JK Anapodhalilishwa hadharani

Ujinga uliopo ngeleja anaipumzikia wizara aliyopewa.anachofanya ni wizara kumtumikia na si kuitumikia ndipo tunapofikishana hapa
 
Jamani tusishabikie hata kidogo mwenendo wa huyu JM manake ni picha mbaya sana kwa vijana kisiasa japo what goes around comes around,anafikiri na kuona kwa mtazamo wake kuwa kwa kuwa ameshakuwa na mausiano na wakubwa kidplomasia na wafanya biashara wanasiasa ambao wanamwambia JK ana lolote dogo kaamua kumpandia kichwani kiana Msure huyo huku akilenga kumuonyesha kuwa hana lolote katika utawala ukizingatia kuwa alikuwa ndie mwandishi wa hotuba za Rais,ufahamu wake kwenye mambo mengi ya Nchi,kwa kuwa inabidi awe anaccess ya information nyingi kuhusu Nchi aweze kujua malengo ya hotuba yawezwe kuelekezwa wapi kulingana na matakwa ya hotuba husika.

Yote hayo kwa kuwa KIJANA HANA NIDHAMU imemgeuka Mzee aliyejaribu kumkuza,na kuitilafiana kwa tofauti za baba yake kiutendaji nae kazichukua kuziweka kichwani,ukiunganisha na kukosa uwaziri huku ndani yake akijua kuwa kuna mawaziri ana hakika anawazidi kiupeo na uelewa wa mambo basi imekuwa shida tupu.

Ukilejea na kama anajua Mheshimiwa fulani nae alishakuwa Mwandishi wa Hotuba za Rais wa Kwanza Mwalimu JK,na kuwa Mheshimiwa huyo baadae amekuja kuwa Rais wa awamu ya tatu ya Taifa hili,basi anafikiri kama jana kama kesho.Kamwe sio kuna tofauti kubwa sana kihaiba kati yake na BM, manake sidhani hata kama BM aliutaka URAIS,na ndio viongozi wazuri wanavyokuwa nahisi alifanya kushtukizwa tu kachukue form.

Kiongozi mzuri anganganii kuwa kiongozi bali ananganganizwa kuwa kiongozi kwa kuwa walioko nyuma yake wanajua anaweza kuwaongoza.Kibaya kilichotokea kwa BM ni kukubali kuingia kwenye mtego wa wajanja wanaotega mitego kila siku kuakikisha kuwa Viongozi na watu wenye dhamana wanaingia kwenye mtego wapate njia ya kuwacontrol kwa kivuli cha GUILT CONSCIOUS,kwa kiongozi husika hivyo wao kupata nafasi ya kupitisha mambo yao chini ya yale madudu walio muingiza nayo mkenge.Kianchowaponza viongozi wetu ni kutokusema,Mwalimu JK anasema kwa kikwao yaani kizanaki "Mubisa Kilerwe......."yaani "Mficha kidonda harufu itamuumbua".

Kwa kuwa dogo anategemea kupitia akili yake na connection alizonazo one day yes basi yeye Prezidar Bongo.Du mwana hapo sipo,kama umeshindwa kuwa na busara na mtu aliyekupa shavu,leo umma tukikabidhi KISU mwanangu hao kina Riz 1 watatafuta pa kwenda.Wakati Bongo tuanchoitaji unapotofautina na mtu unastep down una buy time,unasubili mwelewa mwingine akichukua kasi kama faili lako analo mezani anapima yaliyotokea, anapima ustaarabu wako wa kutoleleti mambo na utulivu wako wakati wa kukosa jambo la muhimu sana wakati unalihitaji most wewe kama wewe,lakini kwa kuwa linawahusika wengi ambao wanadetermine upatikanaje wake na kwa kuwa liko nje ya uwezo wako basi ilikupasa uwe mpole.

UNAFIKI,NA UNDUMILAKUWILI,NA KUUZA [KULOPOKA KWA WASIO HUSIKA ] MAFAILI [TAARIFA NYETI] kwa watu ambao unategemea wakupe support kwenye siasa za bongo haulipi kamwe.Zaidi wenye akili wanakukusanyia nguvu tena wanakusubilia kwenye kolasi.

Nilikuwa napenda sana kuona vijana kwenye siasa,lakini wawe ni Models wenye upeo na maono kwa faida ya madogo walio nyuma yao.Leo wasure [Watu wazima] wameshaharibu na dogo nae anataka kuleta hizo hizo wasure waliyoyatenda dogo simile hasira za umma dhidi ya mafisadi unazijua siku nawe wakikuhararishia kuwa your one of them I cant Imagine!!!!!!!!!!!!.
 
Duh!! This time around tutayasikia mengi, ngoja tuone vita vya mafahari wawili!!
 
Fuata hatua hizi, jifunze kuandika heading,body na conclusio then ndiyo utoke huko Bumbuli uje hapa Jf. Thread ilikuwa na mashiko but not well organized....!
 
Hii ni michezo tu ya siasa, kila anayempata kibonde wake anammaliza ila naogopa kitu kimoja kuwa Mkulu ndio amekua kibonde zaidi.....maana Waziri wake akipelekwapelekwa kiasi hicho ina maana hukuchagua mtu sahihi..........
 
Kwangu hata wapigane haina shida hata wauwane hainiiumi maana hakuna anyepigana kwa ajili ya maslahi ya watoto na wadogo zetu tuliowajengea makaburi na kuyaita shule za Kata......kule kunafanyika ngono, mimba, madawa na kila adha ya kila kitu halafu mshenzi mmoja juzi kwene TV anasema Tz inaongoza kuwa na wanafunzi wengi vyuo vikuu waliosoma shule za Kata!! Nilitamani kulia kabisa sooo hata wakichinjana haitaniuma hata kidogo, nchi imefikia pabaya, wao ni kuvaa suti na VX, V8 huku wakipandisha mafuta ya taaa, what the hell is this? tumewakosea nini watu hawa? Juzi nilikua kijiji kimoja Nyangao hukoooo Lindi, karibia machozi yanitoke, hawana chochote wakijuacho, mambo ni magumu, kisha uniambie kuna wapuuzi sijui wanaongea upumbavu gani bungeni hukooo, it pains brethren, kama unaipenda nchi yako itakuuma pia. God bless Us............Amen
 
January ni msaliti mkubwa na anatumwa na rachel kuvuruga nchi , msimwamini kabisa hata unapomuangalia anaonyesha hivyo. Kwa vile anatumwa na mafisadi naye ni fisadi, siri zake tunazo. Atuachie nchi yetu tulio wazalendo. Jm ulichofanya kule bumbuli si unafahamu mwenyewe. Mungu atakuhukumu usifikiri watz hawajui. Endelea lakini umma unakujua
Pamoja na hayo, january anataka uwaziri wa ngeleja, ndio maana amekuwa akimsakama sana na hadi kapeleka uthibitisho wa rushwa za ngeleja. Nadhani jk alimwambia akomae nae hadi ajiuzulu halafu ateuliwe yeye ili kukidhi kiu ya mafisadi.
 
Hivi ukiwapandishia bei ya mafuta ya taa hawa bibi zetu na babu zetu ambao kipato chao ni sifuri unataka waishije? si unatafuta laana za bure tu? kweli kabisa yaani mtu unakuja na wazo la kijinga namna hio ili uwapendezeshe akina fulani? No, kama ni rushwa basi ilichanganywa na dawa za kuwapumbaza, haiwezekani kwa mtu mwenye akili timamu kufanya maamuzi ya kitoto kiasi hik...............
 
January ni msaliti mkubwa na anatumwa na rachel kuvuruga nchi , msimwamini kabisa hata unapomuangalia anaonyesha hivyo. Kwa vile anatumwa na mafisadi naye ni fisadi, siri zake tunazo. Atuachie nchi yetu tulio wazalendo. Jm ulichofanya kule bumbuli si unafahamu mwenyewe. Mungu atakuhukumu usifikiri watz hawajui. Endelea lakini umma unakujua
Pamoja na hayo, january anataka uwaziri wa ngeleja, ndio maana amekuwa akimsakama sana na hadi kapeleka uthibitisho wa rushwa za ngeleja. Nadhani jk alimwambia akomae nae hadi ajiuzulu halafu ateuliwe yeye ili kukidhi kiu ya mafisadi.
 
Pamoja na hayo, january anataka uwaziri wa ngeleja, ndio maana amekuwa akimsakama sana na hadi kapeleka uthibitisho wa rushwa za ngeleja. Nadhani jk alimwambia akomae nae hadi ajiuzulu halafu ateuliwe yeye ili kukidhi kiu ya mafisadi.

