Jussa: Hakuna "kupatana" na Watanganyika

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Kwenye facebook wall yake ametupia kitu hiki:
"Wakati tunaelekea India wiki iliyopita tukiwa Uwanja wa Ndege wa Dubai wakati tunabadilisha ndege, tulikutana na mmoja wa Makamishna wa Tume ya Katiba kutoka upande wa Tanganyika ambaye ni msomi wa hali ya juu.

Katika majibu ya kustaajabisha wakati nilipomuuliza vipi hali ya utoaji maoni inaendelea, alitujibu kuwa inaendelea vizuri na pamoja na kwamba upande mmoja (nna hakika alikusudia Zanzibar) unatoa madai makubwa, yeye haimpi tabu kwa sababu anajua wanaofanya hivyo wanajipa nafasi kubwa ya kuja kupatana (alitumia neno la Kiingereza 'bargaining') ili kupata muafaka wa kati na kati.

Bahati mbaya mawazo kama haya ya Kamishna huyu ndiyo mawazo mgando ya watunga sera na sheria wengi wa Tanganyika wanaojiona kama ni watawala au wamiliki wa Zanzibar na hivyo kujipa matumaini kuwa Zanzibar tunaposema tunataka kurejesha mamlaka yetu kamili kitaifa na kimataifa tukiwa na kitu chetu Umoja wa Mataifa huwa tunatafuta 'kupatana' au kwamba hatuna uwezo huo mpaka Tanganyika waridhie.

Wanapaswa wajue sasa kabla hawajachelewa kwamba mamlaka kamili ya Zanzibar (Sovereign Zanzibar) siyo ombi ni matakwa ya Wazanzibari na tutayasimamia kwa nguvu na uwezo wetu wote. Na katika kulifikia lengo hilo hakuna wa kutuzuia isipokuwa Mwenyezi Mungu. Pamoja Daima!"

My take
Naanza kuona kwamba Tanganyika inafaidika na huu muungano kuliko zanzibar.Kama isingekuwa inafaidika,basi wangejitokeza hadharani wanaharakati (kutoka Tanganyika wanaotambuliwa na serikali) kufanya harakati kama hizo za akina Jussa na Maalim Seif kuhusu Tanganyika huru.

Hivi akina Lipumba na Mtatiro huwa wanasemaje kuhusu hili au ni MABUBU mbele ya akina Jussa na Maalim?
 
MKUU!

Watajwa hapo juu, hawana uwezo wa kupinga hoja hizo. Hii ni kwa sababu kula yao si inatoka huko kwa WABURUSHI!!!!!!!!!
 
Mimi naona wangepatikana watu 20 tu waTanganyika wenye uthubutu kama wa Tindu Lissu Kwenye Bunge la Muungano basi mambo yangekuwa sawia kabisa.

Hebu pitieni kwenye ansard za Bunge muone maneno yake haya.

``Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Rasimu ya Muswada hayakubaliki kwa sababu yanaweka mchakato wa Katiba Mpya kwenye huruma na/au fadhila ya Rais wa Zanzibar na siasa za Zanzibar kwa ujumla. Kwa mapendekezo haya, Rais wa Zanzibar asipokubaliana na jambo lolote linalohitaji ridhaa yake basi mchakato mzima utasimama au kusitishwa. Aidha, endapo katika kura ya maoni inayopendekezwa, theluthi mbili ya Wazanzibari hawatakubaliana na Katiba Mpya basi Katiba hiyo haitapitishwa hata kama inakubaliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania Bara.

Mustakbala wa taifa letu hauwezi kuwekwa tena rehani kwenye siasa za Zanzibar na kwenye matakwa ya Wazanzibari kwa kiasi hicho. Kuhusiana na jambo hili, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar ahusishwe tu katika masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Nje ya masuala hayo, Rais wa Zanzibar hana sababu yoyote ya kuhusishwa na mchakato wa kikatiba unaohusu mambo ya Tanzania Bara."

