Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Sitta amsifu JK kumteua mbunge makini
na Hellen Ngoromera, Dodoma
MBUNGE wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CUF), jana ameingia bungeni kwa kishindo baada ya kuzungumza kwa mara ya kwanza akionya kuwa suala la mgombea binafsi si hiari ya serikali bali ni uamuzi halali wa Mahakama Kuu hivyo serikali inatakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kulitekeleza. Jussa alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za uchaguzi wa mwaka 2009 uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Philip Marmo.
Alisema hivi karibuni Jaji Mkuu Augustino Ramadhan akishirikiana na jopo la majaji kutoa kauli kuwa suala la mgombea binafsi ni halali kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa mbunge huyo suala la serikali kupeleka rufani ya mgombea binafsi Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji Mkuu na jopo lake haileti taswira nzuri katika utawala wa mihimili mitatu ya dola ambayo ni mahakama, Bunge na serikali.
Mheshimiwa Spika nimepata shida kidogo baada ya kusikia maneno ya Naibu Mwanasheria Mkuu kuhusu suala hili kwani maelezo yake yalikuwa ya utatanishi, alisema Jussa.
Alisema mahakama inapaswa kuheshimiwa kama ilivyo kwa Bunge hivyo hatua zozote za serikali kutaka kupindisha mambo na kuminya haki za msingi za Mtanzania haziwezi kuvumiliwa.
Jussa alisema sehemu kubwa ya muswada huo imezungumza mambo ya juujuu na kwamba kuletwa kwake muda mfupi kabla ya uchaguzi, hakuleti sura nzuri.
Muswada huu una upungufu mkubwa sana, ungezingatia mambo mengi ikiwemo utendaji wa vyombo vya dola wakati wa uchaguzi kwani suala hili halijaguswa, alisema Jussa.
Akizungumzia kuhusu uteuzi wake, Jussa alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kufanya kitu cha kihistoria na anaamini kuwa amefanya hivyo kuyaletea nguvu maridhiano yaliyofikiwa kati ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na Rais wa Zanzibar Aman Abeid Karume.
Mheshimiwa Spika kabla sijatoa hoja yangu napenda kumshukuru mheshimiwa rais kwa hatua yake hii ya kihistoria kuniteua kuwa mbunge.
Awali sikuwa na taarifa kuhusu hili, lilipotangazwa hili, kuna mtu alinichokoza na kuniambia kuwa unaenda bungeni wakati ikiwa imesalia miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu kwa hiyo utaipeleka ile hoja yako uliyoitoa katika Baraza la Wawakilishi, nami nataka kusema kuwa sikusudii kuileta hoja hiyo hapa niliipeleka kule kutokana na uhalisia wake, alisema Jussa.
Jussa aliitaka serikali kupunguza ukaidi kwa baadhi ya mambo na isikilize hoja zinazotolewa na kambi ya upinzani katika kurekebisha kasoro mbalimbali zinazotolewa ili nchi iweze kupiga hatua.
Baada ya kumaliza kutoa mchango wake, Spika Samuel Sitta alimsifu Jussa kwa kuchangia hoja yake vizuri na kusema kuwa hakika rais anajua kuteua.
Kwa mujibu wa Spika pamoja na ugeni wake, Jussa amepangilia vyema hoja zake na kuziwasilisha inavyotakiwa na kusema kuwa hali hiyo inaashiria mambo mazuri.
Akijibu hoja mbalimbali, Waziri Marmo alisema suala la mgombea binafsi ni hoja nzito na kwamba si ya kupuuza kwani inagusa Katiba.
Alisema kwa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu suala hilo si rahisi kushughulikiwa kwa sasa kwani linahitaji marekebisho mbalimbali yakiwemo marekebisho ya kisheria.
Mheshimiwa Spika suala la mgombea binafsi ni zito na linagusa katiba hivyo kwa kuwa muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu ni mdogo sio rahisi suala hili kushughulikiwa kwa sasa kwani linahitaji mchakato mzima wa kubadilisha sheria zetu, alisema Marmo.
Angalau Jussa ameanza vizuri...naamini tafanya vizuri zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha kulitumikia Bunge na wananchi.