Joshua Nassari ashambuliwa na kujeruhiwa huko Makuyuni, vurugu zatawala!

Status
Not open for further replies.
Kwa sasa nimeshikwa na kigugumuzi kisicho cha kawaida katika kuchangia yanayojilia katika uchaguzi huu mdogo. Hali kama ni hiyo kwa uchaguzi huu mdogo, Uchaguzi Mkuu ujao hali itakuwaje?

Tunatakiwa tujizatiti kwa confrontation za kinadharia na vitendo. Yaani kuiondoa CCM inakuwa hatari kuliko kumwondoa mkoloni. Hata iweje hakuna kurudi nyumba daima ni mbele
 
Ametoa taarifa sasaivi kwenye ukurasa wake wa face book kuwa damu nyingi zinamtoka imebidi arudi Arumeru.

Hii ndio TANZANIA
 
Chadema mnafanya haya kwa kuwa mnajuwa wa kumnyooshea kidole ni nani, mnataka kuaminisha watanzania kuwa ninyi mnaonewa ili mpate huruma ya wananchi huu ni uhuni unaopaswa kupingwa kw nguvu zote, kw nn kila ni nyinyi tuu .wenye kufikiri zaidi lazima wajiulize sana kuhusu hili.
 
Mbona hali ni mbaya kiasi hiki jamani!! Naamini ipo siku nchi hii tutapigana wenyewe kwa wenyewe.
 
Wana Jf,
Hali si shwari katika uchaguzi mdogovwa makuyuni, CCM wamevamia vituo vya kura, mawakala wa CHADEMA wamepigwa vibaya sana.

Kamanda Nassari naye kaumizwa vibaya sana.

Jamani watanzania tunaelekea wapi kwa hali hii?
Ee Mungu utusaidie sisi wanao!

taarifa za kimbeya na majungu hizi, hivi nyie wanachadema mnafanya hizi za propaganda uchwara kwa faida ya nani?? unaweza kutupa source na pictorial evidence ya huu uzushi wako?
 
weka taarifa iliyokamilika amepigwa akiwa kituo cha nini? alikuwa wapi na anafanya nini amepigwa na nani na kwa sababu gani?sio wote tuna access na wall yake ya facebook!!
 
Mkuu hujuwi kuwa chama chako cha chadema ndiyo chanzo cha vurugu kwani kipindi hakikuwepo vurugu zilikuwope.

Hoja yako DHAIFU kama kiongozi wa chama chako. cHADEMA ingefutwa kama kuna mahali kimekwenda kinyume na sheria na pia CHADEMA kipo kwa mujibu wa Sheria. CCM inachotaka ni commua competitor badala ya kumshinda kwa hoja na huu ndo mwanzo wa mabomu na tutaona viongozi wakiuawa kama kule Lebanoni.
 
Chadema mnafanya haya kwa kuwa mnajuwa wa kumnyooshea kidole ni nani, mnataka kuaminisha watanzania kuwa ninyi mnaonewa ili mpate huruma ya wananchi huu ni uhuni unaopaswa kupingwa kw nguvu zote, kw nn kila ni nyinyi tuu .wenye kufikiri zaidi lazima wajiulize sana kuhusu hili.

Wewe naona umeamua kujiondoa akili hivi mwembe na mchongoma upi ushambuliwa sana? ukipata jibu utaacha kuandika hiki ulichokiandika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom