ngalikikinakiki
Member
- Mar 29, 2011
- 55
- 18
Kati ya wanamuziki ambao wananishangaza ni John Kitime, ameweza kuwa na blog za muziki ambazo zina taarifa nyingi ambazo zingekuwa mali sana kama wanamuziki wenzie wangweza kuzisoma lakini naona hazijapata promotion zinazofaa. Kuna hii blog www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com ina picha za kihistoria za muziki wa Tanzania, ni darasa kubwa sana kwa wanamuziki na wadau wa muziki wa Tanzania. www.musicintanzania.blogspot.com ina picha za bendi mbalimbali zikiwa kazini, nyingi za hizi bendi huwa hazionekani kabisa katika vyombo vya habari vya kawaida, ya kawaida. Kuna hii ya www.johnkitime.blogspot.com ambayo inaongelea haki za wasanii nayo pia ni darasa kubwa kwa wenye kutaka kujua haki zao.