Kumbe uwaziri unapatikana kihivyo?
 
NAONA HII HEADING NA CONTEXT ZIME DIFFER SIGNIFICANTLY. Muanzilishi atatusaidia kwa kutupa summary ya deliberations. This is sick
 
wakuu

Hivi vita ni kati ya Jairo na ngeleja

1.Jairo,seasonal security officer na mtu ambaye anataka awe on top kwenye issue zote za wizara kwa sasa..
2.Ngeleja ni mtu mjanja mjanja ambaye ametokea kupata madaraka na kupendwa na rais..na ana influence wizarani

Toka Jairo ahamie pale Nishati yeye na Ngeleja wamekuwa wakifitiniana sana ..inasemekana wao kwa wao hawaaminiani..

between the dot,JM na Jairo wamefanya kazi wote pale magogoni na waliondoka pamoja pale...hivyo wanajuana vyema

All in all hii ni battle ambayo sisi haituhusu kabisa,tunachotaka ni umeme wa uhakika..JM na Ngeleja wanatakiwa kutuambia mipango ya kujenga vyanzo vya umeme itakamilika lini na pesa watazitoa wapi...kama ni PPP tujue..siyo blah blah..umeme kwanza

again,JF has been credible since then..hivyo tuache kujadili watu na tukate issue..

I am down

Gembe!

wakuu
Hivi vita ni kati ya Jairo na ngeleja

1.Jairo,seasonal secuity officer na mtu ambaye anataka awe on top kwenye issue zote za wizara kwa sasa..
2.Ngeleja ni mtu mjanja mjanja ambaye ametokea kupata madaraka na kupendwa na rais..na ana influence wizarani

Toka Jairo ahamie pale Nishati yeye na Ngeleja wamekuwa wakifitiniana sana ..inasemekana wao kwa wao hawaaminiani..

between the dot,JM na Jairo wamefanya kazi wote pale magogoni na waliondoka pamoja pale...hivyo wanajuana vyema

All in all hii ni battle ambayo sisi haituhusu kabisa,tunachotaka ni umeme wa uhakika..JM na Ngeleja wanatakiwa kutuambia mipango ya kujenga vyanzo vya umeme itakamilika lini na pesa watazitoa wapi...kama ni PPP tujue..siyo blah blah..umeme kwanza

again,JF has been credible since then..hivyo tuache kujadili watu na tukate issue..

I am down

Gembe!

Tunashukuru kwa hilo, ingawa mimi bado sioni connectivity between the title head and contents in the thread
 
Kwa wale wanaofuatilia sakata la Umeme, majina mawili mtakuwa mnayafahamu vizuri sana. January Makamba na William Ngeleja. William Ngeleja ni Waziri aliyeteuliwa na Rais JK, na January Makamba ni kijana ambaye amewahi kumfanyia JK kazi, kama mwandishi wa hotuba. Baada ya JM kukosa uwaziri, aliahidi kuwafanyia wana bumbuli kazi waliyomtumia bungeni. Wengine wamemuita JM mnafiki na msaliti wengine wanamuona kama kijana mwenye ndoto kubwa

Kumekuwepo mvutano, wa vuta nikivute kati ya ngeleja na makamba Jr. Mara Barua, mara kukingiana kifua, mara rushwa. Haya yote kwa mtizamo wangu yanafanywa ili kuonyesha uwezo mdogo wa Bwana ngeleja katika wizara ya nishati na madini, na uwezo wa JK katika uteuzi wake wa mawaziri. Wachambuzi wengi wa kisiasa wamekuwa wakitoa lawama nyingi dhidi ya JM kwamba ni kibaraka wa mafisadi na mtu mwenye ubinafsi mkubwa. Lakini mwisho wa siku yote ni maneno, ila ujumbe mzito ni kwamba

1. Amedhiirisha wazi, na anaendelea kuudhiirishia umma kwamba JK hana uwezo wa kuiongoza nchi
2. Ameamua kumtumia taarifa JK kwamba nafasi yoyote anaweza kuipata bila usaidizi wake JK

nabado subirini
 
Kweli JK anastahili sifa kwa kuacha watu watapike kila wanapojisikia. Haya aliyoaandika humu yana uhusiano gani na JK. Hebu tupeni fursa ya kufikiria mengine siyo hoja zenye matege kama hizi.
 
Back
Top Bottom