JF Ladies and Gents,niko sawa au?

Mc Tilly,mali za mdogo wangu hazinihusu labda niambiwe na muhusika vinginevyo!Fahamu pia kumsomesha ndugu,mtu yoyote ni haki yake ya msingi siwezi kuhusisha kumsomesha mtu na mali alizopata huo ni ujinga!

Eiyer!wewe ni wa tofauti sana na binadamu wengine kama hujijui juwa hilo!ndio maana unapata shida kuelewa shida ipo wapi!kwa wengi tuliobaki hatuwezi vumilia kuona mali za ndugu yetu zinahamia kwa mtu mwingine!tatizo ni mali tu!ndio maana babu asprin kakuambia "atafufuka" endapo mkewe ataponda mali zake na jamaa mwingine!kama vipi aache mali!so tatizo lipo hapo!i hope umeanza kuelewa!
 
nikiendelea kujaribu kukuelewesha,nitoe mfano,kijana tu maskini wa kibongo apate zali amuoe Paris Hilton,mara kijana akafa,ndugu zake kijana watakuwa na nguvu ya kudai mahotel ya Hilton ni yao?Paris akijiachia na mwanaume mwingine roho itawauma?!tafakari uone na ujue kiini ni mali,hasa ikizingatiwa imepatikanaje!
 
au mfano mdada leo akaolewe na Yusuf Manji,ghafla Manji kafa,halafu huyo mdada ahodhi mali zote,na mara apate jamaa lingine halafu jamaa ghafla moja lina sauti ktk mali za manji,kina manji watamuangalia tu?tafakari mwenyewe kisha uone ukweli mwenyewe
 
kwahiyo ukiangalia mivutano yote iliyopo hapo ni mambo ya mali!watu wakiamini mali imetengenezwa na fulani zaidi hawako tayari kuona mali hiyo inahama toka ukoo huu kwenda mwingine!zamani tulizoea sana kesi za mwanamke kubanwa kwa vile mali nyingi zilizalishwa zaidi na wanaume,leo hii wanawake wana-make kwa kwenda mbele utaona kubanwa huku kunahamia hadi kwa wanaume!mfano bob brown kabaniwa sana mazishi ya whitney,ndugu wanahofu kupitia mtoto bobby christina,bobby brown atazi-cross border mali za whitney kwenda kwake na anaweza kutumbua na mwanamke mwingine vilevile!
 
jamani!nisichoelewa hapa ni kuwa,ni kwanini iwe sio heshima mwanamke kuolewa na wakakaa nyumba ileile?tofauti ni nini?aibu ni ipi?plz help me to understand this!sijajua hapa inakua nini ni nini!nielewesheni hapa!

habari za heshima sijui nini sijui weka pembeni, cha kuzingatia hapa ni sheria inasemaje kwa mujibu wa dini/mila yake mkuu! Atakachomilikishwa kisheria atakuwa huru kukitumia apendavyo hata kama itakuwa nyumba au kinginecho.
 
Mi nikiRIP afu mke wangu alete njemba lilale kitandani mwangu..... wallah nawaibukia toka kaburini.

1.Mi nikiRIP.... Mke wangu atarithi kuwa kiongozi wa kusimamia mali zangu endapo tu hataolewa tena.
2.Akiolewa na aende zake kwa amani, atakuwa na gawio la mali zangu ambazo sasa zitasimamiwa na ndugu zangu.

Ila MALI ZOTE hizo ni MALI halali ya wanangu bila kujali 1 na 2 hapo juu. Watoto wakishakuwa wakubwa wataamua namna ya kumshirikisha mama yao.

Mkimwona Bibi mumwambie nimesema hivyo eti. Na ole wake akiuke.

Yaani wewe ndo kama unamuongelea mdingi wake na kipipi!!!
 
Eiyer!wewe ni wa tofauti sana na binadamu wengine kama hujijui juwa hilo!ndio maana unapata shida kuelewa shida ipo wapi!kwa wengi tuliobaki hatuwezi vumilia kuona mali za ndugu yetu zinahamia kwa mtu mwingine!tatizo ni mali tu!ndio maana babu asprin kakuambia "atafufuka" endapo mkewe ataponda mali zake na jamaa mwingine!kama vipi aache mali!so tatizo lipo hapo!i hope umeanza kuelewa!

