"JF M & F Politician Of The Year 2011" Competition

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Angalizo: Mods kwa hekima mnaombwa msiiamishe thread hii wala kuichanganya na nyingine yoyote.

Wanajamii; Wana JF

Mwaka 2010 tulifanya mchakato wa kumpata JF Man & Woman of The Year 2010. Shindano kama hili pia lilifanyika Mwaka 2009.

  • Washindi wa 2009 "JF SuperLady" au "Celebrity wa JF" alikuwa WoS (Woman of Substance)
  • Washindi wa 2010 "Regia Mtema" (RIP) - Kwa JF Woman of the Year 2010
  • na Nyani Ngabu kama "JF Man of The Year 2010"

Mchakato wote mpaka mshindi kupatikana unaweza kuupitia hapa:
https://www.jamiiforums.com/complaint...ar-2010-a.html

Mwaka huu tunataka kuuboresha mchakato huu na tunapenda kupitia mchakato huu kupata washiriki wengi na kuipa taswira JF kuwa kuna watu wanafakubalika katika hii online community.

Mwaka huu 2012 tunafanya mchakato wa kuwapata Washindi wa 2011 (lakini michango yao ya sasa inakubalika iingizwe 2011).Tulichelewa kufanya kwa sababu zilizo nje ya uwezo. Categories za Mwaka huu ni:

  • JF WOMAN OF THE YEAR 2011 na pia JF MAN OF THE YEAR 2011 (Overall).

  • Lakini Pia Tutaongeza Category ya: "JF QUEEN OF MMU" and "JF KING OF MMU" na Pia Category ya:

  • "JF MALE POLITICIAN OF THE YEAR 2011" na "JF FEMALE POLITICIAN OF THE YEAR 2011"

Mchakato wa kumpata "JF MALE & FEMALE POLITICIAN OF THE YEAR 2011" ndiyo unaanza sasa.Katika mchakato wa awali tutapendekeza majina mbalimbali katika category hii kulingana na unavyoona mhusika anakubalika na mwishoni tutachagua watatu kutoka katika kila category na kisha kuwapambanisha kupitia JF POLLS. Mwaka huu napendekeza tutoe zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Tutajulishana zawadi hizi tutakapoingia katika mchakato wa Kupiga kura.

Vigezo vifuatavyo vizingatiwe katika kutoa mapendekezo ya watakaoshindanishwa katika hizi KURA ZA MAONI:

1. Kama ni category ya WOMAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanamke na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike. Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - JEC (Superman) ya Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

2. Kama ni category ya MAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanaume na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike.

Katika 1 na 2: Uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya JF (JEC) wa Shindano hili utakuwa ni Final. wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post anazobandika. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF.

4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.

6. Kwa Wanaogombea Overall tittle, asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua mawili. Kwa wale wanaopendekezwa MMU basi akubalike katika jumuiya ya MMU

7. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".

8. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.

9. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.

10. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.

Sasa kila moja yuko huru kutoa mapendekezo yake ya nani wanastahili kuingia katika tatu bora katika kila category.

Angalizo: Washindi wa Miaka ya Nyuma ni Macelebrity tayari hivyo hawaruhusiwi kupendekezwa.

Nashauri kuwa mapendekezo ya majina yaambatane na maelezo mafupi.

Uwanja ni wenu. Karibuni sasa mto mapendekezo au NOMINATIONS.

Zingatia: ID za kuchakachua haziruhusiwi: i.e ID ambazo ni mpya kabisa na zimetengenezwa kwa ajili ya kupiga debe na kuongeza kura tu na ID zilizokuwa hazitumiki muda mrefu na sasa zimeibuka ghafla:

Unapofanya nomination yako andika kabisa, Unamnominate nani na kwa title gani:

Mfano: "Superman awe JF Male Politician of The Year 2011" NB: Pls msimchague Superman huu ni mfano tu.

Wasalaam
Superman-Logo.jpg

Signed & Sealed:

Superman

Mwenyekiti - Tume Ya Uchaguzi ya JF (JEC)

images
 
hahahaha, hata sijui niwataje kina nani. Mkuu, usihesabu hii kama pendekezo, I am just thinking... hivi Ritz yuko wapi?
 
Man - Nnauye Jr

Woman - Mary Chitanda

Nawasilisha
 
Safi sana Mhe. Mwenyekiti...

Hapa tuko pamoja sana mkuu.....

Pia ni vema anayependekezwa awe hajawahi kulambwa BAN....

