OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 420
- 670
Kwa walio hata wasio wapenzi wa usomaji wa vitabu wanauwezekano mkubwa wa kuwa wamewasikia watu hawa
Kiuhalisia hawa ni watu wa kufikirika, ni wahusika katika riwaya mbali mbali.
Joram Kiango alikuwa ni muhusika katika vitabu vingi vya Ben Mtobwa, huku Willy Gamba akiwa ni muhusika katika vitabu vya Elvis Musiba
Joram Kiango na Willy Gamba wanafanana vitu vingi, kama wote walikuwa majasusi, tofauti ni kuwa Joram Kiango alikuwa ni jasusi wa kujitegemea huku Willy Gamba akiwa ni jasusi wa serikali.
Wamekuwa ni wahusika vinara kwenye riwaya Zaidi ya moja. Hawa ni tofauti na ngoswe, muhusika wa tamthiliya ya E. semzaba ambaye alitamba kwenye kitabu kimoja tu. Joram kiango yupo kwenye vitabu kama Lazima ufe, tutarudi na roho zetu, mikononi mwa nunda, nk, Wiily Gamba ametokea katika vitabu kama Hofu, Kikosi cha kisasi, njama nk
Tabia ya waandishi kuwapa umaarufu wahusika ipo hata kwenye baadhi ya riwaya za waandishi wan je, kama Prof. Longdon kwenye riwaya za Dan Brown