True kabisa.
 
habari za heshima sijui nini sijui weka pembeni, cha kuzingatia hapa ni sheria inasemaje kwa mujibu wa dini/mila yake mkuu! Atakachomilikishwa kisheria atakuwa huru kukitumia apendavyo hata kama itakuwa nyumba au kinginecho.

Eti mwanaume mwenzio anakuja kustarehe kwenye jasho lako huku wazazi na wadogo zako wanaishi kwenye mjengo wa maana! hii haikubaliki.
 
Daaah AshaDii ivi mfumo dume mpaka lini jamani so mke akifarii alafu mali ziwe na yeye alichuma mume anaruhusiwa kuoa mke mwingine na kuishi nae pale ndani sio mh????? nadhani kwa mtazamo wangu mdogo tubadilike jamani aibu na fedhea wote tunapata sio mwanamke wa mwanamke. ifikie kipindi mwanamke sio kujifanya unamsimo kwa mwanaume wakati huo huo unaweza kwenda kukaa kwenye nyumba ya mwanamke mwenzio ata hilo unalo leza kwamba mwanamke atakiwi kuishi na mwanume humo ndani ni wachache wanye msimamo huo wengi wetu utamkaribisha huyo mwanaume uje kuishi nae hapo kwa mumewe. ila kwa mtu mwenye akili kwa nini kama wewe mwanaume na wewe mwanamke mwenzio kaondoka au kafariki basi kajenge nyumba nyingine au kapange kwingine muanze maisha huku ile nyumba sio mali yenu ni kwaajili ya watoto wenu. na kama wewe ni msimamizi nzuri mwambie huyo jamaa yao tukaanze maisha sehemu nyingine hapa sio kwetu ivyo ivyo kwa mwanaume alafu hapo ndio utakapo jua maharage muda mwingine ni kiungo cha makande. ila mume anapofariki msimamizi mkuu ni mke na watoto
 
Sikumbuki hasa kilichotufikisha kwenye mjadala wa kujadili kuhusu mwanandoa mmoja kufariki,lakini ambacho nakijua ni kuwa kuna mgogoro mkubwa kwenye tulichokua tunakijadili.Mjadala wenyewe ni kuwa,je mume anapofariki na kuacha watoto na mjane,mali alizoacha nani anatakiwa kuzisimamia?Pia kama mjane atakuwa anahitaji kuliwazwa je akipata mtu ahame nyumbani na akakae sehemu tofauti au palepale?Vijana wote isipokuwa mimi tu walidai kuwa,mali anatakiwa asimamie ndugu wa mume na kama atahitaji mume ahame pale nyumbani,walizungumza mengi na kudai mali ni za mume na mke haruhusiwi kuzisimamia!!Nilishangaa sana!MSIMAMO WANGU ulikuwa hivi;mke ana haki sawa na mume kwenye suala la kutolea maamuzi,mume ni kiongozi mkuu,maadam hayupo mke ndie mwenye last say!Ni aibu kubwa mwanaume mzima kwenda kuleta usumbufu kwenye mali za mwanaume mwingine,atafute zake!Pia mke anaweza kutumia mali atakavyo bila kuulizwa na YOYOTE,hata akitaka kuolewa hatakiwi kuulizwa chohote ni sawa na mume angeoa na kuishi pale na mke mpya!!Je nyie wana JF mwasemaje?

Mkuu, hayo mambo mwisho wa siku ni umaskini tu unasumbua watu. Kama ndugu wa mume aliyefariki, yaani wazazi wake au wadogo zake wangekuwa wanajiweza kiuchumi wasingesumbuka na mali za marehemu. Huo ndiyo ukweli. Lakini utakuta sehemu zote wako hoi - upande wa mwanamke na mwanaume. Akifa mwanaume, ndugu zake wanaona mali za ndugu yao zinaenda kunafaisha ukoo wa mwanamke na wao wanabaki patupu. Nimeona familia ambazo mwanaume amefariki lakini mjane akawa na busara ya kusaidia pande zote mbili na amani inakuwepo. Lakini akili hiyo haiji ghafla, dalili huwa zipo toka mwanzao wote wakiwa hai. Familia za wanaojiweza hawafuatilii mali za marehemu, wanamwachia mke wake ana watoto wake.
 
Back
Top Bottom