JK apigiwa magoti na Foreign Minister wa Malawi!!



jamani kila binadamu hupenda kusifiwa mtu ukioan watu wanaonyesha kukusifu hapo nilazima ufurahi! ukiona watu wanatambua ukuu wako lazima ufurahie!
mie simlaumu kwa hilo!
 
huu ni utumwa wa kiafrica SIONI sababu yoyoteya mwanamke WA KIAFRICA kumpigia mtu yoyote magoti. NASEMA HUU NI UTUMWA NA IBABIDI UKEMEWE

Wewe ndio wale wasiopenda utamaduni wa kwao bali hushabikia kwa wengine. Pengine hapo ulipo unashabikia ushoga na usagaji.
 
:frusty::frusty::smash::smash:Unacceptable, shame, kneeling is not sign of displine or obedience, this is slavery with the world we have now.:A S 114::A S 114::ranger::ranger: let me drive away:car:

Kwa mnaotoka Kilimanjaro lazima muone ajabu maana huko mwanamke hata anapomsalimia mkwe anasisimama kama mlingoti!, lakini lazima mjue kuheshimu uafrica wenu sio kuiga vya wazungu tu. Kuna mwanasayansi mmoja wa kizungu alishasema waafrica kazi yao ni kuiga iga tu, ona sasa jinsi wazungu wanavyotutukana. Kutokuwa na utamaduni wa kukutambulisha napo ni mapungufu. Kwa kabila langu hata mwanaume, kwa mfano, anapomsalimia mkwe lazima ainame kidogo.
 
mie mume wangu akiwa mpole nitakuwa namsalimia kwa hivyo ila akiwa mkali mkali hivi asahau...:whoo:
 
huo ndio utumwa wenyewe ninaoupinga .....kuna haja gani ya mwanamke kupigia mwanaume magoti? si kama ukeketaji tu huu?
Tuko pamoja mkuu, watu wanapenda sana kujifanya miungu ati kwa kisingizio cha tamaduni zetu.
 
huyu jamaa bonge la tyranny, ningekuwa ni mimi nisingemruhusu afike kwenye floor. shame..... So pernicious!!!!!
 
Kwa mnaotoka Kilimanjaro lazima muone ajabu maana huko mwanamke hata anapomsalimia mkwe anasisimama kama mlingoti!, lakini lazima mjue kuheshimu uafrica wenu sio kuiga vya wazungu tu. Kuna mwanasayansi mmoja wa kizungu alishasema waafrica kazi yao ni kuiga iga tu, ona sasa jinsi wazungu wanavyotutukana. Kutokuwa na utamaduni wa kukutambulisha napo ni mapungufu. Kwa kabila langu hata mwanaume, kwa mfano, anapomsalimia mkwe lazima ainame kidogo.




haki za binadam lazima iingilie kati
 
ni kweli nimekupa thanx.

Halafu jamaa anafurahia kuabudiwa nini?

hizi ni mila zetu waafrika ambazo mimi nitazipigania mpaka kiama.
Ni mila ya ambazo zinamfanya mwanamke wa kiafrika awe mwenye heshima na kuwajibika. Kama mama huyu mzuri wa kiafrika. Mabinti wadogo wakiona mfano huu, kwa kweli watajifunza vitu vizuri vingi.
Ni mila zetu ambazo zilipunguza talaka katika ndoa, zilipunguza watoto wanaoishi mazingira magumu kwa sababu ya talaka za wazazi wao.
Kuzitupa mila hizi kumetusababishia maafa makubwa kama talaka, watoto kuzagaa mitaani n.k.
 
mila na desturi inabidi ziheshimiwe watu wasijifanye kwa vile ni mawaziri basi ni kusimama mlingoti kutoa salamu hiyo namsifu sana huyu mama!
 
Tunaoijua Malawi toka enzi za Ngwazi Kamuzu Banda hatushangai hayo kwa JK leo!
 
Mkuu wa kaya anaonekana yuko very Bossy, very comfortable na mama kumpigia magoti na anafurahia hicho kitendo, nadhani anatamani amwambie rudia tena, maana hiyo heshima kuipata ni kwa nadra sana siku hizi, akirudi bongo wananchi ndo wanampotezea kabisa mpaka nafsi inamsuta anashindwa kutoa hotuba kwa wananchi kwenye siku maalumu.
 
Safi kabisa!Tujivunie vilivyo vyetu.Alichofanya huyu mama ni sehemu tu ya utamaduni wa jamii nyingi za kiafrika.Hakuna udhalilishwaji wowote wa mwanamke hapo.Utamaduni ni dynamic kwa hiyo with time kama kupiga magoti litaonekana ni tatizo basi wanawake wataacha kabisa kufanya hivyo.Zamani mtoto ukimuamkia mkubwa lazima umshike kichwa lakini miaka hii watoto hawafanyi hivyo tena kwa hiyo haya mambo yanaenda na kubadilika na sidhani kuna tatizo lolote hapo.Heko mama!
 
Nionacho mimi ni heshima tu ya huyo mwanamke kama walivyo wanawake wengi wa kiafrika kwa waume zao au kwa watu waliowazidi umri au cheo.Inawezekana ikawa ni mfano mbaya kwa yeye kumpigia magoti JK ila ingekuwa kwa mfalme MSWATI sidhani kama watu wangechangia kwa kiasi hiki nilichoona maana kule utamaduni bado unatumika na kuheshimika.
Jamani mwanamke katimiza wajibu wake na sisi tutimize wetu kwa kuheshimu mila za watu wengine hata kama zinakandamiza ila kwangu mimi kupiga magoti si ukandamizaji bali ni utaratibu tu sawa na kuinama,kupeana mikono na hata kuchuchumaa.
 
Back
Top Bottom