mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 821
- 1,343
Watu wawili Wakazi wa mtaa wa Majengo, kata ya Vingunguti, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam wamefariki baada ya kupigwa risasi jioni ya Jumatano, Desemba 27.2023. Akizungumza na Jambo TV leo, Ijumaa Desemba 29.2023 Kaka wa mmoja wa marehemu hao aliyejitambulisha kwa jina la Omari Shomari ambaye anadai kushuhudia 'ndugu zake' wakipigwa risasi amesema baada ya watenda kuwajeruhi marehemu hao awali waliondoka nao kwenye gari bila ndugu kujua watu hao ni kina nani na wamewapeleka wapi.
Hata hivyo hisia za awali za ndugu zilidhani ni Maafisa wa Polisi, hivyo kuchukua hatua ya kufuatilia kwenye vituo kadhaa vya Polisi na baadhi ya Hospitali bila mafanikio, kabla ya siku iliyofuata (Alhamisi, Desemba 28.2023) kupokea taarifa kuwa ndugu zao wamefariki na miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Amana; Jambo TV inaendelea kufuatilia zaidi kuhusiana na tukio hili, ikiwemo kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam
Chanzo: Jambo TV
View: https://x.com/jambotv_/status/1740760090917863855?s=46&t=oRmMsM7qro-rKCtBSefuig