johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,036
- 142,123
Kaimu Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo Jussa amesema Tanganyika suala dogo tu la Bandari kelele kila kona wakati wao wameipora Zanzibar vitu kibao kuanzia 1964
Jussa amesema Zanzibar Ilikuwa na Polisi wake, Ilikuwa na Jeshi lake, Ilikuwa na Passport, Ilikuwa na Mabalozi, Ilikuwa na fedha yake, Ilikuwa na Kiti UN na mambo mengine chungu nzima lakini yote yameporwa na Tanganyika
Jussa amesema suala la Bandari wao Zanzibar haliwahusu so Watanganyika wapambane na hali zao
Jussa ameonya wanaozungumzia kuvunja Muungano kwamba wao wako tayari hata kesho wameshachoka
Jussa alikuwa akihutubia Mkutano wa hadhara huko Puja Zanzibar uliohudhuriwa na Makamu wa kwanza wa Rais Masoud Othman
Mlale unono!