Fikra mlazo
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 237
- 37
Habari nduguz. mwenye namna ya kuteblngeneza kalimati anielekeze pls. recipe nlopewa mara ya mwisho zilitoka nyembamba na zilinyonya sana mafuta, in short sikuzifurahia. Msaada tafadhali.
ndiyo.Kalmati si ndio maandaz ya kumimina?
Kalmati si ndio maandaz ya kumimina?
Habari nduguz. mwenye namna ya kuteblngeneza kalimati anielekeze pls. recipe nlopewa mara ya mwisho zilitoka nyembamba na zilinyonya sana mafuta, in short sikuzifurahia. Msaada tafadhali.
usiniambie sio hayo hahaha hebu mkuje mtuhabarishe hzo kalmati jamani lolNshakuitia mtaalamu wa kaimati Usijali
ShukriyaJaribu hii
Kaimati
Vipimo
Unga 2 vikombe vya chai
Hamira 1 ½ cha chai
Samli 1 kijiko cha chai
Maji 1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
Mafuta ya kukaangia kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
- Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
- Ziepue na zichuje mafuta.
Shira:
- Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia *Shira zikiwa tayari.
Sukari 3 vikombe
Maji 1 kikombe
Hiliki ¼ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 3-4 matone
Namna Ya Kutayarisha Shira
1.Tia sukari na maji katika kisufuria kidogo, acha kwenye moto ichemke pole pole hadi iwe nzito ya kunata.
Kidokezo:
- Tia hiliki na arki ikiwa tayari kumwagiwa juu ya kaimati, huku unavichanganya na huku shira ikipowa na kugeuka kuwa sukari kavu.
Shira ya Kaimati hizi iwe nzito ili unapochanganya na kaimati igeuke kuwa kama sukari ya visheti.
Angalizo usiache unga ukaumuka sana!Nlijaribu siku moja mmmh nikiweka kwenye mafuta zinasambaa zinakua kama chura
Haukuumuka kiivoAngalizo usiache unga ukaumuka sana!
Nlijaribu siku moja mmmh nikiweka kwenye mafuta zinasambaa zinakua kama chura
Ha ha ha nimecheka kwa kweliNlijaribu siku moja mmmh nikiweka kwenye mafuta zinasambaa zinakua kama chura
Acha tu ngemuwekea mtoto zile lazma angekimbia angejua waduduHa ha ha nimecheka kwa kweli
Hamn inategemea na jinsi ya uumuaji wako wa unga mm nikipika huwa hazin kabs hayo mafuta unayoyazungumziaTatizo LA kalmat zinanyonya mafuta
Unaumua dk ngapi?Hamn inategemea na jinsi ya uumuaji wako wa unga mm nikipika huwa hazin kabs hayo mafuta unayoyazungumzia