Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,599
Wanabodi,
JK ameteua wabunge watatu wapya na kuna uwezekano wawili kati yao atawateua mawaziri!.
Ili mtu kuteuliwa waziri lazima kwanza uwe mbunge. Mtu akiteuliwa Mbunge, hawi mbunge bali huwa mbunge mteule mpaka baada ya kuapishwa!.
Mbunge mteule hawezi kuteuliwa kuwa waziri mpaka kwanza awe mbunge!.
Hivyo jee kutaitishwa kikao cha bunge la dharura ili hao wateuliwa wapya waukwae uwaziri, au JK atatuvunjia tena katiba kwa kututeuliwa mawaziri ambao sio wabunge bali ni wabunge wateule?!.
Ila kama atambadili PM basi ni lazima kwanza bunge la dharura likutane kupitisha jina la PM, then PM na Rais ndio wakae chini kupendekeza baraza la mawaziri!.
Subirieni taarifa ya kikao cha bunge la dharura!.
Pasco.