Je, wananchi wanapaswa kuziamini mahakama hasa kwenye kesi za kisiasa?

kenethedmund

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
347
89
Napenda kutoa mada tajwa hapo juu, Je wananchi wanapaswa kuziamini mahakama hasa kwenye kesi za kisiasa.
Nasema hivi kulingana na hukumu iliyotolewa kuhusu uchaguzi na kuenguliwa kwa mbunge wa Arusha Godbless Lema, vifungu vilivyotumika na Jaji vinatia mashaka, na vinahoji credibility ya Judge alipoitoa hukumu hiyo.

vilevile napenda kueleza usiri wa hukumu hiyo haukuwepo kwani taarifa zilienea sehemu mbalimbali watu wakijua kuwa Lema atashindwa na kuenguliwa ubunge.

Napenda kumalizia kwa kuuliza swali je - mahakama zinapaswa kuaminika kwenye hukumu hasa kwenye kesi za kisiasa ?

Kama hapana wananchi wanapaswa kutumia hatua gani ili kulinda haki zao za kuchagua muwakilishi wao ?
 
CCM ni adui wa HAKI,ni adui wa Demokrasia.
DAWA YAKE: Kuchagua upinzani, has CDM.
 
Hivi hili swali ungeliuliza hata kama habari zingevuja na Judge angejikanganya katika vifungu kama verdict ingekuwa on favour ya Lema?
 
tangu walipomfunga babu seya na wanae na kesi ya akina zombe na hii sina imani nao tena.
 
Hivi hili swali ungeliuliza hata kama habari zingevuja na Judge angejikanganya katika vifungu kama verdict ingekuwa on favour ya Lema?

Kwa hali ya nchi ilivyo, kumpoteza mbunge mmoja wa CDM ni hasara kubwa sana. Mbunge mmoja wa CDM ni sawa na wabunge 20 wa CCM. Kwa hiyo swali lililoulizwa lina umuhimu sana. Favour yoyote kwa mbunge wa CDM ni halali maana wanafanya kazi kubwa kweli ya kutetea wananchi. Sio sawa na wabunge wa CCM wanaokwenda bungeni kusinzia, wakistuka wanapiga meza ku-support bila kujua kilichokuwa kinazungumzwa. Miaka 50 ya kuwepo madarakani hakuna tatizo lililopatiwa ufumbuzi likamalizika. Mtu yeyote anayeendelea kui-support CCM ktk zama hizi, mtu huyo ni msaliti mkubwa wa taifa letu.
 
Tusifanye siasa kwenye sheria.Tatizo kubwa la Watanzania ni kujump kwenye conclusion.Katika kesi ya Lema wale waliokuwa wanakwenda mahakamani na kufuatilia mwendendo mzima wa kesi ile ndio walitueleza kuwa Lema anapoteza kiti.Kwa bahati mbaya Kitanzania ubashiri wa mwenendo wa kesi ulikwenda sambamba na hukumu, HAPO TENA IMEKUWA ISSUE.Lazima tuwe na imani.
 
Nadhani mahakama ni mhimili ambao hata usipopenda kuamini outcomes ya maamuzi yake bado tunapaswa kuendelea kuziamini, cha msingi tu ni pale tunapoona hatujaridhika na maamuzi husika kwenda the next step. Kimsing bado kuna changamoto nyingi nyingi unapoongelea judiciary independence, kwani the president who is the head of the executive ni ndiye mwenyekiti wa chama kinachoongoza dola, ndiye huyu huyu anayeteua na kuwaapisha majaji.
 
Back
Top Bottom