Waziri Bashungwa atoa maelekezo kwa TANROADS kukarabati mifereji, Novemba 7, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 13, Kikao cha 7, leo Novemba 7, 2023.


NAIBU WAZIRI: CHANGAMOTO YA MTANDAO WA VODACOM IMEATHIRI WATU MILIONI 1.8
BUNGENIWizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akijibu swali la Mbunge Dkt. David Mathayo David kuhusu changamoto ya Mtandao wa Vodacom iliyotokea Novemba 6, 2023 amesema “Changamoto ya kiufundi iliyotokea kwenye Kampuni ya Vodacom iliathiri kupiga, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kufanya miamala ya fedha hivyo kuathiri wateja milioni 1.8.”

MBUNGE ADAI ASKARI WA MWEKEZAJI EFATHA MINISTRY WAMEWAJERUHI WANANCHI KWA RISASI
Mbunge wa Kwela, Deus Clement Sangu amesema mgogoro wa Ardhi uliopo kati ya Wananchi na mwekezaji Efatha Ministry katika Kijiji cha Skaungu, Kata ya Msanda Muungano umesababisha Wananchi kujeruhiwa kwa risasi, matukio ya ubakaji na vifo, akidai hakuna hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Ardhi licha ya kufikisha malalamiko mara kadhaa

Akizungumza Bungeni, Sangu amesema “Jana (Novemba 6, 2023) Askari wanaolinda shamba la mwekezaji wamewapiga risasi za moto Wananchi wakiwa shambani na kuwanyang’anya ngombe 42, mmoja amepigwa risasi 5 kichwani na hali yake si nzuri, mwingine kapiga risasi tumboni mwingine shavuni.”

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo kwa njia ya dharura, Naibu Waziri wa Ardhi, Geofrey Pinda amesema “Maelezo ya Mbunge ni kweli, natoa pole kwa waathirika wote, niwaombe wawe na utulivu, Serikali inaenda kuchukua hatua za haraka kuondoa migogoro ya Ardhi kati ya Wananchi na wawekezaji.”


BASHUNGWA ATOA MAELEKEZO KWA TANROADS
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amewaagiza Mameneja wa Mikoa wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mikoa yote nchini kukarabati mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuu ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua ikiwemo kuharibika kwa barabara.

Bashungwa ametoa agizo hilo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta aliyeuliza kuhusu ni lini Wizara Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi itasafisha mifereji iliyozibwa wakati wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo.

“Nitumie nafasi hii niwaelekeze Mameneja wa TANROADS mikoa yote nchini kufika kwenye maeneo ambayo yana changamoto kama Wabunge walivyosema na kuona namna ambavyo tunaweza kukakabiliana na jambo hili kwa dharura na haraka, Serikali inajipanga kutafuta namna ya kuwaondolea adha ya mafuriko Wananchi katika barabara ya Mwenge”

Soma >>> DOKEZO - Barabara za Mitaa jimbo la Segerea ni mbovu, zinajaa maji na hazina mitaro
 
KAPIGWA RISASI 5 KICHWANI NA HALI YAKE NI MBAYA!!!! 🙄🤔😳
 
Back
Top Bottom