John Rambo: First Blood 1982

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
700
Habari kwa wana 'JF'

Niende moja kwa moja kwenye uzi, baada ya kupita muda bila kutazama movies za zamani nikajipa muda kwa siku za mwisho wa wiki kuanza kutazama hizo movies moja moja kadiri muda utakaponiruhusu.

images (3).jpeg


Nilianza na hii "First Blood" ya Sylvester Stallone.

images (2).jpeg


Stori ipo hivi:
John Rambo akiwa kama mwanajeshi pekee aliyebakia kwenye vita ya Marekani na Vietnam anarudi nchini Marekani na lengo lake ni kuanza maisha mapya. Katika kujifikiria anataka kufikia kwa rafiki yake ambaye naye alifariki kitambo mno.

Nikiimalizia utashindwa kuitafuta 🍟
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    13.2 KB · Views: 7
Kiuhalisia inaonekana nchi ya Marekani ipo tayari kutumia mabilioni ya pesa kuukataa ukweli kwamba walishindwa na nchi ya Vietnam. Hata baada ya kuiangalia hii movie ya First Blood nimegundua ni muvi ambayo imejaa propaganda za Marekani dhidi ya nchi ya Vietnam.

Mazingira ya Vietnam yanaonekana mabovu (though inaweza kuwa hivyo) ila kwenye hii muvi ni kama yameongezewa makali. Ukiichunguza tena kwa makini utaona kwamba Mmarekani alikuwa akimshutumu Mrusi kuhusika kuipa nguvu nchi ya Vietnam (First Blood II, hapa inaonekana pale ambapo Rambo anapanda meli ndogo ambayo inamilikiwa na warusi wanaoongea ki-Vietnam).
 
Back
Top Bottom