Jinsi tuzo ya CAF ya timu bora ya karne waliyopewa Al Ahly ilivyozua mgogoro mkubwa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,151
7,916
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa vigezo gani CAF waliitangaza Al Ahly kuwa ni timu bora ya karne ya 20? Wengi mnadhani ni kwa kubeba makombe mengi kuliko timu nyingine yoyote lakini siyo kweli.

Karne ya 20 iliisha 31/12/2000. Katika mafanikio ya Al Ahly hadi kufikia tarehe hiyo, katika mashindano yanayoandaliwa moja kwa moja na CAF Al Ahly walichukua makombe 6 na moja la mabara (Afro-Asia Cup).

Wakati huo huo, Zamalek hadi kufikia mwisho wa karne ya 20 ilikuwa imechukua makombe 7 ya CAF na mawili ya mabara (Afro-Asia Cup).

Kilichoipa tuzo hiyo Al Ahly ni system ya kuhesabu point iliyotumiwa na CAF ambayo iliyapa points tofauti makombe na hatua mbalimbali ambazo timu ilifikia, kama wanavyofanya sasa hivi kwenye ranking zao. Kutokana na kutokubaliana na hilo, ilifika wakati Zamalek nao wakajitangaza kuwa wao ndiyo Club Sahihi ya Karne. Huu ulikuwa ni mgogoro mkubwa uliodumu kwa miaka mingi.

Al Ahly toka karne hii ya 21 imeanza ndiyo wamekuwa hawana mpinzani linapokuja suala la makombe.

Hivi TFF wakisema watangaze Club Bora ya Tanzania kwa Karne ya 20 wakizingatia mafanikio katika ligi ya ndani pamoja na kwenye mashindano ya CECAFA na CAF, timu gani inastahili kutwaa tuzo hiyo?
 
Sasa usha sema TFF mashindano ya CECAFA na CAF yanaingiaaje?
 
Jibu hilo hapo

20240322_153710.jpg
 
Yanga bingwa mara 30
Yanga pekee ndiye mwenye mafanikio kimataifa ( fainali Confederation na medali)

Kwa hiyo jibu unalo
Hazijafika hizo bwashee. Halafu tunaongelea karne iliyopita ambapo ni Simba pekee Ilibeba medali ya CAF. Pia Simba ndiyo timu ukanda wa Africa Mashariki na Kati iliyochukua mara nyingi zaidi kombe la CECAFA.

Na tungesema tuangalie timu bora kwa miaka 20 iliyopita............au ngoja niache maana huko ndiyo kabisa kuna watu wameachwa mbaali sana maana makundi tu wamechungulia kwa mara ya kwanza mwaka huu.
 
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa vigezo gani CAF waliitangaza Al Ahly kuwa ni timu bora ya karne ya 20? Wengi mnadhani ni kwa kubeba makombe mengi kuliko timu nyingine yoyote lakini siyo kweli.

Karne ya 20 iliisha 31/12/2000. Katika mafanikio ya Al Ahly hadi kufikia tarehe hiyo, katika mashindano yanayoandaliwa moja kwa moja na CAF Al Ahly walichukua makombe 6 na moja la mabara (Afro-Asia Cup).

Wakati huo huo, Zamalek hadi kufikia mwisho wa karne ya 20 ilikuwa imechukua makombe 7 ya CAF na mawili ya mabara (Afro-Asia Cup).

Kilichoipa tuzo hiyo Al Ahly ni system ya kuhesabu point iliyotumiwa na CAF ambayo iliyapa points tofauti makombe na hatua mbalimbali ambazo timu ilifikia, kama wanavyofanya sasa hivi kwenye ranking zao. Kutokana na kutokubaliana na hilo, ilifika wakati Zamalek nao wakajitangaza kuwa wao ndiyo Club Sahihi ya Karne. Huu ulikuwa ni mgogoro mkubwa uliodumu kwa miaka mingi.

Hivi TFF wakisema watangaze Club Bora ya Tanzania kwa Karne ya 20 wakizingatia mafanikio katika ligi ya ndani pamoja na kwenye mashindano ya CECAFA na CAF, timu gani inastahili kutwaa tuzo hiyo?
Yanga,ofcourse
 
Kuna watu wakiona huu uzi wanatafuta pakujificha 😀😀😀 Timu ambayo hata ikiachiwa ishinde Ligi mara 5 mfululizo bado haiwezi kufikia rekodi ya mabingwa wa kihistoria 😀 achilia mbali medali za CAF
 
Kwa bongo huo mjadala hautokaa uishe, labda waipe timu tofauti na hizi mbili
Takwimu zipo ni TFF wanaogopa tu kuvitolea vitu ufafanuzi.

Nina wazo liwafikie wahusika, waanzishe tuzo ya "Timu ya Muongo (Team of the Decade). Waweke wazi mfumo wa point utakaotumika halafu kila baada ya miaka 10, timu moja yenye point nyingi ipewe tuzo. Mfumo ujumuishe bingwa wa ligi, FA (bingwa na mshindi wa pili), pamoja na CAFCL na CAFCC kuanzia robo fainali.

Tukutane June 2029 kwa kutangazwa mshindi wa kwanza wa 2019-2019.
 
TFF wana deal na mashindano ya ndani pekee
 
Al Ahly waliwahi shiriki kombe la CAF huku wakiwa nafasi ya tatu na wakabeba Kombe hao Al Ahly washawahi kuwa washindi wa pili kombe la Klabu Bingwa mabingwa wakiwa Wydady ila wao ndio walipata nafasi ya kushiriki Club Bingwa ya Dunia...
Hao Al Ahly ligi ya Misri wamecheza mechi chache kuliko Timu yeyote wakiwa na mechi 7 wakati Timu zingine zina mechi 15 na 16 swala la upangaji matokea kwa mfumo huu haukwepeki hawana Ligi bora kwa sasa ndio maana hata Timu yao ya Taifa ni ya kawaida sana...
 
Back
Top Bottom