NB.....Usitusahau na wanamichezo na Burudani pia......Tunategemea JEC mtaliangalia hili pia

Mkuu, naendelea kujitahidi sana. Ila ndo niko hoiii. Kazi zote zimesimama . . . lol
 
Safi sana Mhe. Mwenyekiti...

Hapa tuko pamoja sana mkuu.....

Pia ni vema anayependekezwa awe hajawahi kulambwa BAN....

NB.....Usitusahau na wanamichezo na Burudani pia......Tunategemea JEC mtaliangalia hili pia
Hicho kigezo cha BAN kigumu sana!
Wanasiasa wengi waliofanikiwa wamepitia mikiki mikiki mingi, vifungo vikiwa mojawapo! Huku inabidi hicho kigezo cha BAN kiondolewe!
 
iko kigezo cha ban naona kakitoa baada ya kumweka FF kule kwenye JF woman of the year..
 
Safi sana Mhe. Mwenyekiti...

Hapa tuko pamoja sana mkuu.....

Pia ni vema anayependekezwa awe hajawahi kulambwa BAN....

NB.....Usitusahau na wanamichezo na Burudani pia......Tunategemea JEC mtaliangalia hili pia

Mkuu Bala,
Nakuunga mkono katika kuzingatia nidhamu za nominees, kama mtu amekula ban katika mwaka unaotafutiwa mshindi asiruhusiwe kushindanishwa.
Ban yake iwe inamdisqualify moja kwa moja!
 
Hicho kigezo cha BAN kigumu sana!
Wanasiasa wengi waliofanikiwa wamepitia mikiki mikiki mingi, vifungo vikiwa mojawapo! Huku inabidi hicho kigezo cha BAN kiondolewe!
Mkuu Rejao nimeifurahia hoja yako. Nadhani mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ataiangalia vizuri hasa kwa category ya wanasiasa. Mandela anaheshimika dunia nzima lakini pia ndiye mfungwa wa kisiasa alitumia muda mrefu gerezani. Makaburu walikuwa wakisema ni mhaini tu na si mfungwa wa kisiasa.
 
Mkuu Bala,
Nakuunga mkono katika kuzingatia nidhamu za nominees, kama mtu amekula ban katika mwaka unaotafutiwa mshindi asiruhusiwe kushindanishwa.
Ban yake iwe inamdisqualify moja kwa moja!
Mkuu angalia Rejao anachokisema hapa. Hakina mantiki kweli?

Hicho kigezo cha BAN kigumu sana!
Wanasiasa wengi waliofanikiwa wamepitia mikiki mikiki mingi, vifungo vikiwa mojawapo! Huku inabidi hicho kigezo cha BAN kiondolewe!
 
Hicho kigezo cha BAN kigumu sana!
Wanasiasa wengi waliofanikiwa wamepitia mikiki mikiki mingi, vifungo vikiwa mojawapo! Huku inabidi hicho kigezo cha BAN kiondolewe!

Ni kweli wanasiasa wengi waliofanikiwa wamepitia mikikimikiki mingi pamoja na vifungo kwa kutetea haki za watu wao.
Hawa wanasiasa wa hapa JF wanaokula ban ni kwa sababu ya kutojiheshimu, kushindwa kujenga hoja na kuishia kuvurumisha matusi!
Kwahiyo utaona kwamba kazi bila nidhamu ni vurugu, inabidi ban kiwe kigezo muhimu ili wajirekebishe kuanzia mwaka huu na kuendelea.
 
Mkuu Rejao nimeifurahia hoja yako. Nadhani mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ataiangalia vizuri hasa kwa category ya wanasiasa. Mandela anaheshimika dunia nzima lakini pia ndiye mfungwa wa kisiasa alitumia muda mrefu gerezani. Makaburu walikuwa wakisema ni mhaini tu na si mfungwa wa kisiasa.
Tupo pamoja Kimbunga,
But naona Mwita Maranya anashupalia sana hili suala la ban.
 
Hicho kigezo cha BAN kigumu sana!
Wanasiasa wengi waliofanikiwa wamepitia mikiki mikiki mingi, vifungo vikiwa mojawapo! Huku inabidi hicho kigezo cha BAN kiondolewe!
Uko sahihi......

Sidhani kama ni BUSARA kulinganisha kifungo cha mtu kama Nelson Mandela na BAN wanazopewa watu wanaoishiwa HOJA ndani ya JF na kutoa VIROJA na hatimaye kupigwa BAN kwa sababu ya matusi/lugha za kejeli kwa kuwaita wenzao 'Masaburi', 'Magamba',Magwanda','Unafikiri kwa kutumia Masaburi', Bi Kiroboto' N.k......Itakuwa ni dhihaka kwa wapigania Uhuru wa aina ya Mandela kufananishwa na wana JF wanapigwa BAN kwa kutukana na kuharibu mijadala/kuvunja sheria za JF ....

