Jeshi la polisi linamtafuta kamanda godbless lema na makamanda wengine..

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Jeshi la polisi mkoani Arusha linamsaka aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tuhuma za kushambulia mwili pamoja na upotevu wa simu pamoja na fedha.

Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa kamanda polisi Lebaratus Sabas alisema kuwa jeshi la polisi linamsaka lema na wenzake ambao idadi yake hawajatajwa kwa tuhuma za kushambulia mwili wa watu wawili tukio lililofanyika october 28 mwaka huu katika kata ya daraja mbili.

Alisema kuwa jeshi la polisi lilipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa watu wawili waliojulikana kwa jina la Ibrahimu Juma pamoja na Maritin Daniel wote wakazi wa daraja mbili kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la arusha mjini Godbless Lema akiwa na wanzake walimvamia na kuwashambulia kwa ngumi pamoja na kuwanyanganya simu aina ya samsang yenye samani ya shilingi laki tatu pamoja na fedha taslim kiasi cha shilingi laki mbili kisha kuondoka na kuwaacha.

Alisema kuwa watu hao waliamua kutoa taarifa polisi na jeshi la polisi linamsaka lema kwa ajili ya kujibu tuhuma hizi .Lkibeneke la kaskazini lilimsaka lema kujibu tuhuma hizi akupatikana kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa imezimwa.
 
Kawaambie hao mbweha nguvu ya umma haitakufa milele hata wakitunyanyasa na kututakisha tamaa!
Kilio ha wananchi ndicho kinawamaliza viongozki.
 
Hawa polisi nao watumie akili sasa! Sio kila upuuzi basi wanafungua mashtaka kisa tu ni cdm. Polisi walikuwepo eneo la tukio na waliona yaliyotokea, iweje wafungue mashtaka wakati waliona waliopigana na waliofanya fujo! Waliona Lema aliwapembeni wakati hao jamaa wakisukumana na mmoja akafyatua risasi. Wanawafahamu na wanajua sababu ni wanandugu hao waliotaka kupigana. Sasa Lema anashtakiwa kwa lipi! Huu ni upuuzi kabisa. Au wanafikiri ni sifa kutangaza kumsaka Lema wakati watu walikuwepo na waliona yaliyotokea.
Lazima polisi wafanye kazi yao kwa weledi na uadilifu sio kisiasa!
 
Mbona kamanda lema yupo mjini..huyu Rpc anatafuta media coverage.Hata ivyo kukamatwa kwetu wapambanaji ni kawaida.
 
Leo siku nzima tulikuwa na Lema tumeandamana kata nzima ya Daraja mbili kushangilia ushindi,na tumefanya mkutano wa hadhara,Lema alikuwepo,polisi walikuwepo,
Hii habari nina mashaka nayo
 
Hii no moja kati ya ile mikakati ya project ya hao polisi wanayolazimishwa kufanya kwa niaba ya magamba. Hiyo kutangaza tu kwamba hao wanatafutwa eti kwa kushambulia ni mbinu ya hiyo project ili kuueleza umma wote wa Tanzania wasikie kwamba viongozi wa CDM ni vurugu tupu.

Hao policcm wangeweza kuwatafuta hao watu kimya kimya kama vile wanavyofanya kwa maelfu ya wahalifu wanaowatafuta, tena wengine kwa makosa more serious kuliko hayo ya kushambulia.

Policcm sasa wanajidhalilisha kweli kweli kutumika kwa namna hii.

Inanikumbusha miezi kadha iliyopita Dr Slaa alipokamatwa pale Unga Limited Arusha na alipopekuliwa akakutwa na bastola,ambayo anamiliki kihalali. Tukio hilo polisi walilitangaza sana kwa umma umma. Compare kabla ya hapo pale AlShaba Rage kule Igunga alipopanda jukwaani huku na bastola ikininginia kiunoni na kila mtu kuiona Polisi waliokuwapo walijifanya vipofu hadi gazeti la Mwananchi lilipotoa picha yake!

policcm ni watumwa wa CCM!
 
Kwani lema anawaogopa hata ajifiche? Polisi waache tabia hizi za kujikomba kwa CCM ili waonekane wapo kazini!!!
 
