Juma Dogan: Kada wa CCM 'aliyemwokota' Abdul Nondo Mafinga na kumpa nauli ya taxi aende kuripoti Polisi kupatikana kwake

Anaweza asiwe mshukiwa.

India zamani walifanya hivyo. Unampeleka mtu Polisi yanakuwa yako gharama zote mpaka hospitali na ushahidi wa kuisaidia polisi. Basi watu wakawa wanaacha hata majeruhi wa ajali wanapita pembeni tu.

Siku hizi kampeni zimeanza za kuelimisha watu umuhimu wa kuwasaidia majeruhi na watu wanaookotwa kwa shida mbalimbali na kuwapeleka panapostahili.

Dreva wa taxi mmoja maarufu jijini Delhi anafanya hivyo na taarifa zake ziliandikwa sana na vyombo vya habari hivi karibuni.

Tumshukuru huyo bwana. Tusimlaumu kwa kutompeleka maana kwa hakika ingebidi aisaidie polisi. Bado anapaswa kuisaidia. Ila asiogope. Kutoa ushahidi kitu chema.
Umeongea vizuri sana...ila tatizo maelezo ya msamaria mwema yana ukakasi unaofanya atiliwe shaka...
 
Alishushwa kwenye basi gani? Kaokotwa na kada saa 4 usiku kwenye msitu wa sao hill !!? Alikua hajitambui halafu akakodiwa tax impeleke polisi?!!!!
 
Anaweza asiwe mshukiwa.

India zamani walifanya hivyo. Unampeleka mtu Polisi yanakuwa yako gharama zote mpaka hospitali na ushahidi wa kuisaidia polisi. Basi watu wakawa wanaacha hata majeruhi wa ajali wanapita pembeni tu.

Siku hizi kampeni zimeanza za kuelimisha watu umuhimu wa kuwasaidia majeruhi na watu wanaookotwa kwa shida mbalimbali na kuwapeleka panapostahili.

Dreva wa taxi mmoja maarufu jijini Delhi anafanya hivyo na taarifa zake ziliandikwa sana na vyombo vya habari hivi karibuni.

Tumshukuru huyo bwana. Tusimlaumu kwa kutompeleka maana kwa hakika ingebidi aisaidie polisi. Bado anapaswa kuisaidia. Ila asiogope. Kutoa ushahidi kitu chema.

Ukweli ni kwamba huyu kada anatakiwa kuhojiwa na watu wenye uweledi na walio huru kabisa katika hili. Kuna mambo mengi ya kujiuliza kabla ya kudhani ni muhusika na kabla ya kudhani ahusiki.
1. ni lazima kujua huyu bwana mafinga ameenda lini akitokea dsm
2. Mwenyeji wake huko mafinga alikuwa nani.
3. Anafanya biashara gani na ameanza lini hiyo biashara.
4. Alipataje habari za kijana huyu huko mafinga mpaka anafika kutoa msaada/ alikutana naye tu barabarani au alisikia habari za mtu kutelekezwa kisha akaenda kutoa msaada.
5. Alikuwa na nani wakati wa kutoa msaada
6. Alipataje namba ya simu ya Kumbusho downson (mzee wa expansion joint)
7.Kwanini yeye hakutaka kwenda polisi kumsikindikiza.

Lakini ni hatari kubwa sana kumhusisha moja kwa moja huyu jamaa na hilo tukio maana kwa kufanya hivyo kutafanya wengine nao waogope kusaidia watu wanaopatwa na majanga. Wengine wanataka kumhukumu kwasababu ya neno kada wa ccm, hiyo ni hatari na haipaswi kuwa hivyo .JAPO NARUDIA TENA HUYU JAMAA LAZIMA AHOJIWE KWA MBINU IMARA NA IKIBIDI ACHUNGUZWE HATA MIENENDO YAKE YA NYUMA ILI TUWEZE KUJIRIDHISHAA MAANA BINADAMU NI KIUMBE HATARI NA KISICHOELEWEKA.
 
