Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,719
- 114,064
Wanabodi,
Kama kawa, leo nimepata fursa kuwaletea makala elimishi ya uchambuzi wangu wa muswada huu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, kwa swali Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili? Je, muswada huu ni mvinyo ule ule wa zamani, kwenye chupa mpya?. Muswada huu una nini kipya? Nini kilichobadilika tofauti na zamani?. Huu ni ubatili mtupu, ila ndani ya ubatili huu pia kuna baadhi ya mambo ni mambo mazuri!
Naomba nianze bandiko hili kwa utambulisho
Mwandishi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea na Wakili wa kujitegemea, ambaye japo ni mhitimu wa LL.B (Hons) ya UDSM, yeye sio wakili msomi, kwasababu haendi mahakamani, huyu ni wakili mtangazaji na muelimishaji umma kuhusu katiba, sheria na haki, kupitia makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" zinazotoka humu JF, baadhi ya magazeti na kipindi cha TV na oline
Nimeanza na utambulisho huo, kwasababu kitendo cha wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, wa serikali wametunga muswada, wamejiridhisha uko ok ndio maana wakauwasilisha Bungeni, ambako nako kuna mabingwa wa sheria, wabobezi na wabobevu nao wakaoona uko sawa na ndio maana wakaruhusu uwasilishwe Bungeni na umeisha somwa kwa mara ya kwanza, halafu akaibuka mtu tuu kuukosoa kwa kuwaambia watu muswada huu ni batili!, lazima watu watajiuliza huyu ni nani?, hivyo huu ni uthibitisho kuwa Tanzania tuna wanasheria wa ajabu sana!. Jambo limeishatamkwa na Mahakama Kuu kuwa ni batili, serikali yetu sikivu inawezaje tena kutuletea ubatili huo huo kwenye hii sheria mpya? Hii sio mara ya kwanza kwa serikali yetu kututungia sheria batili, na niliwahi kuuliza Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?, hivyo zinapokea fursa za kubadili sheria, tuzibe kwanza paa letu, tuzibe matobo ili tuwe salama.
Jee inakuwaje madudu haya yakafanywa na wanasheria wetu?. Jibu ni moja tuu, sheria ni fani bahari, eneo ngumu kuliko yote kwenye sheria ni eneo la kutafsiri sheria, kwa Tanzania mamlaka pekee ya kutafsiri sheria ni Mahakama Kuu ya Tanzania, ila naomba kusema wazi hata Mahakama zetu zimekosea kutafsiri baadhi ya sheria zinazokwenda kinyume cha katiba. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?
Ubatili wa muswada huu, sio ubatili mwingine wowote, zaidi ya ubatili ule ule ninaoupigia kelele humu jukwaani kila uchao, wa serikali yetu kutunga muswada wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Bunge letu Tukufu kuupokea huo muswada batili na ubatili wake na waheshimiwa wabunge wetu kujadili kutunga sheria batili kama mazuzu!
Ubatili huu nimeuzungumza hapa
Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii iyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.
Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.
Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
Muswada huu unatunga Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka, 2023. Kwa ujumla, Sheria hii inaunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292. Hivyo sasa masharti ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani ni sheria moja na kutekelezwa na mamlaka moja ambayo ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hapa ninapendekeza chaguzi zote nchini, uchaguzi wa Rais na Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa, ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume moja Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hili ni jambo jema!.
Muswada huu umegawanyika katika Sura Kumi.
Uchambuzi wangu wa sura kwa sura na maoni yangu
Karibu
Maadam sheria batili hii imeisha somwa kwa mara ya kwanza, nashauri tutoe maoni yetu, pili hoja hizi zizingatiwe
Hayamambo ya serikali yetu kututungia ubatili, na kulipelekea Bunge letu likaubariki ubatili huu kuwa sheria, tutaendelea nayo hadi
lini? Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
na nikasema Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
Hivyo mambo haya yakiendelea, kiukweli kabisa we'll be left with no option but to do something! (ambacho naomba nisikitaje)!.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali

Kwa vile Mkuu wa nchi ni rais wa nchi, hivyo likitokea tatizo lolote, analaumiwa mkuu wa nchi, na madudu yote hayo yalitokea kabla Rais Samia hajaingia madarakani, hivyo nimemjengea indemnity Rais Samia asilaumiwe kwa madudu haya Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.Ubatili huu nimeuzungumza hapa
- Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
- Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?
- Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii iyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.
Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.
Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
Kwenye mada hii pia ninaainisha kwa mukhtaasari, sura zote 10 za sheria hii, ili kuwaelimisha elimu ya uraia, sheria na haki ili tuitumie kikamilifu hii miezi 3 ya kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ya sheria hii.Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
- Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
- Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Muswada huu unatunga Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka, 2023. Kwa ujumla, Sheria hii inaunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292. Hivyo sasa masharti ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani ni sheria moja na kutekelezwa na mamlaka moja ambayo ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hapa ninapendekeza chaguzi zote nchini, uchaguzi wa Rais na Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa, ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume moja Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hili ni jambo jema!.
Muswada huu umegawanyika katika Sura Kumi.
Uchambuzi wangu wa sura kwa sura na maoni yangu
Karibu
HitimishoSura ya Kwanza ya Muswada inahusu masharti ya utanguliziyanayo jumuisha jina la Sheria inayopendekezwa, mawanda ya matumizi,utaratibu wa kuanza kutumika pamoja na tafsiri ya misamiati mbalimbalikwa kadri ilivyotumika ndani ya Sheria inayopendekezwa. Kwa mujibuwa masharti ya Sehemu hii, Sheria inayopendekezwa itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano, na itatumika Tanzania kwa uchaguzi wa Madiwani. Sura hii inajumuisha pia masharti kuhusu ugawaji wa maeneoyaqq uchaguzi na uteuzi wa watendaji mbalimbali wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambao husaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za Tume kamavile uandikishaji wa wapiga kura, usimamizi wa uchaguzi na uratibu wataarifa, upatikanaji wa vifaa, rasilimali na masuala mengine muhimu kwaajili ya kuendesha uchaguzi.
Maoni: Miongoni mwa malamiko, wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa CCM, Wakurugenzi, ma RAS na ma DAS ndio wasimamizi, hawa walikataliwa na mahakama kwenye kesi ya Bob Chacha Wangwe, wasimamizi bado ni hawa hawa!. Nashauri wawekewe watu neutral juu yao.
Sura ya Pili ya Muswada inaweka masharti kuhusu uandikishaji wawapiga kura. Sura hii imegawanyika katika Sehemu Nne ambapo Sehemu ya Kwanza inaainisha sifa za mtu kuandikishwa au kukosa sifa zakuandikishwa kuwa mpiga kura, sehemu ya kupigia kura na mashartikuhusu Daftari la Awali na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Miongoni mwa sifa muhimu za kuandikishwa kuwa mpiga kura zilizoainishwa katika Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge Na Madiwani 2023
Sifa kuu ni kuwa raia wa Tanzania na kutimiza umri wa miaka kumi nanane. Sehemu ya Pili inaweka masharti ya uandikishaji ambayo yanajumuisha muda wa uandikishaji, wakala wa uandikishaji, kadi yampiga kura, utaratibu baada ya mtu kubadili makazi, namna ya kupata kadi mpya endapo kadi ya awali imepotea, imefutika au imeharibika na utaratibu wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura ambao unapendekezwa ufanyike mara mbili kati ya uchaguzi mkuu mmoja na uchaguzi mkuu unaofuata. Sehemu ya Tatu ya Sura hii inaainisha masharti kuhusu utaratibu wa kuweka pingamizi dhidi ya mtu kuandikishwa au dhidi ya jina la mtu kuendelea kubaki katika Daftari. Kwa mujibu wa Sehemu hii, pingamizi dhidi ya uandikishwaji litawasilishwa kwa afisa mwandikishaji. Sehemu ya Nne inajumuisha masharti kuhusu rufaa dhidi ya pingamizi la kuongezwa au kufutwa katika daftari ambapo kwa mujibuwa Sehemu hii, rufaa dhidi ya uamuzi wa afisa mwandikishajizitawasilishwa katika Mahakama ya Wilaya.