Nijuacho mimi BAN inatolewa kwa mtu anayevunja sheria za JF na si kwa kuonewa kama ilivyokuwa kwa akina Mandela na wenzake......

Itakuwa ni kichekesho kumpa Tuzo mtu ambaye kutwa anashinda JF kuharibu hoja/mijadala kwa matusi na lugha zisizo za kistarabu na baadae kupigwa BAN....

Tafakari........Chukua Hatua
 
Mkuu Rejao nimeifurahia hoja yako. Nadhani mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ataiangalia vizuri hasa kwa category ya wanasiasa. Mandela anaheshimika dunia nzima lakini pia ndiye mfungwa wa kisiasa alitumia muda mrefu gerezani. Makaburu walikuwa wakisema ni mhaini tu na si mfungwa wa kisiasa.

Kimbunga,
Majibu niliyompa rejeo ndio hoja yangu. Kwa msisitizo ni kwamba Mandera hakuwa mzushi wala muongo, alikuwa anawaambia ukweli watu wake-weusi lakini pia alikuwa anawapasha ukweli makaburu. Sasa makaburu kwa kuhofia kupoteza madaraka yao ya kuiongoza nchi ilibidi wamfunge.
Tofauti na Mandera wanasiasa wengi wanaokula ban hapa jf ni kwa sababu za kutukana, uongo, uzushi na mambo mengine ya kitoto.
Tukiruhusu wapate tuzo basi tutakuwa tunawapongeza kwa ''kazi nzuri'' ya kulidhalilisha jukwaa la siasa hapa JF!
 
Uko sahihi......

Sidhani kama ni BUSARA kulinganisha kifungo cha mtu kama Nelson Mandela na BAN wanazopewa watu wanaoishiwa HOJA ndani ya JF sababu ya matusi/lugha za kejeli kwa kuwaita wenzao 'Masaburi', 'Magamba',Magwanda','Unafikiri kwa kutumia Masaburi', Bi Kiroboto' N.k......Itakuwa ni dhihaka kwa wapigania Uhuru wa aina ya Mandela....

Nijuacho mimi BAN inatolewa kwa mtu anayevunja sheria za JF na si kwa kuonewa kama ilivyokuwa kwa akina Mandela na wenzake......

Itakuwa ni kichekesho kumpa Tuzo mtu ambaye kutwa anashinda JF kuharibu hoja/mijadala kwa matusi na lugha zisizo za kistarabu na baadae kupigwa BAN....

Tafakari........Chukua Hatua
Nafikiri siyo wote wanaopewa ban ni kwa sababu ya kutumia lugha chafu. Wengine wanapewa ban simply kwa sababu ya misimamo yao. Kuna ban nyingi sana hapa JF ambazo hazina kichwa wala miguu. unakuta mtu anapewa ban simply kwa sababu msimamo wake au sababu amesema maovu ya kiongozi flani anayelindwa na MODs wa hapa!!

Kuharibu mijadala ni moja ya sifa ya mwanasiasa mzuri. Inabidi mwanasiasa ujue mbinu mbali mbali za kuwasahaulisha watu mambo flani especially kama yana madhara kwenye uongozi wako.
 
Tupo pamoja Kimbunga,
But naona Mwita Maranya anashupalia sana hili suala la ban.

Lazima nilishupalie kwakuwa naona bila kufanya hivyo hii tuzo itakosa maana kwa kuruhusu waporomosha matusi, wazushi na wapika majungu nao kujiita wanasiasa!

Mkuu Bala nimekusoma tuko pamoja, naona watu wanataka kumtumia vibaya mzee Madiba kuficha madhaifu yao.
 
Nafikiri siyo wote wanaopewa ban ni kwa sababu ya kutumia lugha chafu. Wengine wanapewa ban simply kwa sababu ya misimamo yao. Kuna ban nyingi sana hapa JF ambazo hazina kichwa wala miguu. unakuta mtu anapewa ban simply kwa sababu msimamo wake au sababu amesema maovu ya kiongozi flani anayelindwa na MODs wa hapa!!

Kuharibu mijadala ni moja ya sifa ya mwanasiasa mzuri. Inabidi mwanasiasa ujue mbinu mbali mbali za kuwasahaulisha watu mambo flani especially kama yana madhara kwenye uongozi wako.
I see!!!..............
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom