Jengo la mahakama ya rufaa lauzwa kwa kempisky hotel?

Sasa kama hata jumba la kutolea HAKI nchini linaweza kuuzwa kinyemela tu kwa mfanyabiasha yeyote alimradi kaonyesha jinsi vijisenti vilivyojaa mfukoni mwake, je HAKI yenye ambayo ndio bidhaa pekee inayotolewa na mahakama yoyote duniani kweli itakosa kuwa exclusive right ya matajiri peke yao nchini huku akina yakhe ndio tukiendelea kuswekwa lupango kwa idadi ya kutisha????????????

Kikwete, rudisha jengo letu la mahakama haraka ili ufanisi wa kuendesha mikesi kwa haraka na haki zaidi ipate kuongezeka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Natamani majengo yote ya serikali na wizara zilizoko city centre ziuzwe ziwe hotel za kitalii

Halafu serikali yote ihamie dodoma, yaani wakiuza wanajengewa jengo dodoma wanatimka mjini

foleni itapungua tutapua tufanye kazi..
 
Punguza kidogo hamaki; kweli najua mambo mengine yanavyochefua watu kusikia. Yaani, hata kwa taasisi ya mahakama nchini nako CCM huingiza ufisadi wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Natamani majengo yote ya serikali na wizara zilizoko city centre ziuzwe ziwe hotel za kitalii

Halafu serikali yote ihamie dodoma, yaani wakiuza wanajengewa jengo dodoma wanatimka mjini

foleni itapungua tutapua tufanye kazi..
 
Huna haja ya kupiga huo waraka picha, kwa nini husi-scan to PDF file kisha weka hapa? Kesho utakuja na kusema betri iliisha nguvu, hukuweza kupiga picha.
 
Lowassa kweli wanasema ni mwizi lakini wakati mwingine ana uzalendo; nakumbuka hapo siku za nyuma wakati Kitwana Kondo alipotaka kumuuzia mfanyabiashara mmoja viwanja vya mnazimmoja, Lowassa was instrumental kuhakikisha kuwa ile dili Kitwana hakuifanikisha kwani vijana waling'oa uzio wamabati [ kwa instructions za Lowassa] uliokuwa umezungushswa mnazi mmoja tayari kwa kuanza ujenzi!! Mtoto wa mkulima hana ubavu huo ,yeye yupo yupo tu!! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni jamani.
 
Huyu rais kama naye anahusika basi watz tukae mkao wa kula hata pale magogoni patauzwa kwa sababu za kiusalama kuwa pamezungukwa na majengo marefu na sasa mkuu wa kaya hana faragha!
 
Duuh hii hatari watawekezwa hadi wananchi sasa.



nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya mahakama ya rufaa na mahakama kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa mahakama ya rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni uuzwaji wa mahakama ya rufaa kwa kempisky hotel. Nikaelekezwa nimuone engineer wa mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa mahakama na huyo mwenye kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa jaji mkuu mstaafu na jakaya.

Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.
 
Nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa Mahakama ya Rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA KWA KEMPISKY HOTEL. Nikaelekezwa nimuone engineer wa Mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni Mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa Mahakama na huyo mwenye Kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na Gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa Jaji mkuu mstaafu na Jakaya.

Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya Rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.


Huyo mwekezaji kwa nini asiazishe biashara ya crusie ship dar- kigamboni kule kwenye eneo lake lingine.

Anununue na huo ufukwe atoe hayo mameli mabovu mabovu

Ningependa kusikia hilo jengo jipya linajengwa Dodoma. Gymkahana tena mhhh madudu juu ya madudu

Kuna madudu mengine unaweza kukubaliana nayo kama yakifanywa kwa njia bora. Sioni sound reason ya kuhamishwa hapo alafu kwenda ghymkhana .
 
Huyo mwekezaji kwa nini asiazishe biashara ya crusie ship dar- kigamboni kule kwenye eneo lake lingine.

Anununue na huo ufukwe atoe hayo mameli mabovu mabovu

Ningependa kusikia hilo jengo jipya linajengwa Dodoma. Gymkahana tena mhhh madudu juu ya madudu

Kuna madudu mengine unaweza kukubaliana nayo kama yakifanywa kwa njia bora. Sioni sound reason ya kuhamishwa hapo alafu kwenda ghymkhana .

majungu kuna watu wanatafuta vyeo kwa njia chafu
 
wanaJf hebu tuache porojo kwa hili. jengo la mahakama ya rufaa ilipo sasa ilikuwa ni hotel.
Mahakama ya Rufaa walikuwa wanatumia jengo moja na mahakama Kuu hapo walihamia
miaka michache iliopita nadhan 2005 kama sijakosea kwa vile kule mahakama kuu kuna uhaba
wa vyumba vya majaji ikabidi majaji wa mahakama ya rufaa wahamie jengo jipya
zamani lilikuwa hotel pale nako hapana hadhi ya kuwa mahakama ya rufaa.
Mpango wa kujengewa mahakama ya rufaa ulikuepo tangu zamani.Itakuw ajambo la kheri
kama mwekezaji huyo kaaamua kuwajengea jengo jipya lenye hadhi ya kisasa itakua vema
na serikali itajipunguzia mzigo wa kujenga wenyewe.Kama mlishawahi kufika pale mahakama
ya rufaa chunguzeni vema jaji anakaa kachumba kadogo nk.Kusema ni hifadhi ya majengo
ya zamani kwa hili nawakatalia kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.Ingekuwa inauzwa mahakama kuu
pale ningewaunga mkono kulalamika. mkitaka details zaidi mwoneni msajili wa mahakama
ya rufaa mtapewa maelezo.lazima tukubali maendeleo wanaJF. cha kujiuliza hapa tuelezwe kama
kutakuwa na uwazi ktk makubaliano hayo na kama hakuna ufisadi au kukiukwa kwa sheria.
sina hakika kama lile jengo waliuziwa mahakama ya rufaa ninachofahamu walipewa kwa muda
hadi hapo watakaojenga la kwao.Lakini kwa vile ni majengo ya serikali tusianze kualaumu mahakama
kuwa jengo limeuzwa wakati sii lao.
 
Karibuni wawekezaji wote tuchume shamba la Bibi
Babu kesha kufa Bibi hana macho wala hasikii tena
Vijana wanalishwa pipi, na viongozi wanapewa chipsi kuku tu
Nchi haina wenyewe, Njooni njooni kabla ya Dr wa ukweli hajaishika

Miye JK niandalieni makazi kwenu, kwa sababu kuna vichaa wamepanga kunishtaki
Miye msinijengee tena Saudia, Vijana wa huko wamecharuka
Uturuki naona inafaa, Tuswali wote
Nchi haina wenyewe, Njooni Njooni kabla Dr wa Ukweli hajaishika.

Kuna vichaa wanafanya maandamano, dawa yao iko jikoni Nimemkabidhi Nape
Nitapeleka kundi langu huko JF, wasifurukute hata nitawalipa kwa malaki
Dua la kuku halimpati mwewe, Ninawaambie njooni tutafune
Nchi haina wenyewe, Njooni Njooni kabla Dr wa Ukweli hajaishika.
Hii nimeipenda
 
Imefikia mahali ambapo itabidi tuwaige ndugu zetu walichofanya North Mara. Huu sasa ni UJINGA
 
Back
Top Bottom