Lema yupo mtaani just at Large!
Huyo Rpc anamtafutia wapi?
Lema hajawahi kuwaogopa polisi na hatafanyj hivyo.

Hawa ccm wanachofanya ni uwoga kwa kujua kuwa DHAIFU atafika Arusha tarehe 1.11.2012 kuzindua jiji , hivyo wanaota ndoto kwamba huenda Lema akaongea lolote au kuhamasisha wana A-Town siku hiyo ili wafanye jambo lolote.

Walichoona cha maana kwa upeo wa akili zao ni kwamba ashikwe na kupewa jamba jamba ya kipolisi ili afyate mkia, na pia ndiyo moja ya michapo watakayokuwa wanamsimulia DHaifu wakati wanapata Lunch inayotokana na kodi zetu.

Wasihangaike kutangaza kuwa wanamtafuta, maana hata leo alikuwa polisi akiwawekea dhamana watu walioshikwa jana eti walileta fujo kwenye uchaguzi wa diwani.

Kwanini wasingemshika palepale polisi au kwenye mkutano uliohutubiwa na Diwani mpya wa kata ya DarajaII?

Propaganda za kipumbafu hizi.
Senzi sana!
 
Leo siku nzima tumezunguka arusha nzima kwa maandamo ya amani ya kupongezana kwa ushindi wa daraja mbili na askari walikuwepo lakini hawakumshika lema.
Maji taka hizi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Jeshi la polisi mkoani Arusha linamsaka aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tuhuma za kushambulia mwili pamoja na upotevu wa simu pamoja na fedha.

Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa kamanda polisi Lebaratus Sabas alisema kuwa jeshi la polisi linamsaka lema na wenzake ambao idadi yake hawajatajwa kwa tuhuma za kushambulia mwili wa watu wawili tukio lililofanyika october 28 mwaka huu katika kata ya daraja mbili.

Alisema kuwa jeshi la polisi lilipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa watu wawili waliojulikana kwa jina la Ibrahimu Juma pamoja na Maritin Daniel wote wakazi wa daraja mbili kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la arusha mjini Godbless Lema akiwa na wanzake walimvamia na kuwashambulia kwa ngumi pamoja na kuwanyanganya simu aina ya samsang yenye samani ya shilingi laki tatu pamoja na fedha taslim kiasi cha shilingi laki mbili kisha kuondoka na kuwaacha.

Alisema kuwa watu hao waliamua kutoa taarifa polisi na jeshi la polisi linamsaka lema kwa ajili ya kujibu tuhuma hizi .Lkibeneke la kaskazini lilimsaka lema kujibu tuhuma hizi akupatikana kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa imezimwa.

Tanzania bwana anasakwaje? mi nikitoka nje hapa kwangu naiona nyumba ya LEMA na alikuwepo! siwamfuate!
 
Kama siasa za maji taka na uhuni wa CCM, kama Lema katenda kosa ni haki yao kumkamata na kumfikisha mahakamani ili haki itendeke. Ila kama wanampakazia, wanalitafuta la kulitafuta. Hivyo hatuwezi kutoa hitimisho hadi tujue ukweli ni upi hapa.
 
Hawa polisi nao watumie akili sasa! Sio kila upuuzi basi wanafungua mashtaka kisa tu ni cdm. Polisi walikuwepo eneo la tukio na waliona yaliyotokea, iweje wafungue mashtaka wakati waliona waliopigana na waliofanya fujo! Waliona Lema aliwapembeni wakati hao jamaa wakisukumana na mmoja akafyatua risasi. Wanawafahamu na wanajua sababu ni wanandugu hao waliotaka kupigana. Sasa Lema anashtakiwa kwa lipi! Huu ni upuuzi kabisa. Au wanafikiri ni sifa kutangaza kumsaka Lema wakati watu walikuwepo na waliona yaliyotokea.
Lazima polisi wafanye kazi yao kwa weledi na uadilifu sio kisiasa!

kisiasa gani jamani,na wakati kapora huo si ujambazi huo!!!!
 
Back
Top Bottom