Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 914
- 4,264
Katika interview ambazo zilikuwa na maswali marahisi kwa mtu neutral lakini maswali magumu kwa mwanasiasa ni interview ya juzi Clouds kati ya Mnyika na wanahabari wa chombo hiki.
Lakini kati ya story zote zilizojitokeza unamwona Mnyika akichambua na kujibu maswali na hoja zote kiuhalisia bila kuzua mjadala kuhusu uhalali wa majibu yako. Hakuna majibu yakupika
Lakini eneo la pili anaonekana wazi siyo mwanasiasa bali ni binadamu mwenye uwezo na ufahamu sahihi kuhusu mahitaji ya Dunia kabla,sasa na baadaye. Anatambua wazi kwamba CHADEMA siyo nchi bali ni chama cha siasa kilichoundwa kukidhi matakwa ya mfumo wa kisiasa na kwamba kupitia taasisi hii upo uwezekano mkubwa wa binadamu waliopo ndani kupishana kimtazamo.
Mfano mzuri ni pale alipokiri kwamba yeye binafsi alikataa kumpokea Lowasa, lakini mwisho akaona kiu ya kisiasa ya kuiondoa CCM madarakani iliyokuwa ndani ya watu walio wengi na hapo ndipo alikubali kuendelea kutokukubaliana na msimamo wa chama kuhusu aina ya mgombea wao lakini akaamua kuunga mkono maono ya wananchi ya kuiondoa CCM madarakani.
Tafsiri kubwa hapa anatuambia si chadema wala CCM wanaoweza kuitoa nchi hapa ilipokwama isipokuwa watanzania kuamua kuunda mfumo wa kikatiba unaotoa haki na unaosimamia nidhamu ya kisiasa na serikali. Incase tukipata mfumo sahihi wa kikatiba may be tunaweza kufuata mfumo wa Kenya ambapo ikifika uchaguzi zinaundwa pande mbili let say UPANDE YANGA NA UPANDE WA SIMBA AU NG'OMBE NA MBUZI AU KUSHOTO NA KULIA THEN MNAUZA SERA WANANCHI WANACHAGUA.
Maono ya Mnyika yanatufumbua macho kwamba tuache imani kwa chama tubaki na imani ya nchi. Kenya wanapiga hatua kwa sababu hakuna akili zinazosubiri kuwa chawa zipewe nafasi....kila nafasi inamgumo wa ushindani.
Lakini jambo la mwisho kuhusu John Mnyika ni uwezo wake wakusimama kama Katibu mkuu na chama kubaki imara kipindi cha JPM. Kusimama imara kutetea chama dhidi ya waovu wa tume ya uchaguzi ambao walifikia hatua yakughushi nyaraka na kuzipeleka Bungeni.......Mnyika amesema wazi kwamba Tume ya Uchaguzi haijawahi kuonyesha popote barua yakuwapitsha akina Mdee iliyodaiwa kutolewa na Chadema. Maana yake anakiri kwamba pamoja na mawimbi mazito alisimama kama katibu mkuu na itoshe kusema kwamba huyu ndiye katibu mkuu bora kuwahi kutokea baada ya Mzee Kinana na Dr. Slaa. Katika mazingira ya kawaida, Mbowe alifahamu msimamo wa Mnyika dhidi ya Lowasa lakini alidiriki kumpendekeza kuwa katibu mkuu jambo ambalo siyo dogo. Uvumilivu wake ungekuwa mdogo angeungana na Slaa na matokeo yake angekuwa ameshapoteza dira kisiasa au ni DC kama walivyo akina Nassary, Mashinji nk
Natamani atunukiwe nishani ya utumishi uliotukuka