Jimbo la Sitta

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
884
Yani, halmashauri ya wilaya ya Urambo ina madiwani hovyo kabisa, wamemnunulia Mkurugenzi wa halmashauri gari GX V8 wakati madawati, vitabu, maji katika mji wa Urambo hakuna. Inabidi katika katiba mpya angalau udiwani sifa iwe kuanzia kidato cha sita.
 

Attachments

  • Gari.-small.jpg
    Gari.-small.jpg
    20.7 KB · Views: 212
mwenye jimbo hana habari anahangaikia urais,sasa kama jimbo linamshinda ataweza nchi?
 
kazi ya kuwa na wanasiasa ndio hiyo
"wao wanachofikiria ni uchaguzi tu hakuna maendeleo wala mipango ya maendeleo"
waone jinsi ambavyo hawataki kukosolewa,kuambiwa ukweli wanapinga harakati
hawataki hata changamoto za wananchi wao
 
haah haha sio six peke yake mkuu halmashauri nyingi zimeyafanya hayo mf halmashauriya wilaya ya Kilolo mkoani iringa nayo ni madudu matupu.......... tatizo ni usimamizi mbovu wa halimashaurihizi na tatizo kubwazaidi ni BULGA waliyokula baadhi ya viongozi wetu (wa zamani wanjua bulga ni nini )
 
tatizo hatuna vipaumbele kwa hesabu la haraka haraka. mafuta ya vx kwa siku ni sawa na kununua madawati nane piga kwa mwaka.
 
Halafu madiwani walivyo bogazi wanajisifu eti Mkurugenzi ana gari zuri. 2015 wana Urambo piga chini magamba weka CDM tupu, hakuna ujinga huu halmashauri zinazoongozwa na CDM.
 
Yani, halmashauri ya wilaya ya Urambo ina madiwani hovyo kabisa, wamemnunulia Mkurugenzi wa halmashauri gari GX V8 wakati madawati, vitabu, maji katika mji wa Urambo hakuna. Inabidi katika katiba mpya angalau udiwani sifa iwe kuanzia kidato cha sita.

I believe Chadema hawana ujinga huo au kwenye majimbo au Halmashauri za Chadema kuna upuuzi wa VX ? Basi chagueni Chadema kwa wingi kuzuia ujinga huu
 
CAG apewe mandate ya kufukuza wafanyakazi wa serikali soon baada ya hati chafu..(No value for Money at all wen CCM re dizzy)
 
Taifa linaonekana watu wake wanaupeo kuliko viongozi waliowachagua,lazima mambo yaende hovyo mpaka watu wafanye kinyume chake.
 
Mbona unawashambulia madiwani pekee? Mbunge wao pia anawajibika kupata tuhuma hii kwani ni mjumbe katika vikao vyote vya Finance na Full Council sasa wakati wanajadili si alikuwepo mbona hakupinga? au kama hakuwepo alikuwa wapi? na taarifa hakuwa nayo? Lakini kinachoonekana hapa Mwenyekiti wa Halmashauri ndo anatakiwa kubeba lawama zote kwani Halmashauri nyingi wenyeviti ndo upendelea sana ununuzi wa magari ya kifahari kwa halmashauri kwani nao uyatumia wakati wa safari nyingi na hivyo kujisikia ufahari.
 
Six...................siku hizi magreth sitta simsikii kabisa hivi yuko kitengo gani vile
 
urambo ni sehemu kubwa.. kuna urambo mashariki [kwa sitta] na urambo kusini [ kwa kapuya].. sasa ukisema urambo kwa sitta unamaanisha nini..
 
Wizi ndani ya wizi. Hapa wa kulaumi si madiwani bali mfumo wa CCM wa Chukua Chako Mapema. Huu ni mchezo unaoanzia bungeni ambapo wabunge wanapewa mikopo ya kununulia migari mikubwa na aghali isiyofanana na wale wanaowawakilisha. Kinachofanyika Tanzania ni kujihudumia kwa kutumia raslimali za umma. Kila mtu ni kibaka kwa nafasi yake so to speak.
 
Mama cta anaandaliwa mazingira ya kuchukua jimbo la mme wake analotawala na jinsi walivyo wa2 wa urambo wanavyopenda wali wa kuku watampokea kwa mikono miwili na hii ndivyo itakavyokuwa ck ya kuja kutambulishwa wataandaliwa wali kuku halafu watatoa jimbo tena kwa miaka mitano kwani cta anawajua watu wake shida huwa wali kuku
 
Back
Top Bottom