Jengo la mahakama ya rufaa lauzwa kwa kempisky hotel?

Mama PC

Member
Nov 2, 2010
44
2
Nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa Mahakama ya Rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA KWA KEMPISKY HOTEL. Nikaelekezwa nimuone engineer wa Mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni Mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa Mahakama na huyo mwenye Kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na Gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa Jaji mkuu mstaafu na Jakaya.

Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya Rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.
 
Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo.
Kwa kasi hii historia ya nchi yaweza kufutwa na watu wachache wenye uchu wa mali kwa manufaa yao binafsi! Wadau wa Antiquities Department msikubali tena uvamizi huu kufanyika kirahisi namna hiyo kama vile ilivyotokea kwa jengo la Salamanda. It is entirely unjustifiable to "give away" such a historical building just like that to a private investor for whatever a reason. Hakika mamlaka "iliyo juu" haitawaacha watu wanaofuja mali za uma watese daima. Mwisho wao uko karibu na kila kitu kitakuwa wazi!
 
Nikweli lile jengo liko katika hatua za mwisho kuuzwa. Maafisa wa idara ya antiquities walifanya jitihada zote za kulinusuru lakini imeshindikana. Mkuu wa kaya hajui na wala haoni umuhimu wa majengo ya kihistoria. yeye anaona ni kurudisha nyuma maendeleo
 
mhh so funny, hivi hao viongozi wenu wanajua kwamba watalii wengi wanasafiri kutoka nchi moja kwenda nyengine kwa ajili ya kuona majengo ya kale?(history). wajukuu zetu watakuwa wanahadithiwa tuu bila ya kuona hayo majengo, sitashangaa kule kaole magofu yote yakapigwa nyundo.

shame on you Jakaya Kiwete.
 
Nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa Mahakama ya Rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA KWA KEMPISKY HOTEL. Nikaelekezwa nimuone engineer wa Mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni Mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa Mahakama na huyo mwenye Kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na Gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa Jaji mkuu mstaafu na Jakaya.

Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya Rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.

Karibuni wawekezaji wote tuchume shamba la Bibi
Babu kesha kufa Bibi hana macho wala hasikii tena
Vijana wanalishwa pipi, na viongozi wanapewa chipsi kuku tu
Nchi haina wenyewe, Njooni njooni kabla ya Dr wa ukweli hajaishika

Miye JK niandalieni makazi kwenu, kwa sababu kuna vichaa wamepanga kunishtaki
Miye msinijengee tena Saudia, Vijana wa huko wamecharuka
Uturuki naona inafaa, Tuswali wote
Nchi haina wenyewe, Njooni Njooni kabla Dr wa Ukweli hajaishika.

Kuna vichaa wanafanya maandamano, dawa yao iko jikoni Nimemkabidhi Nape
Nitapeleka kundi langu huko JF, wasifurukute hata nitawalipa kwa malaki
Dua la kuku halimpati mwewe, Ninawaambie njooni tutafune
Nchi haina wenyewe, Njooni Njooni kabla Dr wa Ukweli hajaishika.
 
kama huku nje mambo yako hivi hapo magogoni ofisini pakoje,
kuna kilichobaki kweli? au kuna DOWANS nyingi mitaani hatujazigundua
 
Nikweli lile jengo liko katika hatua za mwisho kuuzwa. Maafisa wa idara ya antiquities walifanya jitihada zote za kulinusuru lakini imeshindikana. Mkuu wa kaya hajui na wala haoni umuhimu wa majengo ya kihistoria. yeye anaona ni kurudisha nyuma maendeleo
 
weka huo waraka hata kwa scanner za kulipia huwezi kukosa ele ya kufanyia scanning
 
Kwa taarifa hii kuhusu Serikali yetu isivyo makini na inayodabganywa na pipi huku ikiibiwa madini sishangai wala sijiulizi mara mbili kuamini.Kweli wananchi wa Tanzania tutaendelea kuwa masikini mpaka siku ya mwisho.
 
As a nationa, Tanzania hawana uwezo wa kujijengea jengo jipya la Mahakama na kuacha jengo la linalouzwa kwa vizazi vijavyo? Aibu gani hii that nchi yenye rasilimali nyingi (madini etc) tunafanya tunajengewa jengo na 'mwekezaji'? And after nyuma za serikali nilifikiri watu wamejifunza, obviously not!
 
daaahh..tumekwisha. tutabaki na nini? huko vijijini wawekezaji wanachomewa mashamba na matractor sababu ya ubadhilifu wa viongozi wetu. hapa mjini tufanye nini juwaadabisha hawa watu.
 
Nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa Mahakama ya Rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA KWA KEMPISKY HOTEL. Nikaelekezwa nimuone engineer wa Mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni Mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa Mahakama na huyo mwenye Kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na Gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa Jaji mkuu mstaafu na Jakaya.

Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya Rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.

Roho inauma jamani mtaniua,mmm.
 
Nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa Mahakama ya Rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA KWA KEMPISKY HOTEL. Nikaelekezwa nimuone engineer wa Mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni Mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa Mahakama na huyo mwenye Kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na Gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa Jaji mkuu mstaafu na Jakaya.<br />
<br />
Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya Rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.
<br />
<br />
Tuwekee huo waraka na sisi tuuone
 
Hali ikiendelea hivi, Sitashangaa nikisikia Mnazimmoja nayo imepata 'mwekezaji'
 
Huwa Nyerere nae angeuza leo wao wangeuza nini?leo tungeridhi nini?leo wangepata wapi viburi hivi?wawe wazalendo kama waliotangulia wajifunze katika kosa la kuuza nyumba za serikali
 
Hadithi ya "mchezo mchafu" iliyotolewa miaka karibu nane iliyopita, kuhusiana na uuzwaji wa Kilimanjaro hotel inaelekea ilikuwa ya ukweli.

Ilianza hiyo, tukaambiwa na kama ilivyo kawaida yetu tukaipuuza, at most tukatumia msemo huo ( mchezo mchafu) kwa kejeli bila kujua kuwa ujumbe uliomo humo ndani ya huo msemo ni saratani mbaya sana. Ikaja Zanzibar, nasikia huyu bwana kauziwa afisi ya serikali ilikowa afisi usajili wa vizazi na vifo, na nasikia inataka kuwa hoteli ya nyota tano, inaelekea kupitwa bila watu kuhoji.

Muwekezaji kanogewa, kaona kuwa jengo la Mahakama ya Rufaa linafaa kuwa hoteli, kalinunua.

Walahi hii ni maajabu ya mwaka. Tunauza majengo ya kutolea haki ya wananchi kwa muwekezaji, akitaka kununua ikulu tutamkatalia kweli???????

Maswali matatu ningependa tuyajadili:

1. Je mpaka kufikia uamuzi huo wa kuuza mali ya serikali, Je serikali ilifuata sheria ya manunuzi?

2. Je ni kweli serikali imeshindwa kutumia rasilimali zake kujenga jengo la kutolea haki kwa serikali mpaka iende kumpigia magoti mwekezaji?

3. Huyu mwekezaji atanyimwa haki akiingia kwenye jengo ambalo yeye mwenye kalijenga?

Kama hii ni kweli basi ni kashfa ya karne, imbayo tutaweka kwenye kumbukumbu za taifa wakati wa sherehe za miaka 50 ya Uhuru ( ambao haupo anyway).
 
Mwekezaji ananunua Jengo la Mahakama ya Rufaa..kuna siku watanunua Ikulu hawa wawekezaji kwa madai ya kipuuzi kama hayo
 
Back
Top Bottom