J'tatu hiyooo, Lema njeeee....

Unapaswa kuelewa kuwa Lema alikataa dhamana kwa kutafuta sifa. Hana uwezo wa kusimamia msimamo wake.
 
Ondoa magamba yako hapa
Mbassa jamaa kajenga hoja na wewe unatakiwa kujibu kwa kujenga hoja, unaposema 'Ondoa magamba yako hapa' una maana gani? Sishangai lakini ni Jumatatu na weekend huwa ina mambo mengi, inawezekana umeamka nazo.
 
Naomba nikunuu "baadhi ya wanachama wa chadema walimfananisha na Mandela lakini mandela hakulilia dhamana kama Lema!" "je alikuwa na dhamira ya kweli kutaka kuwakomboa wanachama wake? au alikuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa? je Lema anaweza kufananishwa na Mandela hata chembe?""....nimependa hoja yako kwa asilimia kadhaa but naona inaupande ambao ni kishabiki zaidi,na co kwa maslah ya sisi na vizazi vijavyo,asubuh njema.mi napita tu..
 
Alikuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa..matokeo yake kaumbuka!
sasa hivi kila mtu anamuona kama punguani flan hivi!
 
hahaah...lol!
akitoka si yule tena tunayemfahamu!.... atakuwa na mentality nyingine! si unajua tena wazee wa kazi hawakuachi hivi hivi?
Hahaha, sasa CDM ndio watakuwa wametekeleza matakwa ya waingereza.

Waliamua kumpeleka kijana wao course huko lupango
 
Lema hana uwezo wa kusimamia msimamo wake, agomee dhamana tena! ki..ro kilichomkuta nasikia haja kubwa inampita bila break.
 
  • Thanks
Reactions: Omr
Shujaa gani mrebo tu yule,tuulizeni sisi tunaemjua,ni mlimbwende tu,halafu habari nilizosokia wamemnanihii kule gerezani sasa amenogewa hataki kutoka

Wewe gamba! Fikiri kwa ku2mia kichwa nyambavu wewe! Acha mambo yako ya ugamba mpk leo na uwe hata na aibu.
 
Alikuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa..matokeo yake kaumbuka!
sasa hivi kila mtu anamuona kama punguani flan hivi!

huyu jamaa huwa anafanya kabla ya kufikiria.

Alijua kuwa kukataa dhamana ni njia nzuri ya kuteka hadhira. Usanii mtupu.
 
Asipotoka leo basi tumpelekee jiko awapikie wazee wa kazi.

nashauri kama akitoka apelekwe hospital kwa wataalam wa saikoloji wamtibu. Najua atakuwa amekuwa ameathirika kisaikoloji.
 
Kama ni umarufu kasha upata na mwanasiasa yeyote asiye marufu si mwana siasa upo sasa sikiliza miziki wa leo arusha potachimbika mandamano ya kufa mtu ole kwa mbwa wa jk wakibweka tu watakwenda na maji
 
mbunge wa Arusha mjini Godbless leo ataletwa mahakani kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili pamoja na wanachama wenzake 25 ambapo baadhi walipata dhamana lakini mh Lema aligomea dhamana yake na kudai kesi hiyo ifutwe, baadhi ya wanachama wa chadema walimfananisha na Mandela lakini mandela hakulilia dhamana kama Lema! yeye alisimamia Msimamo wake, je? ikiwa Lema atapewa dhamana leo bila kesi kufutwa itakuwa amesimamia Msimamo? au ameshindwa kuvumilia dhiki, shida, tabu, misukosuko, kulala saa 9, huko gereza la kisongo, je alikuwa na dhamira ya kweli kutaka kuwakomboa wanachama wake? au alikuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa? je Lema anaweza kufananishwa na Mandela hata chembe?

Mapokezi ya Lema kutetemesha Arusha

KUTOKA GEREZANI KISONGO LEO, POLISI WASEMA USALAMA WA RAIA KWANZA
Mussa Juma na Peter Saramba, Arusha
JIJI la Arusha na viunga vyake leo linatarajiwa kujaa shamrashamra za kumpokea Mbunge wake, Godbless Lema anayetarajiwa kurejea uraiani kutoka mahabusu Gereza Kuu la Kisongo alikokwenda kwa hiari yake kupinga kile alichokiita manyanyaso ya jeshi la polisi dhidi yake na kuonyesha ujasiri wa kutoogopa jela.Oktoba 31, mwaka huu, Lema na wenzake 18 walifikishwa mahakamani wakidaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali na kukaidi amri ya polisi iliyowataka watawanyike yeye na wenzake.Walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kudhaminiwa lakini Lema akikataa dhamana akisema ameamua kutangulia gerezani kudhihirisha kwamba haogopi gereza.

