Jerry Muro Kurudi Tena TBC

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1][/h]
Jerry Muro Mtangazaji/Mwandishi wa habari ambae alisimama kufanya kazi kwa miezi kutokana na kesi ya kuomba rushwa, kesi ambayo baadae alitangazwa kushinda, ametangaza kituo chake cha kazi baada ya wengi kutomuona kwa muda TBC alikokua akifanya kazi.


Jerry amesema anarudi kufanya kazi TBC na jumapili hii saa tatu na nusu usiku ndio kipindi chake cha kwanza kitaanza kuonekana ambapo kitakua kinaingia kwenye siasa, afya, Uchumi na mengine.


Kuhusu kuendelea kutoa habari zake za kufichua maovu, Jerry amesema “ni kazi ambayo iko kwenye damu yangu unajua watu wanaweka matuta barabarani lengo ni kufika mbali japo utafika sehemu utapunguza spidi unaruka tuta unakwenda, sasa hivi tutaifanya kwa ubora zaidi lakini pia sio siku zote tu tuchunguze chunguze kuna saa nyingine inabidi utoe breki alafu uangalie”


Kwenye sentensi nyingine Jerry amethibitisha kwamba wakati alipokua kimya baada ya kushinda kesi kuna vituo vingi vya TV Tanzania ambavyo vilitaka kufanya kazi na yeye lakini alishindwa kwa sababu vituo vingi sasa hivi vinafanya kazi kwa makundi ya kisiasa, vingine vimeegemea upande mmoja ndio maana akaamua atumikie kwanza wananchi.


“Sio kwamba TBC ndio mwisho wangu lakini ni sehemu ambayo naweza kukaa na kuangalia nakwenda wapi nafanya nini sehemu gani, kila kitu lazima kiwe na mwanzo kwa hiyo hilo kwangu ni mwanzo tu lakini kama nafasi nzuri zitajitokeza basi zitapewa nafasi” – Jerry Muro


CHANZO-MJENGWA BLOG

34209281-3149784212832667478
 
Wamemlipa Pesa kwanini arudi huko? Ni Bado Iko Chini ya Serikali ya CCM; Watamfukuza kwa AIBU; TIDO MHANDO yuko

Wapi?
 
Labda kama amepata haki zake fine, ni maamuzi yake kuchagua mahala pa kufanyia kazi!
 
Unauhakika lakini na hili?, maana hata wewe kama mtayarishaji wa vipindi, unaweza kutumiwa na shirika au kampuni yeyote uwatengenezee kipindi kwa makubaliano yenu, wao wanapeleka channel yeyote kununua airtime na kurusha, kama vile Kibonde na kipindi cha NHC. Yeye akuonyeshe mkataba wa kazi na TBC ndio utasema anarudi TBC
 
Labda Lau Masha Mbabe hayupo tena serikalini, lakini utazuiwa kusema Ukweli ndani ya hicho chombo
 
vema jerry Muro mimi ninaamini msemakweli siku zote mpenzi wa MUNGU fanya kazi kwa kujiamini lakini kuwa makini na watu hawa wasiotaka ukweli.
 
pengine ataendelea pale alipoishia. Lakini nafahamu ya kuwa TBC1 inalipa vizuri kulikoni vituo vingi vya TV.....na mazingira ya kufnyakazi ni bora zaidi........................
 
sasa hivi atajiepusha na issue za kuibua maovu.
Napenda kuwajulisha wanamabadiliko kuwa kuanzia jumapili tarehe 10 mwezi huu,saa tatu na nusu usiku nitaanza kurusha mfululizo wa vipindi vyangu TBC,lengo la vipindi hivi ni kuonyesha kazi mbalimbali zilizofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi ya mkapa foundation haswa katika masuala ya afya.
Vipindi pia vitaonyesha changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo katika sekta ya afya ili kwa pamoja tuweze kuzitatua haswa katika maeneo ya pembezoni mwa nchi(vijijini).
Vipindi hivi nimefanya mwenyewe na kampuni binafsina vitarushwa TBC kwa ufadhili wa mkapa foundation.
Napenda ieleweke,mimi jerry muro sijaajiriwa TBC bali narusha vipindi vyangu pale kwa muda wa miezi miwili na nusu.
Mashabiki na wapenzi wa kazi zangu karibu tutazame ili pamoja tuweze kukabiliana na changamoto zinazolikumba taifa letu na hatimae tuweze kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
Naomba kuwakilisha,
Jerry muro.
 
kila la kheri jerry,majaribu ni mtaji kwa binadamu!chapa kazi,kuwa makini na watu!maana duniani kuna watu na viatu!
 