Aidha, wajumbe wa Tume ya Mapitio ya Katiba ambao watatoka Zanzibar wahusike tu katika mchakato wa masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wananchi wa Zanzibar washiriki katika kura ya maoni inayohusu mfumo mpya wa Muungano tu. Hii ndio kusema kwamba, kama vile ambavyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Tanzania Bara hawajashirikishwa katika mchakato wa kikatiba wa Zanzibar kwa sababu ulihusu mambo yasiyokuwa ya Muungano, vivyo hivyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Zanzibar wasishiriki katika mchakato wa kikatiba wa mambo yasiyokuwa ya kikatiba kwa upande wa Tanzania Bara.``

Wanakosea kufanyia harakati zao huku tanganyika, wange deal na bunge lao tu, wakatoka na azimio la wazanzibar, wala sii uhaini. Tumechoka kelele zao.
 
Watanganyika wanafiki, hawako wazi juu ya Muungano. Mimi binafsi faida za muungano huu ni chache kuliko kero/mabaya ya muungano wenyewe. Hautufai, tuwe na serekali tatu, Tanganyika, Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Serekali ya shirikisho la Tanganyika na Jamhuri ya watu Wa Zanzibar. Full stop.
 
Muungano hauna faida hata uku bara nashangaa kwa nini tunaung'ang'ania?
 
Hata ukivunjia huo Mvungano basi atachukua viza na kuja kama atataka. Wala isiwe sababu kwa mtu makini kusema fulani yupo nchii hii.

Kwani taratibu zote za uhamiaji zitafuatwa kwa wafanyabiashara na hata wenye vitega uchumi. Hilo si ajabu kuona Mtanzania anamiliki nyumba au ana biashara katikati ya London.

Ondoa khofu.
 
Muungano ni maslahi ya viongozi wa CCM wa Tanganyika wala hakuna lingine.

Hili ulisemalo halina ubishi.Muungano kama ulivyo leo ni ngao ya CCM, sio viongozi wa CCM wa Tanganyika tu bali hata viongozi wa CCM wa Zanzibar. Lakini vinara wa ung'ang'anizi wa mfumo/muundo wa muungano uliopo ni viongozi wa CCM wa Tanganyika na wapiga debe wao wachache hapa JF. Hasa kinara mmoja wa fikra pevu.
Guess who? Na mwandishi mmoja wa makala za muungano.
 
Kama mchango wa Barubaru unavyojieleza hapo juu post#4. Wakati CCM wanajitahidi kukumbatia mfumo/muundo wa muungano kama ulivyo. Watanganyika bado tumepiga usingizi. Lissu mmoja ambaye anaishia kwenye kauli tu ni dalili tosha kuwa bado hatuna mwamko wa kutosha kuhusu mambo yanayoihusu Tanganyika kutekwa nyara na CCM kwa maslahi yao ya kisiasa.

Dai alilolitoa Lissu juu ya umuhimu wa kuirejesha Tanganyika na katiba yake limeishia kwenye Hansard tu za bunge lakini hakuna mkakati wa kuhakikisha linatokea.

Muungano huu unaweza kuondolewa au kufanyiwa ukarabati ili kukidhi matakwa ya wanachama wake bila ya kejeli, vitisho, dharau au kupandikiza chuki lakini inaonekana CCM wanautumia muungano kama karata yao ya mwisho ya kujihakikishia inabaki madarakani kwa kadiri wananchi wanavyoshindwa kuelewa ujanja huu wa CCM.

Lakini CHADEMA na vyama vyengine vya upinzani pia havionekani kuwa vimegundua siri hii ya CCM. CHADEMA ingesimamia hili la Muungano kwa dhati na kuirudisha serikali ya Tanganyika basi 2015 ingewakalia vyema.
CHADEMA wakilivalia njuga, sio kwa kauli tu bali kwa vitendo itaungwa mkono na vyama vyengine vya upinzani na wananchi wa pande zote za muungano kwa asilimia kubwa sana.

