Zaidi ya Bilioni 1.4 yajenga Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Sagini atoa neno

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mb), Jumanne Sagini amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4.

Akizungumza baada ya kukagua wa Mradi huo, Sagini amesema kuwa, kukamilika kwa Mradi huo utaipa heshima na hadhi Ofisi ya Kamanda wa Polisi kwani kila Kitengo kitakuwa na Ofisi yake tofauti na ilivyo kuwa sasa.
Ofisi.JPG

Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma lenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4 Novemba 17, 2023.

Ofisi 2.JPG
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) (Wa pili kushoto), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salim Morcase (Wa pili kulia), pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi hilo kwenye picha ya Pamoja baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4, leo Novemba 17, 2023.

"Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na nimearifiwa kuwa, fedha za awamu ya pili na tatu tayari zimetoka hivyo basi nimuombe mkandarasi kukamilisha ujenzi kama inavyoelekeza ili ofisi ianze kutumika." Alisema

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Salim Morcase, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ufuatiliaji wa karibu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara.

“Sisi kama Jeshi la Polisi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchi tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kwako kwa ufuatiliaji wa karibu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo letu,” alisema ACP Morcase.
Ofisi 3.JPG

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) (Kushoto), akikagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4, leo Novemba 17, 2023.
Aidha, amebainisha kuwa, Mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 92 na ulianza kutekelezwa Novemba 18, 2021 na unakadiriwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2023.
 
View attachment 2816287
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma lenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4 Novemba 17, 2023.

View attachment 2816288
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) (Wa pili kushoto), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salim Morcase (Wa pili kulia), pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi hilo kwenye picha ya Pamoja baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4, leo Novemba 17, 2023.

"Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na nimearifiwa kuwa, fedha za awamu ya pili na tatu tayari zimetoka hivyo basi nimuombe mkandarasi kukamilisha ujenzi kama inavyoelekeza ili ofisi ianze kutumika." Alisema

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Salim Morcase, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ufuatiliaji wa karibu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara.

“Sisi kama Jeshi la Polisi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchi tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kwako kwa ufuatiliaji wa karibu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo letu,” alisema ACP Morcase.
View attachment 2816289
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) (Kushoto), akikagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4, leo Novemba 17, 2023.
Aidha, amebainisha kuwa, Mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 92 na ulianza kutekelezwa Novemba 18, 2021 na unakadiriwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2023.
Hili jengo kwa hiyo 1.4B linaleta mantiki, ila kile kituo cha polisi butiama kwa 800M linaleta mashaka
 
Back
Top Bottom