Jesca Magufuli achangia Ujenzi Nyumba ya Katibu UVCCM Wilaya ya Chato. Asisitiza Kumuenzi Hayati Magufuli

Hakuna mtoto wake aliyepata Zero, kutokuwa na hakika ya jibu ni kuropoka!!
Matokeo yaliwekwa humu jf,usijitoe ufahamu kutetea ujinga kisa wewe ni mnufaika.

Mtu mkatili kama yule siwezi mtetea Kwa lolote.

Mwisho nakumbuka Mzee wangu alikaa miaka 2 ndio kuja kupata pension sijui angekufa kabla ingekuja e lakini humwambii kitu kuhusu Magufuli 😆😆😆😆😆
 
"Mimi nikasema si vibaya nikajumuika na vijana wenzangu (UVCCM) Wilaya ya Chato katika ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Chato na kuhakikisha inakamilika, nikasema nichangie kidogo nilichobarikiwa kuhakikisha kazi za Chama na pia siyo mwisho, nitaendelea kuchangia zaidi na zaidi mpaka kuhakikisha nyumba imekamilika kabisa" - Jesca Magufuli (Mtoto wa Hayati JPM)

Jesca Magufuli amesema kuwa amewiwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi vya nyumba ya Katibu wa UVCCM kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za vijana wa CCM ambao wameonyesha dira ya uwajibikaji

Bi. Jesca Mafuguli ametoa vigae kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chato ambayo kwa sasa imefikia Asilimia 90 ya ujenzi huku akiwaasa vijana kuendelea kushirikiana katika Kulijenga Taifa la Tanzania kupitia serikali ya awamu ya Sita.

Naye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka UVCCM mkoa wa Geita, Rubein Saganyika Amewataka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chato kumuenzi Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk John Magufuli kwa kuchapa kazi na kuiishi slogan yake ya Hapa Kazi Tu.

Aidha, Ruben Sagayika amewaomba vijana kuendelea kujitolea kwa ajili ya kukijenga chama ambapo amemushukuru binti wa Hayati Dk Magufuli ambaye ni Jesca Magufuli kwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM Chato.

View attachment 2937331View attachment 2937332View attachment 2937333View attachment 2937335View attachment 2937336
Safi sana ana uthubutu na moyo kama mzee jpm!
 
TANU YOUTH LEAGUE ilikuwa inawalea vijana kuwa wazalendo, lakini UVCCM ya leo inawafunza vijana kuwa majambazi ma mafisadi kupitia siasa.

UVCCM ndiyo chanzo cha wasiojulikana kupitia green guard.

Ukitaka kuijua UVCCM ya leo, mtazame muuaji Makonda, jambazi Sabaya, fisadi January and the like. Hakuna UVCCM aliyenyoka.

Kusaidia UVCCM, kwa kiasi kikubwa ni kusaidia wahalifu wa kuliharibu Taifa. UVCCM ndiyo genge la uhalifu la CCM. Hawa ndiyo huwa wanatrka watu, wanajeruhi na wakati mwingine hata kuua.

Tanzania ingekuwa nafuu zaidi bila ya UVCCM. Bila ya UVCCM, watanzania wengi wangekuwa hai mpaka leo.
 
Back
Top Bottom