Ukweli ni kwamba huyu kada anatakiwa kuhojiwa na watu wenye uweledi na walio huru kabisa katika hili. Kuna mambo mengi ya kujiuliza kabla ya kudhani ni muhusika na kabla ya kudhani ahusiki.
.

Juma dogan(Msamaria mwema), Abdul Nondo(Mtekwaji) na Kumbusho downson(Rafiki wa Msamaria mwema na Mtekwaji) ni wamoja, kimsingi wameigiza pamoja katika nafasi tofauti tofauti.
 
Hayaa kile kikundi tunachosemaga kimejidhihirisha..Huwa wanatembea na Noah muda mwingine Nissan...Tulishasema tuingie mzigoni tuwafyeke bado mnasitasita!

Noah nyeupe au Nissan unasema ? Utaisadia polisi kwa upelelezi.. Naombeni msihusishe CCM na mambo haya plse, CCM haifanyi upuuzi huo, kama ni kada muulizeni huyo ila sio tuhuma mnaitupia CCM.
 
Juma dogan(Msamaria mwema), Abdul Nondo(Mtekwaji) na Kumbusho downson(Rafiki wa Msamaria mwema na Mtekwaji) ni wamoja, kimsingi wameigiza pamoja katika nafasi tofauti tofauti.

Mkuu tume ya katiba hoja yako si ya kweli ukizingatia kwamba huyu msamaria ni kada wa ccm na kivyovyote anajua mambo kama haya mara nyingi ccm na serikali (ya ccm) ndiyo zinalaumiwa. Sasa huoni ni vigumu kada mtiifu kwa chama kushiriki kwenye mambo yanayokichafua chama na serikali yake?. Mimi nadhani huyu kada lazima achukuliwe kwa uzito katika swala hili wakati wa uchunguzi, lakini bado siwezi kusema kwa kujiamini kwamba anahusika japo pia siwezi kusema hahusiki. Kwamba anahusika au hausiki ni kazi ya vyombo vya dola.
 
Mhuuuum,kampa nauli ya Tax?Why asimsindikize?What a coincidence!Huyo kada anaishi Dar na yeye yupo Mafinga kwa shughuli za kibiashara.Any way all in all Abdul yupo hai.
Sasa kama anaishi dar asiende mafinga?? Na akimkuta mtu ana uhitaji asimsaidie?? Mbona hamna jema?? Suspect kwa lipi?? Hebu kuweni mnafikiria kabla ya kukurupuka
 
Kada wa CCM anajua mchongo mzima, mfanyabiashara usiku anatokea wapi pembeni ya msitu? Why ampe hela ya tax na sio kumpeleka mwenyewe kituoni?? Alijuaje kama ndio aliepotea mpaka ajipitishe hapo na kumpa hela?? Then imekuaje analireport hilo tukio haraka inbox ya marafiki wa Nondo??
Msitu upo katikati ya Mafinga na Nyololo,mtoa nauli alitoka Mafinga kuelekea Nyololo/Makambako?

Kama alitoka Nyololo/Makambako kuelekea Mafinga/Iringa,kwanini ashindwe kumchukua na kumuacha kituo cha polisi?
 
Huyo chizi anayesema alisafiri na mtekwaji kwenye basi la New force ningekuwa sijawahi kusafiri kupitia hiyo njia angekuwa amesha kula kichwa changu. Ila kwakuwa nimewahi kusafiri kupitia hiyo njia basi hanipati ng'ooo! Amejikoroga aliposema kuwa walipofika Morogoro jamaa aliomba anunuliwe maji! Kwa hapo hako ka drama kake kameshaingia shubiri, hakaliki tena!
 
Dar 2 iringa usafr na bus asubuh jion uwe umefka na kutupwa porini what a hell?
 
Back
Top Bottom