J'tatu hiyooo, Lema njeeee....

Sasa ukiisha msindikiza then what? kama ndoo kasha nyea na akifanya mchezo na mahama atarudi ndani na hata mkimuua hakimu bado atakaa ndani! CDM acheni u mbumbu wa kuabudu abudu watu! hali hii hamja chukua nchi mkichuku si itakua balaa!!

Na wewe umo???
 
Ni vizuri atoke ila sasa afanye kazi na sisi tufanye kazi. Hatuwezi kukaa tu mwaka sasa tunaongelea kitu kimoja
Atafanya je kazi wakati kila siku kesi haziishi...hata hivyo umefanya kazi miaka 50 mbona bado tuna didimia kila kukicha mwaka mmoja unaona tabu.....
 
Ni vizuri atoke ila sasa afanye kazi na sisi tufanye kazi. Hatuwezi kukaa tu mwaka sasa tunaongelea kitu kimoja
Mkuu, kufanya kazi maana yake ni nini? Hicho anachokifanya Lema yuko kazini. Huwezi kuanza ujenzi bila kuhakikisha foundation (msingi) umeshakaa sawa, vinginevyo hiyo nyumba itaanguka na kuwa hasara kubwa. Mheshimiwa Mbunge analilia utawala bora unaojali utu na heshima ya binadamu. Kwani nchi ya Tanzania imeanza kujengwa lini, huwezi kukimbilia kujaza ndoo maji huku ikiwa imetoboka. Tafadhali tushirikiane kuona hata vyombo vya dola vikifanya kazi kwa kufuata taratibu za utawala bora.
 
Ni vizuri atoke ila sasa afanye kazi na sisi tufanye kazi. Hatuwezi kukaa tu mwaka sasa tunaongelea kitu kimoja

MIAKA YOTE ULIYOFANYA KAZI UMEPATA NININI NA HAPO ULIPO UNA NINI ZAIDI YA TABU NA UMASIKINI FIKIRIA WEWE,KAZI ANAYOIFANYA LEMA NI KAZI YA MTANZANIA YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA NA NCHI HII NA WALA SIO KUZUIA WATU KUFANYA KAZI KAMA MAFISADI NA MAGAMBA YAO MNAVYOSEMA

wakati wa ukombozi ni sasa
 
Ni vizuri atoke ila sasa afanye kazi na sisi tufanye kazi. Hatuwezi kukaa tu mwaka sasa tunaongelea kitu kimoja

Hilo la kufanya kazi pamoja litawezekana tu kama magamba watakuwa waungwana, vinginevyo magamba wasahau
 
Tuacheni mizaha katika mambo nyeti kama haya. Yanayojalisha mstakabali wa taifa letu. Lema anahaki zote ya kuwazilisha hisia zake zote kwa namna yeyote ile ppopote pale anapopata nafasi hivyo. Tafadhali msimkejili, msifedhei, msimtweze, msimpige vijembe, msimkatishe tamaa, msimtukane, msimsulubishe, msiwaunge maadui zake mkono, msiache kumwombea muumba wake amjaaliye afya njema na fanaka tele n.k. Mambo yote hayo hapo juu tafadhali tuyaache yafanywe na vibaraka wa wawekezaji wa nchi za ughaibuni pamoja na mafisadi. Waungwana tuungane tuweke itikadi za kisias kando tulijenge taifa letu lililobomolewa na mafisadi, madhalani umeme shida, maji shida, madawa hospitalini shida, madaktari shida, elimu shida, waalimu shida,mfumko wa bei za bidhaa nyeti shida, misharahara ya wafanyakazi wa umma shida, ugumu wa maisha shida. Tunategemea nini katika hali kama hiyo waungwana, itabidi tuanze kufikiria kwa kichwa na wala si kwa tumbo, waungwana wenzangu!!! Mungu uibariki Tanganyika, Mungu uibariki Zanzibar. Inshala!!!
 
Majira haya ya Asubuhi jiji hili la Arusha limesimamisha shughuli zake na kuwa kimya huku shamrashamra zikiwa maeneo ya mahakama kuu ya Arusha, Lema amekwisha wasili mahakamani hapo na watu ni wengi mno na wameapa kutembea kwa miguu kwenda sehemu yeyote ile atakayoelekea. Police wamekuwa wa pole kama maji ya mtungi.
 
komaeni nao mwanzo mwisho, tena muwaambie wazifukie silaha zao waje tupambane kwenye kupata katiba mpya isiyokuwa na mazongemazonge
 
Jamani vp, hv leo LEMA atafanya mkutano wa hadhara au polisisisiem wamepiga mkwara? Hawachelewagi kupata habari za kiintelijensia kwenye mikutano ya cdm
 
Juzi wananchi walikataa wawakilishi wateule wa Raisi Mbeya wakamtaka Mbunge wao, polisi, JKT, JWTZ walichemsha kuwatuliza mpaka Mbunge wao Mr Sugu alipowasili. Watu wa Arusha walimpenda Lema wakamchagua wanavyozidi kumghasi ndivyo wanavyo zidisha hasira za wapiga kura wake na wasio wapiga kura.

Polisi imwache Lema afanye kazi zake za kisiasa huru bila kumbugudhi, bila hivyo matukio ya virungu yanaanza kuzoeleka na JWTZ hawako tayari kuuwa raia walioapa kuwalinda.
 
Mtafanya nini nyie waoga wakubwa, juzi tu mlikimbia kama panya, kama mlikuwa wanaume wa kweli basi kwanini msipambane na hao unao waita mbwa wa JK? Hii ni kawaida yenu, kelele nyingi hapa JF lakini hamna lolote.

Acha ushabiki wewe, hebu soma tamko la Polisi

Tamko la Polisi
Jeshi la polisi mkoani Arusha, jana lilitoa tamko kuhusiana na mbunge huyo kufikishwa mahakamani na kupewa dhamana kuwa halitarajii kuwapo kwa vurugu.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema wanatarajia kuwa leo baada ya Lema kupewa dhamana hakutakuwa na jambo ambalo si la kawaida na ataondoka mahakamani bila matatizo.

Alipotakiwa kuelezea kama watawatawanya wafuasi wa Chadema endapo wataamua kumsindikiza kwa miguu mbunge huyo kama ilivyotangazwa alisema hawezi kuzungumzia hatua zitakazochukuliwa kabla ya kosa kutendeka.

"Ngoja tuone kesho (leo) hali itakuwaje, siwezi kusema leo kama tutawatawanya au la. Ila sisi tunaamini mbunge akipewa dhamana ataondoka mahakamani kama kawaida ya watuhumiwa wengine bila vurugu," alisema Mpwapwa.Hata hivyo, ilielezwa kuwa polisi na baadhi ya viongozi wa Chadema walifanya mazungumzo ili kuhakikisha Jiji la Arusha linakuwa shwari mara baada ya Lema kupata dhamana leo.

Kamanda Mpwapwa alisema jeshi hilo halina nia ya kukabiliana au kujenga uhasama na wafuasia wa chama chochote cha siasa kikiwemo Chadema pale wanapofanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, lakini alionya kuwa hawatasita kudhibiti uvunjifu wowote wa amani na utulivu unaofanywa na mtu, kundi au chama chochote cha siasa.

Jiji la Arusha limekuwa likigubikwa na vurugu za kisiasa mara kwa mara tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ambao pamoja na mambo mengine, uliacha majeraha yanayotokana na matokeo ya uchaguzi wa umeya ambayo Chadema kimekuwa kikiyapinga.
 
Matatizo yote ya Arusha yamesababishwa na tabia ya serikali yetu kutozingatia sheria. Halafu tunaambiwa Chief Justice wetu anatafuta nafasi kule ICC! Tusubiri leo tuone kama mahakama itaendeleza siasa au watafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom