Jeshi la polisi likifanya vyema, lipongezwe, hongera FFU kusambaratisha maandamano bila virungu, mabomu ya machozi, risasi za moto, bila maafa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,617
Wanabodi,
Hili ni bandiko la pongezi kwa jeshi letu la polisi. Wewe kama ni mmoja wa wale wenye allergy na pongezi zozote kwa awamu hii ya tano, naomba nikushauri, uishie hapa ili tusiharibiane siku.

Nasisitiza, jeshi letu la polisi likifanya vyema, lipongezwe!, hongera FFU kusambaratisha maandamano ya jana pale ubalozi wa Afrika Kusini bila virungu, bila mabomu ya machozi, bila maji ya washa washa, na bila risasi za moto, hivyo maandamano hayo kusambaratishwa bila kutokea kwa maafa yoyote!.

Niliwahi kuzungumzia humu kuwa taasisi yeyote ikifanya jambo zuri la kustahili pongezi, ipongezwe as encouragement izidi kutenda mazuri hayo!.

Kufuatia kusambaratishwa huko kwa yale maandamano ya jana, jeshi letu la polisi, limeonyesha uwezo, linastahili pongezi.

Pongezi hizi ni kufuatia a simple comparative analysis ya kusambaratishwa maandamano haya ambapo mimi niliuliza swali hili humu jf, Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Kuhusiana na polisi wetu na maandamano yasiyo na vibali, wakati wapinzani walipounda UKUTA na kupanga kuandamana, niliwahi kutoa ombi hili kwa jeshi letu la polisi Ombi Muhimu Kwa Jeshi Letu La Polisi."Nyinyi ni Wenzetu, September Mosi, Please Msigeuke Makaburu!".

Hivyo kama kumetokea maandamano ya amani yasiyo na kibali, yamesambaratishwa kwa amani, bila kuleta maafa yoyote, hili ni jambo jema kwa jeshi letu la polisi kustahili pongezi, ili hii sasa ndio iwe standard format ya usambaratishaji wa maandano yasiyo na vibali.

Kumbe polisi wetu wanaweza kusambaratisha maandamano bila kuleta maafa, na utaratibu huu ungeanza tangu zamani, ungekuta saa hizi Daudi Mwagosi yupo akiendelea na kazi na kuihudumia familia yake, ambayo hata sijui saa hizi inahudumiwa na nani na ina hali gani!. Ungekuta saa hizi Aquiline Akwilin, angekuwa anamaliza kozi yake na kugraduate, aje apate kazi nzuri, apate mchumba, aolewe ajenge familia yake na kujenga taifa la Tanzania.
RIP Daudi Mwangosi, RIP Aquiline Akwilin, Hongera Jeshi letu la Polisi, Hongera FFU wetu, kumbe mkiaamua kwa dhati kulinda amani na kulinda raia na mali zao, mnaweza.

Hongera sana IGP Sirro na vijana wako,
bila kusahau kutoa hongera kwa CinC maana...

Paskali.
Rejea zangu kwa Jeshi la Polisi na Maandamano
Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random ...
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? - JamiiForums
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
 
Napongeza kamanda wa kikosi tu, yaani OCD na si mtu mwengine, unaposema polisi unajumuisha walio-muua Akwilina pale kinondoni, hebu tumpongeze OCD wa kituo cha kati, Dar es salaam.
 
Kuna ukakasi juu ya hayo maandamano kama kweli lile kundi litoke huko lilikotoka mpk kufika eneo la ubalozi bila kusambaratishwa polisi waje walikute tayari eneo la tukio kama itakuwa hivyo kile kiitwacho intelijensia ya polisi inabidi tuwe na mashaka nayo maana ni aidha huwa inatumika isivyo au huwa ni fix tu

Lakini kweli tuwapongeze kwa kutomwaga damu maana risasi kata kona zingeleta mengine, tuwasubirie watu waliokamatwa mahakamani kama Kamanda Mambosasa alivyosema
 
Yalikuwa maandamano ya UVCCM na bashite kwa hiyo ulitegemea kuna mtu angeumia?, subiri waandamane bavicha ndiyo utajua policcm
UVCCM mwananyamala, kuna CCTV tena zipo HD, ubalozi wa afrika kusini wametengeneza video na sura zinaonekana vyema kabisa, hawa CCM kindakindaki, wao wanasifia tu, hata kunya barabarani, machinga kupika posta katikati kwa maji ya AC/AIR CONDITION wao sawa tu
 
IPO tofauti ya kuyatawafanya maandamano ya ccm na ya upinzani. Ya ccm huwa yanatawanywa baada ya lengo La maandamano kutumia kufikisha ujumbe pia intelligence huwa iko likizo wala hayahitaji kibali zaidi ya nia ya maana iwe ni kuunga juhudi pia huwa hakuna majeruhi.Ya upinzani kwanza mtihani kupata kibali intelligence lzm itaona viashiria majeruhi wa kutosha msombemsombe na kipigo cha mbwa koko wengine watazindukia nyuma ya nondo.Hizi ndo dabo standard ziondoazo utaifa.
 
Miongoni mwa ujinga wa wazi ni kuamini kwamba Kuna jeshi la polisi kwa ajili ya umma.

Muundo wa jeshi ni kulinda maslai ya wanasiasa kama katiba mpya ikipatikana DC na RC wasiwe ndio wenyekiti wa vyombo vya ulinzi na usalama maana hawa lzm wawe ni makada mmeona ya juzi ya Sabaya hai ,hii itasaidia vyombo viwe huru visiingiliwe na wanasiasa kama ilivo nchi zingine Huwezi kuta polisi wanatumikia chama hata Malawi tu Huwezi kuta polisi wako upande wa chama chochote wao wanaangalia usalama na kuviacha vyama vinyukane Kwa Hoja
 
Pascal polisi hutoa onyo mara tatu,na wale walioonywa walitii amri bila shuruti,ndivyo wananchi inatakiwa tufanye.
Ukikaidi utapigwa tu(Pinda).
Wale wanaharakati wajifunze kwa yaliotokea jana(chadema)
 
Back
Top Bottom