Hapo anaporudi sijui kama atadumu! Wanamtafutia pa kumpa pigo la mwaka, akae na Tido apate story. By the way nimegundua naye ni mganga njaa u.
 
Jerry Muro Mtangazaji/Mwandishi wa habari ambae alisimama kufanya kazi kwa miezi kutokana na kesi ya kuomba rushwa, kesi ambayo baadae alitangazwa kushinda, ametangaza kituo chake cha kazi baada ya wengi kutomuona kwa muda TBC alikokua akifanya kazi.


Jerry amesema anarudi kufanya kazi TBC na jumapili hii saa tatu na nusu usiku ndio kipindi chake cha kwanza kitaanza kuonekana ambapo kitakua kinaingia kwenye siasa, afya, Uchumi na mengine.


Kuhusu kuendelea kutoa habari zake za kufichua maovu, Jerry amesema "ni kazi ambayo iko kwenye damu yangu unajua watu wanaweka matuta barabarani lengo ni kufika mbali japo utafika sehemu utapunguza spidi unaruka tuta unakwenda, sasa hivi tutaifanya kwa ubora zaidi lakini pia sio siku zote tu tuchunguze chunguze kuna saa nyingine inabidi utoe breki alafu uangalie"


Kwenye sentensi nyingine Jerry amethibitisha kwamba wakati alipokua kimya baada ya kushinda kesi kuna vituo vingi vya TV Tanzania ambavyo vilitaka kufanya kazi na yeye lakini alishindwa kwa sababu vituo vingi sasa hivi vinafanya kazi kwa makundi ya kisiasa, vingine vimeegemea upande mmoja ndio maana akaamua atumikie kwanza wananchi.


"Sio kwamba TBC ndio mwisho wangu lakini ni sehemu ambayo naweza kukaa na kuangalia nakwenda wapi nafanya nini sehemu gani, kila kitu lazima kiwe na mwanzo kwa hiyo hilo kwangu ni mwanzo tu lakini kama nafasi nzuri zitajitokeza basi zitapewa nafasi" – Jerry Muro


CHANZO-MJENGWA BLOG

34209281-3149784212832667478

sasa TBC ndo haijaegemea chama chochote?? jerry muro kweli keshadata....hata chekechea wanajua tbc imeegemea chama gani ndo ije kuwa wewe jerry muro??? kweli ushadungwa sindano ya sumu...
 
Pole sanA jerry Muro.

Maisha ni safari ndefu ambayo hujui nani ni watu kwako na nani ni maadui. Kikubwa ni kuwa makini kwa kumtegemea Mungu maana wakati unaposali na kusoma neno la Mungu kila siku angalau mistari michache nayo inakupa mwanga wa maisha. Hata wakati mwingine mtu akija kwako akimwakilisha shetani yaani utamwona hivi hivi kwamba huyu ni shetani na kwahiyo hatafanikiwa kukudanganya.

Mapito uliyopitia Mungu aliruhusu ili upate kujifunza somo kubwa maana hata YESU alifikishwa Mahakamani.
So Usikate tamaa wala kuona kwamba umepitia jambo baya ni mapito tu na Mungu amekuandalia jambo zuri sana mbele yako.

Jipe moyo na endelea mbele ukimtegeme Mungu wakati unaporudi kazini kwako.

Kumbuka kutoa SADAKA YA SHUKURANI MAADA YA KUSHINDA CASE YAKO
 
Back
Top Bottom