Wewe unaishi tanzania ipi unajua chanzo chake kifo cha Kolimba siyo ajali wala cha kawaida(natural death) yale ni mauaji tena ya mchana kweupe.Ya Kolimba yalikuwa mauaji? Watendeeni haki waliofariki. Vinginevyo hata akina Chacha Wangwe, Mwalimu, yoote tutaita ni mauaji.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mh. Mwankenja ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa leo majira ya Nne na dk 10 nyumbani kwake Kiwira. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa marehemu Mwankenja alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
Wauaji walitoweka mara baada ya kukamilisha mauaji yao na kabla ya watu kukusanyika. Hadi sasa sababu za mauaji hayo hazijafahamika. Hata hivyo baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu usiku huu wanahofu mauaji hayo kuhusiana na masuala ya kisiasa.
Marehemu John Mwankenja
adui yako mpende, usilipe kisasi kwa kisasi. Mungu aifariji familia ya marehemu.amen!!!!!!!natabiri kuwa RPc atsema ifuatavyo kuhusu kifo cha marehemu nanukuru" kwa kuwa chadema juzi juzi tu walikuwepo hapa kwenye maandamano yao na moja ya hoja ambazo sugu alitoa ni kuwa viongozi wakija wazomewe na ikiwezekana wapigwe mawe, sasa wananchi wameamua kutumia risasi badala ya mawe" Mungu hawezi kumuhifadhi mahali pema peponi maana alikuwa mwizi, jambazi,mnafiki na fisadi, ushahidi.., kitendo tu cha kuwa mwanachama wa chama cha magamba ni ushahidi tosha
Mungu muadhibu zaidi huyo gamaba amina
Kuna maswali ya msingi kuna nini katika Halmashauri?Isije ikawa kaponzwa na misimamo yake kuhusiana na mambo fulani na mara nyingi ni mijifedha au miradi yenye utata!mimi sisemi konspirasi hapa lakini nataka kusema inakuaje hasa mtu anapigwa risasi nyumbani kwake.ni kuuawa tu sawa.kwanini?nakumbuka muda fulani aliwekewa ulinzi. Naanza hivi hii halmashauri ina kipato gani?inategemea nini.kulikuwa na kitu gan i mezani kwa mheshimiwa huyu?
haya yangu manenolakini
poleni wafiwa na wanarungwe kwa ujumla. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.