Jimbo la Kiteto - Hafla ya Kusainiwa kwa Mikataba Ujenzi Barabara za Lami

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
JIMBO LA KITETO

TAARIFA KWA WANANCHI WA KITETO

HAFLA YA KUSAINIWA KWA MIKATABA UJENZI BARABARA ZA LAMI

Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto nachukua fursa kuwafahamisha kuwa KESHO tarehe 16. 6.2023 Wizara ya Ujenzi kupitia kwa Mhe. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Mbarawa tutashuhudia kusainiwa kwa mikataba ya Ujenzi wa Barabara zetu kwa kiwango cha Lami itakayofanyika Ukumbi wa JAKAYA Kikwete Mjini Dodoma

1. Barabara ya Kongwa - Kiteto - Simanjiro- Arusha KM 453

2. Barabara Handeni - Kibirashi- Kijungu - Kibaya - Njoro- Chemba - Singida KM 460

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa.

Ndugu wananchi wenzangu wa Kiteto tunayo kila sababu ya kutoa shukuran kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwaajili ya kutatua miradi ya Maendeleo. Tumwombe Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe Afya Njema na kumlinda vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika Kujenga Taifa Letu.

Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni. Ndugu wananchi wenzangu kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa unyenyekevu na uaminifu mkubwa.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara!

Mungu Ibariki Kiteto!
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Mhe. Edward Ole Lekaita Kisau (Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

Leo tarehe 15. 6. 2023
Kazi Iendelee

WhatsApp Image 2023-06-15 at 20.10.58.jpeg
 
Back
Top Bottom