Jee Bunge La Dharura Kuitishwa?

Pasco,
Nasikia mmeitwa ikulu, bila shaka cabinet imesukwa hadi ikasukika.
Mwita, wanaoitwa Ikulu ni waandishi toka media organization!. Mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea. Sijaajiriwa na media yoyote, silipwi na media yoyote wala situmikii media yoyote hivyo kualikwa ni vigumu!.
 
Last edited by a moderator:
Kwa mtazamo wa haraka uneza dhani haiwezekani but tanzania siasa ni zaidi ya sheria so inawezekana kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Ni lini JK alivunja katiba?
Mkuu Gaijin, ni mara kibao tuu JK amevunja katiba na salama yake kutoshitakiwa ni kwa sababu ana kinga ya kutoshitakiwa!.

Kosa sio lazima uvunje sheria hata kuzuia utekelezaji wa sheria kwa mujibu wa katiba pia ni uvunjaji wa katiba na ni kwenda kinyume cha kiapo chake kwamba atailinda na kuitetea katiba ya JMT!.

JK alipoisamehe ile mijizi ya EPA, alitumia sheria gani?!. Mwizi wa kuku anaiwawa kinyama, mijizi ya rasilimali zetu ndio ina peta kwenye ma vogue!.

Tangu lini mwizi anaambiwa arudishe alichokwiba na kusamehewa!?. Huku ni kuzuia sheria kuchukua mkondo wake ambao ni uvunjaji wa katiba!.

Sababu pekee ya msamaha ule ni kuepuka kulikata tawi ulilolikalia!. Nchi za wenzetu wenye private prosecution, JK angekuwa prosecuted in person privately kwa sababu immunity yake inaishia katika utekelezaji wa maamuzi yoyote kwa mujibu wa katiba na inakomea hapo uvunjaji wa katiba hauna immunity!.

Sheria mpya ya Katiba inatamka wazi wabunge wasiwe wajumbe, juzi kamteua mbunge simply eti ni special group!. Kundi hilo lina watu wangapi wazuri tuu mpaka amcholopoe mbunge as if she is the one and only!.

Tanzania tuna bahati wanasheria wetu wengi ni after money, kwa vile hakuna wa kumlipa advocate kufungua kesi kama hiyo, JK anapeta tuu wote kimya tukiendelea kumsifia kwa kumuimbia nyimbo za shangwe na mapambio!.

Baada ya October 2015, tusifanye masikhara patakuwa hapatoshi!.

Pasco!.
 
Pasco bunge la dharura ni kama JK ataunda baraza jipya la mawaziri meaning mpka waziri mkuu kubadilika! nachoona hapa ni kutiwa viraka tu na mabadiliko madogo ya baraza lililopo,, PM hatobadilika
 
Pasco jibu magirini matupu
Mkuu Gaijin, humu jf tunapinga hoja kwa hoja. Nimekupa swali JK alipoyasamehe majizi ya EPA alitumia kifungu gani?. JK anayo mamlaka kuizuia sheria isichukue mkondo wake?.

Katiba inasema rais kwa mashauriano na waziri mkuu atateua mawaziri miongoni mwa wabunge. Mbunge mteule anakuwa mbunge pale tuu baada ya kuapishwa!. Unless hata mbunge mteule ni mbunge tuu hata kabla ya kuapishwa!.

Uteuzi wa wabunge hao wapya umefanyika kwa mujibu wa katiba ila hao ni wabunge wateule. Pia kuwateua kuwa mawaziri pia ni kwa mujibu wa katiba. Kwa tafsiri yangu mimi, hawezi kuwaapisha kuwa mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge!.

Huo nao ni uvunjaji wa katiba!. Kwa jinsi tulivyojaza wanasheria vilaza, hakuna wa kumshauri rais kuwa mbunge mteule si mbunge mpaka ale kiapo!.

Kama alivyousamehe ile mijizi, hakuna alimwambia rais kuwa hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake, kama aliwapenda sana angeacha sheria ichukue mkondo wake halafu kwa mamlaka yake akawasamehe!.

Mamlaka ya rais ni kusamehe wafungwa sio kuisamehe mijizi kabla haijafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Ule ulikuwa uvunjaji wa katiba na akiwaapisha wabunge wateule kuwa mawaziri kabla hawajawa wabunge nao ni uvunjaji wa katiba!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom