Jimbo la Kiteto: Usajili wa Shule Mpya 12 za Msingi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

JIMBO LA KITETO: TAARIFA MAALUM KWA WANANCHI KUHUSU USAJILI WA SHULE MPYA- USAJILI WA SHULE MPYA 12 ZA MSINGI

Ndugu wananchi wenzangu mnatakumbuka kuwa kwa miaka miwili na nusu ya Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tulipokea pesa nyingi za miradi kwajili ya kuboresha Miundombinu na mazingira ya katika shule zetu. Aidha Jimbo letu la Kiteto tulipata madarasa mapya zaidi ya 57 kwaajili ya shule zetu zote Shikizi 18.

Ndugu wananchi wenzangu napenda kuchukua fursa kwa furaha kubwa kuwafahamisha kuwa shule zetu 10 Shikizi zimepata usajili leo na bado tunaendelea kuboresha Miundombinu katika shule zingine Shikizi zilizobaki kwaajili ya Usajili.

Shule zilizopata usajili ni kama ifuatavyo;

1. Shule Shikizi ya Ormemei Kata Njoro

2. Shule Shikizi ya Napilukunya Kata ya Partimbo

3. Shule Shikizi ya Olengashu Kata Partimbo

4. Shule Shikizi ya Ndepesi Kata ya Namelock

5. Shule Shikizi ya Mbarbali Kata ya Sunya

6. Shule Shikizi ya Emurtoto Kata ya Songambele

7. Shule Shikizi ya OLengare, Kata ya Sunya

8. Shule Shikizi ya Kinangali Kata ya Laiseri

9. Shule Shikizi ya Ngaikitala Kata ya Sunya

10. Shule Shikizi ya Lerug Kata Kijungu

11. Shule Mpya ya Azimio A Kata ya Matui

12. Shule Mpya Nguzosita Kata ya Dongo

Aidhaa pamoja na usajili huu bado tunaendelea kuboresha Vituo vya Shule Shikizi kwaajili ya Usajili ambazo ni (Esekii, Oltalet, Orpirikata, Neisuya, Misheni, Ngapapa, Kona na Dotii, na nyingine Orkiloriti na Chamalenge)

Nawaomba tuendelea kumwombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa moyo wa kuendelea kutufuta pesa kwaajili ya miradi ya kuboresha Miundombinu ya Shule zetu kwaajili ya Watoto wetu na kushughulia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa kwa ufanisi na kasi kubwa zaidi.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara !

Mungu Ibariki Kiteto !

Mungu Ibariki Tanzania !

Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge

Edward Ole Lekaita Kisau (Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

Leo tarehe 2. 11. 2023

Kazi Iendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.34.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.34.23.jpeg
    65 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.35.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.35.41.jpeg
    49.8 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.36.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.36.13.jpeg
    72.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.37.59.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.37.59.jpeg
    44.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.38.00.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.38.00.jpeg
    43.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.38.00(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.38.00(1).jpeg
    42.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.38.00(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.38.00(2).jpeg
    46.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.40.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.40.22.jpeg
    479.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.40.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-03 at 00.40.53.jpeg
    538.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom