Mkuu siwezi kukubishia maana enzi zile usalama wa taifa ulifanya kazi kama hizi kafuatilia mambo kama haya,pindi dodoso kama hizi zilipopatikana.Pamoja na kwamba uzi huu umemtaja mwalimu Nyerere,kama mmoja wapo wa waliofuga mfumo huu wa tutsi empire,lakini usalama wa taifa kipindi kile ulikuwa umekaa vizuri.
Na inteligence ilikuwa inteligence kweli siyo kama mfumo wa sasa wa kupeleka waliofail mitihani ya form four ilhali wana ndugu zao wanaowaback up.
Usalama wa taifa umebaki kuilinda ccm na siyo nchi.Zamani watu walikuwa mipakani ukiwaona utadhani hawana kazi lakini habari ziliweza kufika kunakohusika ndani ya siku moja.Miradi yote mikubwa iliyoanzishwa nchi wanausalama wa taifa waliajiliwa kama wataalam huku wakichunguza mambo yanayohusu usalama wa nchi,leo hii nchi ina miradi mikubwa unafanyika usalama wa taifa sifuri eti tunategemea habari kutoka kwa raia wema!Mambo haya siku hizi yamebinafsishwa eti ulinzi shirikishi,sishangai unaposema kuna wanajeshi na polisi wa kigeni nchini huo ndo ulinzi shirikishi wenyewe.Siku hizi hata mwizi analinda mtaa ilhali amejitolea kulinda kumbe unafanya upelelezi wa mitaa tulivu wakati wa usiku na mitaa yenye watu wasiolala,akiisha kamilishja anakuja anaiba.
Uzi huu sio wa kupuuza,usalama wa taifa kama mpo fanyeni uchunguzi wa kina kubaini ukweli.Mipango kama hii ikiwepo watakaoumia wa kwanza ni ninyi wakubwa mtakapoanza kutawaliwa wakati mlizoea kutawala,sisi wadogo tumezoea kutawaliwa,kula kilichosalia maumivu kwetu yanaweza kuwa sawa na hakuna.
Fanya summary umeambiwa ujazad booklet??