe wote bei sawa ikishindikana iwe zamu ya zanzibar kutuuzia umeme bara kwa bei ya chini kuliko inavyotoza raia wake.
- Pasiwapo upendeleo wowote katika usahihishaji wa mitihani....!
Jusa ni m'baguzi, na hata wakoloni walioitawala zanzibar wenye asili yake walitubagua sana weusi.....hapa hana lolote, shida yake anataka apewe cheo au nafasi fulani katika muungao ili anyamaze. Good move JUHa
Kibanga Msese
Kwenye facebook wall yake ametupia kitu hiki:
"Wakati tunaelekea India wiki iliyopita tukiwa Uwanja wa Ndege wa Dubai wakati tunabadilisha ndege, tulikutana na mmoja wa Makamishna wa Tume ya Katiba kutoka upande wa Tanganyika ambaye ni msomi wa hali ya juu.
Katika majibu ya kustaajabisha wakati nilipomuuliza vipi hali ya utoaji maoni inaendelea, alitujibu kuwa inaendelea vizuri na pamoja na kwamba upande mmoja (nna hakika alikusudia Zanzibar) unatoa madai makubwa, yeye haimpi tabu kwa sababu anajua wanaofanya hivyo wanajipa nafasi kubwa ya kuja kupatana (alitumia neno la Kiingereza 'bargaining') ili kupata muafaka wa kati na kati.
Bahati mbaya mawazo kama haya ya Kamishna huyu ndiyo mawazo mgando ya watunga sera na sheria wengi wa Tanganyika wanaojiona kama ni watawala au wamiliki wa Zanzibar na hivyo kujipa matumaini kuwa Zanzibar tunaposema tunataka kurejesha mamlaka yetu kamili kitaifa na kimataifa tukiwa na kitu chetu Umoja wa Mataifa huwa tunatafuta 'kupatana' au kwamba hatuna uwezo huo mpaka Tanganyika waridhie.
Wanapaswa wajue sasa kabla hawajachelewa kwamba mamlaka kamili ya Zanzibar (Sovereign Zanzibar) siyo ombi ni matakwa ya Wazanzibari na tutayasimamia kwa nguvu na uwezo wetu wote. Na katika kulifikia lengo hilo hakuna wa kutuzuia isipokuwa Mwenyezi Mungu. Pamoja Daima!"
My take
Naanza kuona kwamba Tanganyika inafaidika na huu muungano kuliko zanzibar.Kama isingekuwa inafaidika,basi wangejitokeza hadharani wanaharakati (kutoka Tanganyika wanaotambuliwa na serikali) kufanya harakati kama hizo za akina Jussa na Maalim Seif kuhusu Tanganyika huru.
Hivi akina Lipumba na Mtatiro huwa wanasemaje kuhusu hili au ni MABUBU mbele ya akina Jussa na Maalim?
zanzibar hamuwezi kua nchi..hicho ni kisiwa tu cha utalii kama vingine
Facts, umenena
kuongezea ikiwezekana kuwepo na utaratibu wa pass kuingia tanganyika au zanzibar.
Hapo kwenye swala la umeme ndiko kutawafanya wautamani muungano na washindwe kuuvunja.
Heri ya waTg waliojikalia kimya kuliko unafiki wa wazenj! Huku wataka na huku wataka! Manake dawa ya kuuvunja Muungano haiko mwezini ili utafute chombo cha kufika mwezini! TL aliwapa dawa hawakuitaka kwa sababu wanautaka mfumo uliopo wa muungano! Hivyo basi waTg hatutaki kero zenu wazenj na chokochoko na mashairi yenu!Watanganyika wanafiki, hawako wazi juu ya Muungano. Mimi binafsi faida za muungano huu ni chache kuliko kero/mabaya ya muungano wenyewe. Hautufai, tuwe na serekali tatu, Tanganyika, Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Serekali ya shirikisho la Tanganyika na Jamhuri ya watu Wa Zanzibar. Full stop.