Kuvunja muungano au kuusuka upya sio uhasama wala uhaini na hili linaweza kufanyika kwa njia za ustaarabu tu. Majadiliano bungeni, makongamano, kupeleka mswada binafsi bungeni na kura ya maoni kuamua hatma ya muungano. Tanganyika tuoneshe mfano ili tuondokane na muungano wa usanii.
 
Na sisi Watanganyika tuna kero zetu za Muungano;-

  • Rais wa Zanzibar ajaye naye atokee bara, maana mwinyi alishatoka zanzibar - kama urais ni kwa zamu
  • Watanganyika turusiwe kununua ardhi zanzibar, ikishindikana ardhi zinazo milikiwa na wazanzibar zilizopo bara tuzitaifishe
  • Sehemu ya wabunge au wabunge wote wa bara waruhusiwe kuingia katika bunge la zanzibar, ikishindikana basi wabunge kutoka zanzibar wasiingie bunge la bara.
  • Bei za umeme, tutozwe wote bei sawa ikishindikana iwe zamu ya zanzibar kutuuzia umeme bara kwa bei ya chini kuliko inavyotoza raia wake.
  • Pasiwapo upendeleo wowote katika usahihishaji wa mitihani....!

Jusa ni m'baguzi, na hata wakoloni walioitawala zanzibar wenye asili yake walitubagua sana weusi.....hapa hana lolote, shida yake anataka apewe cheo au nafasi fulani katika muungao ili anyamaze. Good move JUHa

Kibanga Msese
 
zanzibar hamuwezi kua nchi..hicho ni kisiwa tu cha utalii kama vingine
Mtotowamjini

Umesoma jiografia?
Kama jibu ni ndio. Unajua Cape Verde iko bara lipi? Mauritius inapatikana wapi? Sao tome?

Kama huna habari ya hayo. Jipatie maarifa hapa. Bonyeza links. São Tomé and Príncipe - Wikipedia, the free encyclopedia link Cape Verde - Wikipedia, the free encyclopedia link Mauritius - Wikipedia, the free encyclopedia

Baada ya kujiongezea maarifa, unaelewa sasa kuwa kuna nchi za visiwa?

Umewahi kusikia nchi inaitwa Singapore, Fiji, Solomon Islands - Wikipedia, the free encyclopedia.

Zanzibar inaweza kuwa nchi kama ulivyoona hapo juu kwa hizo nyengine. Usiwakatishe tamaa.
Unajua Singapore walifukuzwa kutoka Shirikisho la Malaysia? Singapore walilia,walijisikia wanyonge sana, leo linganisha Malaysia na Singapore.

Jee Kongo (Zaire) ni nchi?

Nini kinafanya nchi kuwa nchi?
 
Na sisi Watanganyika tuna kero zetu za Muungano;-
Kibanga Msese
Kutaka Jussa apewe cheo anyamaze si suluhisho.

Suluhisho ni sisi kudai Tanganyika.Umesahau hili.
Tudai Tanganyika na kama tutaona bado kuna umuhimu wa kuwa na muungano basi kutakuwa na mipaka inayoeleweka kuhusu mambo ya muungano, mambo ya Tanganyika na mambo ya Zanzibar.

Mwalimu Nyerere alitoa rai kuwa itakapoanzishwa tena jumuiya ya Afrika Mashariki basi Tanzania iwe na serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar
(
"Kwa kweli hata keshoNchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikishaTanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika ..." Uk 11-12 .link ya kitabu hii Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
 
Miongoni mwa vitu ambavyo Nyerere aliteleza ni kukurupukia huu Muungano ambao hata hauna documents na terms zake mpaka sasa wanazijua TANU na ASP tu! Lakini hatujachelewa ,hivi kwanini isifikie hatua serikali ikubali kufanyika kwa referendum then matokeo yake yazingatiwe na kuheshimiwa na pande zote mbili?Mimi mtanganyika wa kawaida wala sioni faida ya huu muungano.

(Kama ishu ni kupata totooz za kichotara wa kiarabu(shombeshombe) kutoka Pemba hata huku kwetu Tabora tuna warabu wanaongea mpaka kinyamwezi hadi uswahilini (It's a joke)).
 
Back
Top Bottom