Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Mkuu sina haja ya kuendelea na huu mjadala lakini jambo moja nataka kuliweka sawa kwamba Mandela, Sisulu, Mbeki na wenzao walifungwa kwa KUVUNJA SHERIA. Ndio maana nikasema kwa mujibu wa makaburu na sheria zao, Mandela na wenzake walifungwa kwa uhaini. Victorie Ingabire wa Rwanda anashitakiwa kwa uhani (kwa mujibu wa sheria) lakini ukiangalia kwa makini ni suala la kisiasa. Akifungwa atakuwa amehukumiwa kwa uhaini na wala si kwa kuanzisha chama cha siasa. Hayo tu.Uko sahihi......
Sidhani kama ni BUSARA kulinganisha kifungo cha mtu kama Nelson Mandela na BAN wanazopewa watu wanaoishiwa HOJA ndani ya JF na kutoa VIROJA na hatimaye kupigwa BAN kwa sababu ya matusi/lugha za kejeli kwa kuwaita wenzao 'Masaburi', 'Magamba',Magwanda','Unafikiri kwa kutumia Masaburi', Bi Kiroboto' N.k......Itakuwa ni dhihaka kwa wapigania Uhuru wa aina ya Mandela kufananishwa na wana JF wanapigwa BAN kwa kutukana na kuharibu mijadala/kuvunja sheria za JF ....
Nijuacho mimi BAN inatolewa kwa mtu anayevunja sheria za JF na si kwa kuonewa kama ilivyokuwa kwa akina Mandela na wenzake......
Itakuwa ni kichekesho kumpa Tuzo mtu ambaye kutwa anashinda JF kuharibu hoja/mijadala kwa matusi na lugha zisizo za kistarabu na baadae kupigwa BAN....
Tafakari........Chukua Hatua
Niseme tu kwamba kufungwa/ban inategemea unaingalia kwa macho gani. Mimi binafsi si muumini wa matusi na sipendi jukwaa hili liwe jukwaa la matusi. Kama kweli mtu alifungiwa kwa matusi ni halali laikini kama ni kwa tofauti tu ya maoni; hapana.