Jana, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Mkoa wa Arusha Ephatah Nanyaro alisema Lema atapokewa na wafuasi wake kuanzia eneo la mahakama na watatembea kwa miguu hadi sehemu maalumu aliyopangiwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na wapiga kura wake.

“Tunaliomba jeshi la polisi lisitafsiri mapokezi haya kama maandamano. Hatukusudii kuandamana. Tutakachofanya ni kumpokea mbunge na shujaa wetu na tutadhibiti ulinzi na usalama wetu wenyewe ingawa pia hatutakaa ulinzi wa polisi ambayo ni haki yetu kikatiba kama raia wema na walipa kodi wa nchi hii,” alisema Nanyaro.

Alipoamua kwenda gerezani Lema alisema: “Leo nimeamua kwa hiari yangu kutangulia magereza. Watakaotubeza tuwasamehe kwa sababu wanahitaji ukombozi wa kifikra. Watakaotuunga mkono na kutuhurumia tuwafundishe ujasiri wa kutoogopa jela wala magereza katika mapambano ya kutafuta haki, uhuru na utu wa mwanadamu,” alikaririwa Lema katika waraka alioutoa kwa wafuasi wake
siku alipokwenda mahabusu.

Uamuzi huo wa Lema ulifuatiwa na mtiririko wa matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani katika jiji hilo muhimu kwa shughuli za utalii, ikiwamo mgomo wa daladala na pikipiki.

Waraka wa kuhamasisha mgomo huo ulioandaliwa na kusambazwa na watu wasiojulikana ulidai kuwa pia ulikusudiwa kumpinga Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji anayedaiwa kukejeli baadhi ya watu. Hata hivyo, mgomo huo ulioanza saa 2:00 asubuhi na kudumu kwa saa tatu, ulidhibitiwa na polisi huku watu zaidi ya 30 wakitiwa mbaroni, kati yao 25 walifikishwa mahakamani.

Baada ya tukio hilo, hamaki kubwa ilitokea Oktoba 7, mwaka huu baada ya mahakama kugoma kutoa hati ya kumtoa Lema gerezani ili kukamilisha masharti ya dhamana iliyotolewa na Hakimu Judith Kamara, kitendo kilichosababisha kukamatwa kwa viongozi wa kitaifa wa Chadema akiwamo Katibu Mkuu, Dk Willibroad Slaa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe baada ya Jeshi la Polisi kufanya operesheni ya kushtukiza kuwatawanya pamoja na wafuasi wao waliokuwa wamepiga kambi kwenye Uwanja wa NMC Unga Limited.

Hivi sasa Mbowe, Dk Slaa na watu wengine 26 wanakabiliwa na kesi mahakamani kuhusiana na mkesha huo na kufanya idadi ya kesi zilizofunguliwa dhidi ya viongozi na wanachama wa Chadema tangu kuanza kwa mgogoro wa Arusha mapema mwaka huu, kufikia Sita.

Tamko la Polisi
Jeshi la polisi mkoani Arusha, jana lilitoa tamko kuhusiana na mbunge huyo kufikishwa mahakamani na kupewa dhamana kuwa halitarajii kuwapo kwa vurugu.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema wanatarajia kuwa leo baada ya Lema kupewa dhamana hakutakuwa na jambo ambalo si la kawaida na ataondoka mahakamani bila matatizo.

Alipotakiwa kuelezea kama watawatawanya wafuasi wa Chadema endapo wataamua kumsindikiza kwa miguu mbunge huyo kama ilivyotangazwa alisema hawezi kuzungumzia hatua zitakazochukuliwa kabla ya kosa kutendeka.

“Ngoja tuone kesho (leo) hali itakuwaje, siwezi kusema leo kama tutawatawanya au la. Ila sisi tunaamini mbunge akipewa dhamana ataondoka mahakamani kama kawaida ya watuhumiwa wengine bila vurugu,” alisema Mpwapwa.Hata hivyo, ilielezwa kuwa polisi na baadhi ya viongozi wa Chadema walifanya mazungumzo ili kuhakikisha Jiji la Arusha linakuwa shwari mara baada ya Lema kupata dhamana leo.

Kamanda Mpwapwa alisema jeshi hilo halina nia ya kukabiliana au kujenga uhasama na wafuasia wa chama chochote cha siasa kikiwemo Chadema pale wanapofanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, lakini alionya kuwa hawatasita kudhibiti uvunjifu wowote wa amani na utulivu unaofanywa na mtu, kundi au chama chochote cha siasa.

Jiji la Arusha limekuwa likigubikwa na vurugu za kisiasa mara kwa mara tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ambao pamoja na mambo mengine, uliacha majeraha yanayotokana na matokeo ya uchaguzi wa umeya ambayo Chadema kimekuwa kikiyapinga.

Jana kuna thread moja humu JF eti Arusha wanataka kujitenga kisa Lema kanyimwa dhamana akili za ukwaju kabisa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom