JK futa uraia wa Dr Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika, Lema, Pengo na Shivji ili Taifa litawalike!

Status
Not open for further replies.
Huu uhuru wa kila mtu kusema mawazo yake unasababisha wengine wafikirie kwa mfumo wa anticlockwise wakati wengine wanakwenda kwa mfumo wa clockwise!

Bila shaka haya ni matokeo ya pilau la krismasi. Kheri ya krismas godwin!

kaka ukiona watu tunakula pilau ujue ndio maisha bora aliyosema jk. lakini kwanini wakuu wa chama chako wanasababisha serikali kushindwa kupanga mambo ya maendeleo? hiyo sio siasa japo wangengoja 2014 lakini wao peoples power kama tuna kampeni sasa , pinda kashawaambia waache maandamano na mashinikizo kwani wanayumbisha nchi wao wanazidisha.Ndio maana njia pekee kwa JK ni kufuta uraia wa watu ao
 
rais anayo mamlaka ya kumwondoa mtu ndani ya nchi kwasababu za usalama wa nchi. kama ikionekana mtu huyo anahatarisha usalama wa taifa

Hivi wewe ukifukuzwa hapa utaenda wapi? Au unaandika pamoja na viroba vya x mass!
 
watanzania waliomkataa JK na ambao hawamkubali mpaka sasa ni zaidi ya 75% ya watanzania wote kama ananataka atawale atakavyo basi awafutie uraia wao wote hawa
 
Awafukuze wazalendo wa kweli nchi hii, ili walowezi akina Rostam, Bakhresa, Jitu Patel, Tanil Somaiya waendelee kutesa nchii?
Kweli Mungu ana watu wengi sana, baadhi yao Wapumbavu ambaye mmojawapo ni wewe!
 
rais anayo mamlaka ya kumwondoa mtu ndani ya nchi kwasababu za usalama wa nchi. kama ikionekana mtu huyo anahatarisha usalama wa taifa

Anayo mamlaka kama ulivyosema, lakini kwakuwa amechukiwa na wengi, awaondoe watanzania wote abaki yeye na mke wake!
 
Mwisho wenu umekaribia nyie wezi ndio maana hofu zinakujaeni sana,subirini tu mtatafuta urai nchi nyingine bila kupenda na ndio maana hofu imekua kubwa miongoni mwenu,ati Uhamishoni! uharo mtupu
 
Hoja si kwamba JK amfukuze nani na nani ili inchi itawalike. Hoja ni kwamba JK aondoke madarakani apishe uchaguzi huru ufanyike. JK hakuwa chaguo la Watz wengi bali alikuwa chaguo la Tume ya uchaguzi aliyoiunda yeye mwenyewe pamoja CCM yake. Kama ni kuondoka madarakani aondoke tu haidhuru!
 
kaka ukiona watu tunakula pilau ujue ndio maisha bora aliyosema jk.

lakini kwanini wakuu wa chama chako wanasababisha serikali kushindwa kupanga mambo ya maendeleo?

Kweli wanaccm akili zao wote sawa! Yaani unafikiri pilau ndio maendeleo!? Lazima utakuwa mlevi wa gongo ya kinyesi! Mwezio alisema foleni ni maendeleo wewe leo unasema ni pilau! Nyie ndio mnaohongwa pilau na maandazi kuipigia kura ccm! Upuuzi mtupu!

Sasa unataka viongozi wa upinzani wapange mipango ya maendeleo gani wakati umeshapata pilau!? Hiyo kwako si ndio maendeleo!?
 
Kutokana na rais kuwa katika mashinikizo makubwa toka kwa watu na taasisi zinazoongozwa na watu ao ni vema ukafuta uraia wa waliotaja hapo juu ili nchi itulie na shughuli za maendeleo ya taifa zifanyike la sivyo mh rais utawala wako utadondoka kabla ya muda wake.

Wafalme wa ugiriki waliwai kuwaua wanafalsafa waliokuwa wanayumbisha tawala zao lakini mimi sikushauri uwaue bali wafukuze nchini kama nyerere alivyomfukuza kambona au karume alivyomfukuza ibrahimu babu.

baada ya kufanya hivyo nchi itakuwa imetulia na hutakuwa na magonjwa ya moyo

masabur at work.
Afukuze watz wote,nadhan ataweza zaid kuongoza wanyamapori.
 
kaka ukiona watu tunakula pilau ujue ndio maisha bora aliyosema jk. lakini kwanini wakuu wa chama chako wanasababisha serikali kushindwa kupanga mambo ya maendeleo? hiyo sio siasa japo wangengoja 2014 lakini wao peoples power kama tuna kampeni sasa , pinda kashawaambia waache maandamano na mashinikizo kwani wanayumbisha nchi wao wanazidisha.Ndio maana njia pekee kwa JK ni kufuta uraia wa watu ao

Mkuu,kumbe u sirias?
Nenda kapige x ray kichwani,kama una ubongo,uje tuendelee.
 
Haya mazungumzo nimeyasikia kwenye muhadhara Fulani huku Bagamoyo kumbe wale wazee wako serious na huu upupu sasa uko JF
 
@MUNGI & FILIPO
Inawezekana mnamitazamo tofauti na jamii na maslahi ya taifa lakini jaribuni kuficha hisia zenu za kutukana na kudhani ndio mmefikisha ujumbe, Inawezekana mada hii ikawa nzito zaidi ya nyinyi mnavyotaka kudhani, anyway ni mitazamo yenu lakini ikifika wakati ambapo unadhani kuokoa wengi ni kutosa wachache nje ya jahazi ni wakati huu sasa.

Ukiona jahazi linataka kuzama na baharia anakutazama ujue anataka kukwambia kuokoka ni kutosa mizigo, na jahazi la Tanzania linazama na wakati wa kutosa wazamishaji ni Leo na si kesho
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hoja si kwamba JK amfukuze nani na nani ili inchi itawalike. Hoja ni kwamba JK aondoke madarakani apishe uchaguzi huru ufanyike. JK hakuwa chaguo la Watz wengi bali alikuwa chaguo la Tume ya uchaguzi aliyoiunda yeye mwenyewe pamoja CCM yake. Kama ni kuondoka madarakani aondoke tu haidhuru!

pamoja na chaguo la MUNGU wa KILAINI!
 
kikwete anahatarisha vipi usalama wa Taifa wakati yeye ndiyo namba moja katika kulinda usalama wa nchi?

...Ingekuwa hivyo basi nchi yetu isingekuwa katika hali mbaya kama ilivyo sasa. Wengi walidhani ni "chaguo la Mungu" kumbe ni chaguo la mafisadi. Kuwepo kwake madarakani kunaiangamiza nchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom