Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Pamoja na JK kuviita vyama vya upinzani ni "photocopy" ya CCM lakini nyendo zake zimenithibitishia ya kuwa yeye JK ndiyo "fotokopi" murua ya Dr. Slaa na huu ndiyo uthibitisho wake:-
a) Kila aliposikia Dr. Slaa amefunika kwenye mikutano yake JK amejibidiisha kwenda huko ili ajipime ubavu na Raisi mtarajiwa Dr. Slaa.
Mifano ni Mwanza, Arusha, Moshi na jana Mwembeyanga.
JK anaona kujinusuru ni kheri azingatie usemi usemao ...."fuata nyuki ule asali..." na hapo amenithibitishia ya kuwa yeye ni fotokopi ya Dr. Slaa kwa sababu hawezi kufanya lolote mpaka Dr. Slaa kwanza awe amelifanya............yaani JK ni mwigizaji mzuri wa Dr. Slaa...
b) CCM na hususani JK wamekuwa wakiimba ngonjera za ya kuwa elimu na afya bure haviwezekani lakini baada ya Dr. Slaa kuchanganua takwimu kwa kutumia zana nzito za upembuzi yakinifu na za kitalaamu .........JK amemwagiza Waziri wa Elimu Profesa Jumanne Maghembe kukubaliana na Dr. Slaa na Ilani ya uchaguzi ya Chadema ya kuwa elimu bwerere pia ni sera ya CCM ila Maghembe hajafafanua ni kwa nini haimo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM au hata mipango yake ya miaka kumi ijayo............Hili lathibitisha ya kuwa JK ni fotokopi ya Dr. Slaa.
c) CCM walisema midahalo "nuksi" hawaitaki kwa sababu waliyoyafanya ni mengi na yanaonekana lakini baada ya Dr. Slaa kufanya mdahalo wake pale MOVENPICK Dar na kuwa na mafanikio makubwa kufikia hata makada wa CCM kupagawa na kudai watampigia kura kimyakimya Dr. Slaa..... JK naye akazinduka na kuja juu ya kuwa atafanya mdahalo wake kesho.............Hivi sasa ni nani kati ya JK na Dr. Slaa ni fotokopi wa mwenzie? Jibu lipo wazi JK amefilisika kisiasa na sasa hivi anasubiri rubani wetu Dr. Slaa amwonyeshe njia ya kupita........Na katika mazingira haya kumchagua kipofu JK inahitaji uwe mwehu kidogo vinginevyo huwezi kupoteza muda wako hata chembe kwa kiongozi haramu.
Fikiria CCM imewanyima wagombea wake wa ubunge na udiwani kutojinadi kwenye midahalo lakini kwa vile JK sasa anasoteshwa na Dr. Slaa sasa ameona..... "Kheri nusu ya shari kuliko shari kamili" ......pale alipojisalimisha kwenye mdahalo wa waandishi wa habari..........
d) Mwaka 2005 Chadema ndiyo walioanza kutumia helikopta na CCM iliwabeza kuwa wanapenda ufahari na ya kuwa Chadema watayajuaje matatizo ya wananchi wakiwa angani? JK na CCM yake mwaka 2010 imewaigiza Chadema kwa kuwa na helkopta tena siyo moja ila tatu...Hivi ni nani fotokopi wa mwenzie?
e) Baada ya kuona umaarufu wake unapimwa na mahudhurio kwenye kadamnasi za mikutano ya Dr. Slaa, JK na CCM wakaona ni kheri wachakachue mahudhurio kwa kuhamisha watu kwa malori na mabasi kutoka maeneo yasiyohusika lili mradi waweze kujilinganisha na mikutano ya Dr. Slaa kwa idadi ya mahudhurio..............Huu ni ushahidi mwingine ya kuwa JK na CCM ni fotokopi wa Dr. Slaa....
Upo ushahidi mwingi lakini kwa leo huu unatosha......ya kuwa JK ni fotokopi ya Dr. Slaa na aache kupotosha wananchi kuwa vyama vya upinzani ni fotokopi ya CCM wakati yeye mwenyewe amethibitika ni fotokopi ya Dr. Slaa na Chadema........