Usiposomewa Maoni ya Wazee wa Baraza kwenye Kesi za Ardhi, kesi nzima inakuwa batili

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
Usiposomewa Maoni ya Wazee wa Baraza kwenye kesi za ardhi, hiyo kesi nzima ni batili

Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241

Kwa wale ambao mna kesi za ardhi katika mabaraza/mahakama za wilaya mnapaswa kujua kuwa ni lazima kusomewa maoni ya wazee wa baraza kabla ya kusomewa hukumu.

Kutokusomewa maoni ya wazee wa baraza ni kosa kisheria na inabatilisha kesi nzima.

Hivyo ikiwa umekuwa na kesi baraza la ardhi la wilaya, na hukumu imesomwa na kabla ya hukumu wazee wa baraza hawakujitokeza kuwasomea maoni yao, basi kesi hiyo nzima ni batili na hivyo ukikata rufaa kwa kigezo hicho utashinda.

Kesi zote za ardhi mbele ya mahakama/mabaraza ya ardhi ya wilaya (DLHT) husikilizwa na Hakimu/Mwenyekiti pamoja na Wazee wa Baraza.

Kwa uelewa, hapa Hakimu huitwa pia Mwenyekiti na pia mahakama huitwa baraza, yote humaanisha kitu kimoja.

Sasa tujue kuwa ni lazima inaposikikizwa kesi katika mabaraza haya wawepo wazee wa baraza (assessors) na hili ni takwa la lazima kisheria.

Hivyo basi kwakuwa wanakuwepo kwenye kusikiliza basi usikilizaji unapoisha sheria inawataka na wao kutoa maoni yao kwa kueleza nani anashinda na nani anashindwa kutokana na namna walivyosikiliza shauri.

Maoni hayo huwa yanazingatiwa na Hakimu/Mwenyekiti hata hivyo halazimiki kuyafuata na ndio maana yanaitwa maoni (opinion), ikiwa na maana kuwa kuna uhiari, yanaweza kufuatwa au kuachwa.

Hata hivyo, ikiwa Hakimu/Mwenyekiti ameyafuata au hakuyafuata ni lazima aeleze kwenye hukumu, mosi kwamba yalitolewa, na pili kama aliyafuata au hakuyafuata na kwanini.

Pamoja na hayo, kuna jambo moja ambalo limekuwa halifanyiki ambalo sasa unapaswa kulijua ikiwa una kesi ya ardhi.

Jambo hili ni takwa na lazima wazee hao wa baraza kusoma maoni yao mbele ya wenye kesi (parties) kabla ya kusomewa hukumu.

Hili ni takwa la lazima kuwa mnapaswa kusomewa maoni ya wazee wa baraza kabla kusomewa hukumu, ili mpate kujua wao walionaje shauri lenu na walitoa maoni gani.

Ikiwa hamkusomewa maoni ya wazee wa baraza basi shauri lenu lote ni batili, na ikiwa ulishindwa katika shauri la namna hii yafaa ukate rufaa na utafaulu.

Katika Rufaa Na.7/2021 kati ya ATHUMANI HAMIS BENTA vs ISSA MOHAMMED BENTA hukumu iliyotolewa na Mahakama ya rufaa tarehe 29 /9/2023 mahakama imebatilisha shauri zima na kuamuru likarudiwe upya kutokana na kosa la kutowasomea wahusika wa kesi (parties) maoni ya wazee wa baraza.

Maamuzi kama hayohayo pia yametolewa katika Shauri Na.154/2015 AMEIR MBARAKA&WENGINE dhidi ya EDGAR KAHWILI.

Kwahiyo tujue sasa kuwa haya ndio mahitaji ya sheria na kama una shauri la ardhi wilayani basi ni lazima usomewe maoni ya wazee wa baraza ili ujue wao walilionaje hilo shauri.

Ikiwa hawakuwasomea maoni yao na shauri limeisha, basi hii sababu nzuri (ground) ya kukata rufaa kubatilisha shauri zima.
 
Ila kuna maoni mengine ya Wazee wa Baraza ukiyasikiliza unaweza cheka hadi mbavu kuvunjika!! Asante sana kwa taarifa mkuu ubarikiwe sana!!
 
Provision gani ina sema ivyo wanasheria sio essay tu inayo eleweka lazima utoe provisions zinazo eleweka ,hama ni izo precedent tu
 
Wwe nawee, hoja zote zimewekwa pamoja na reference za kesi zilizo aamuliwa before! Sasa wabisha nini!!??
 
Provision gani ina sema ivyo wanasheria sio essay tu inayo eleweka lazima utoe provisions zinazo eleweka ,hama ni izo precedent tu
section 23(1) and (2) and section 24 of the Land Disputes Courts Act , read
together with Regulation 19(1) of the Land Disputes Courts (The District Land and Housing Tribunal) Regulations, G.N. No. 174 of 2002 . Pia usione uvivu msomi kusoma
 
Sahihi,nme pitia
 
Back
Top Bottom