Mc Tilly,mali za mdogo wangu hazinihusu labda niambiwe na muhusika vinginevyo!Fahamu pia kumsomesha ndugu,mtu yoyote ni haki yake ya msingi siwezi kuhusisha kumsomesha mtu na mali alizopata huo ni ujinga!
jamani!nisichoelewa hapa ni kuwa,ni kwanini iwe sio heshima mwanamke kuolewa na wakakaa nyumba ileile?tofauti ni nini?aibu ni ipi?plz help me to understand this!sijajua hapa inakua nini ni nini!nielewesheni hapa!
Mi nikiRIP afu mke wangu alete njemba lilale kitandani mwangu..... wallah nawaibukia toka kaburini.
1.Mi nikiRIP.... Mke wangu atarithi kuwa kiongozi wa kusimamia mali zangu endapo tu hataolewa tena.
2.Akiolewa na aende zake kwa amani, atakuwa na gawio la mali zangu ambazo sasa zitasimamiwa na ndugu zangu.
Ila MALI ZOTE hizo ni MALI halali ya wanangu bila kujali 1 na 2 hapo juu. Watoto wakishakuwa wakubwa wataamua namna ya kumshirikisha mama yao.
Mkimwona Bibi mumwambie nimesema hivyo eti. Na ole wake akiuke.
Eiyer!wewe ni wa tofauti sana na binadamu wengine kama hujijui juwa hilo!ndio maana unapata shida kuelewa shida ipo wapi!kwa wengi tuliobaki hatuwezi vumilia kuona mali za ndugu yetu zinahamia kwa mtu mwingine!tatizo ni mali tu!ndio maana babu asprin kakuambia "atafufuka" endapo mkewe ataponda mali zake na jamaa mwingine!kama vipi aache mali!so tatizo lipo hapo!i hope umeanza kuelewa!
habari za heshima sijui nini sijui weka pembeni, cha kuzingatia hapa ni sheria inasemaje kwa mujibu wa dini/mila yake mkuu! Atakachomilikishwa kisheria atakuwa huru kukitumia apendavyo hata kama itakuwa nyumba au kinginecho.
Sikumbuki hasa kilichotufikisha kwenye mjadala wa kujadili kuhusu mwanandoa mmoja kufariki,lakini ambacho nakijua ni kuwa kuna mgogoro mkubwa kwenye tulichokua tunakijadili.Mjadala wenyewe ni kuwa,je mume anapofariki na kuacha watoto na mjane,mali alizoacha nani anatakiwa kuzisimamia?Pia kama mjane atakuwa anahitaji kuliwazwa je akipata mtu ahame nyumbani na akakae sehemu tofauti au palepale?Vijana wote isipokuwa mimi tu walidai kuwa,mali anatakiwa asimamie ndugu wa mume na kama atahitaji mume ahame pale nyumbani,walizungumza mengi na kudai mali ni za mume na mke haruhusiwi kuzisimamia!!Nilishangaa sana!MSIMAMO WANGU ulikuwa hivi;mke ana haki sawa na mume kwenye suala la kutolea maamuzi,mume ni kiongozi mkuu,maadam hayupo mke ndie mwenye last say!Ni aibu kubwa mwanaume mzima kwenda kuleta usumbufu kwenye mali za mwanaume mwingine,atafute zake!Pia mke anaweza kutumia mali atakavyo bila kuulizwa na YOYOTE,hata akitaka kuolewa hatakiwi kuulizwa chohote ni sawa na mume angeoa na kuishi pale na mke mpya!!Je nyie wana JF mwasemaje?