Maoni: Kwa vile Sifa kuu ni kuwa raia wa Tanzania na kutimiza umri wa miaka 18, bila shurti jingine lolote, hii ndio haki kuu ya msingi ya uchaguzi ni haki ya kuchagua kwa kupiga kura bila sherti lolote, haki ya kuchaguliwa pia iwe bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.
Sura ya Tatu ya Muswada inaweka masharti mbalimbali kuhusu uchaguziwa Rais na imegawanyika katika Sehemu Tatu. Sehemu ya Kwanza inajumuisha masharti ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais, idadi ya wadhamini wanaopaswa kuwa nao na utaratibuwa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi. Sehemu hii pia inaweka utaratibu wa namna ya kuweka pingamizi dhidi ya mgombea wa kiti cha Urais na Makamu wa Rais. Sehemu ya Pili ya Sura hii inaweka mashartimbalimbali yanayohusiana na taratibu za uchaguzi wa Urais ikijumuishasiku ya uchaguzi wa Rais, watu wanaostahili kupiga kura katika uchaguziwa Rais, sifa za mgombea katika uchaguzi wa Rais, majumuisho ya kura katika uchaguzi wa Rais, mazingira yanayoweza kusababisha upigaji kura kurudiwa na masharti ya kutambulika kwa uchaguzi wa Rais kuwa uchaguzi wa Makamu wa Rais. Ili kuepuka kurudia masharti kuhusu taratibu za upigaji kura ambazo hufanana kwa uchaguzi wa mgombea wa kiti cha urais, ubunge na udiwani, Sehemu hii inaweka sharti la matumizi ya Sura ya Sita ambayo inaainisha utaratibu wa upigaji kura.
Sura ya Nne ya Muswada inaweka masharti yanayosimamia uchaguzi wa Wabunge na imegawanyika katika Sehemu mbili. Sehemu ya Kwanza inahusu sifa za wagombea katika uchaguzi wa Ubunge. Sehemu ya Pili inahusu uteuzi wa wagombea Ubunge ambapo inaainisha siku ya uteuzi, uteuzi wa wagombea, utaratibu wa namna ya kuweka dhamana kwa mgombea wa nafasi ya ubunge, masharti ya mgombea kuteuliwa kwajimbo moja tu, pingamizi na uamuzi juu ya uhalali wa fomu ya uteuzi na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023
Sura hii pia inaainisha utaratibu wa kufuatwa endapo kuna mgombea mmoja tu halali wa nafasi ya ubunge au endapo hakuna mgombea. Kwa mujibu wa Sehemu hii endapo kutakuwa na mgombea mmoja halali wa nafasi ya Ubunge ameteuliwa, mgombea huyo atapaswa kupigiwa kura na atatangazwa kuwa amechaguliwa endapo atapata kura nyingi za ndiyo kati ya kura zote halali zilizopigwa.
Maoni: Hili ni jambo zuri na jema, sasa hakuna tena ushindi wa ubwete wa mtu kupita bila kupingwa!. Hii itaondoa zile figusu za kuzuia watu wasigombee, kuwanunua wapinzani na kuzuia fomu zisirejeshwe na mtu kutangazwa mshindi wa kupita bila kupingwa!. CCM ina wabunge 18 ambao wamepita bila kupingwa!.
Sura ya Tano ya Muswada inahusu masharti ya uchaguzi wa Madiwani. Sura hii imegawanyika katika Sehemu Tatu, ambapo Sehemu ya Kwanza inabainisha masharti ya uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani, muda wakuwa madarakani kwa Madiwani, namna na wakati wa kuitisha uchaguzi mdogo na uwakilishi katika Kata. Sehemu ya Pili inaweka masharti kuhusu sifa za mgombea na mazingira ya mtu kukosa sifa ya kuteuliwa katika uchaguzi. Sehemu ya Tatu inajumuisha masharti kuhusu siku ya uteuzi, uteuzi wa mgombea, dhamana za wagombea, utaratibu wa kuweka pingamizi na utaratibu unaopaswa kufuatwa ikiwa kuna mgombea mmoja tu wa nafasi ya udiwani au ikiwa hakuna mgombea.
Sura ya Sita ya Muswada inaweka masharti kuhusu uchaguzi, utaratibu wakupiga kura na uteuzi wa wabunge na madiwani wanawake viti maalum. Sura hii imegawanyika katika Sehemu Sita, ambapo Sehemu ya Kwanza inaweka masharti mbalimbali kuhusu siku ya uchaguzi na tangazo la uchaguzi. Kwa mujibu wa masharti hayo, taarifa ambazo zitakuwa katika tangazo la uchaguzi ni pamoja na siku na muda wa kuanza na kufunga upigaji kura, anwani ya vituo vya kupigia kura, wapiga kura waliopangwa kwa kila kituo cha kupigia kura na taarifa za wagombea walio teuliwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi. Sehemu ya Pili inaweka masharti kuhusu mgombea kujitoa na utaratibu unaopaswa kufuatwa endapo mgombea atafariki au hakuna mgombea. Sehemu ya Tatu inaweka masharti kuhusu kampeni za uchaguzi na namna kampeni zinavyopaswa kuendeshwa, ikiwa ni pamoja na masharti kuhusu kuwasilisha ratiba ya mikutano kwa msimamizi wa uchaguzi kwa lengo la kuepuka migonganoya mikutano. Sehemu hii inaweka pia masharti kuhusu upatikanaji na wajibu wa vyombo vya habari vya umma na matakwa ya kutokuwa naupendeleo na kuepuka ubaguzi kwa mgombea yeyote katika utoaji wamatangazo.
Maoni: Hapa bado kuna tatizo, mgombea mmoja ana vingora, ana media team yake paid by public funds, ana logistics ya serikali, magari, PA, bajeti na watendakazi, nchi za wenzetu, incumbent president anapongombea tena, anakuwa scrapped off all presidential privileges isipokuwa ulinzi na wale wagombea wengine wote wa urais wanapatiwa ulinzi na basic logistical support kama ni ving'ora, wote ni ving'ora na sio utaratibu wa kawaida wa mgombea mmoja mwenye dola ameshika mpini kugombea kisu cha makali kuwili na wagombea makapuku!, unategemea ushindani wa haki?.
Sehemu ya Nne ya Sura hii inaainisha utaratibu wa uchaguzi unaojumuisha masharti kuhusu siku na muda wa kupiga kura, mawakala wa upigaji kura, masanduku ya kura, muundo wa karatasi za kura na katazo la kuweka wazi kura.
Sehemu ya Tano inaweka masharti kuhusu utaratibu wa kupiga na kuhesabu kura. Masharti hayo yanajumuisha watu wanaostahili kupiga kura, mazingira yanayoweza kumfanya mtu kupotezasifa za kupiga kura, utaratibu wa kupiga kura, watu wanao ruhusiwa kuingia katika kituo cha kupigia kura, mazingira yanayoweza kusababisha kuahirishwa kwa upigaji kura inapotokea vurugu, kufungwa kwa zoezi laupigaji kura na utaratibu wa kuhesabu kura. Kwa mujibu wa masharti ya Sehemu hii, mawakala wa upigaji kura wanatambuliwa kuwa mawakala wa kuhesabu kura. Vilevile Sehemu hii inaainisha wajibu wa msimamiziwa kituo baada ya kuhesabu kura, utaratibu wa kujumuisha kura katika uchaguzi wa wabunge na madiwani na utaratibu wa kutangaza matokeo ya ubunge na udiwani. Sehemu ya Sita ya Sura hii inaweka masharti kuhusu uteuzi wa wabunge na madiwani wanawake viti maalum na unatambua utaratibu ulioainishwa katika Katiba na Sheria za Serikali za Mitaa kuhusu wabunge na madiwani wanawake viti maalum.
Sura ya Saba ya Muswada inaweka masharti kuhusu makosa mbalimbali yanayoweza kutendwa wakati wa uandikishaji, uteuzi wa wagombea na uchaguzi. Miongoni mwa makosa hayo ni pamoja na kutumia wadhifa kushawishi watu wengine kutoomba kuteuliwa, mwenendo usiofaa wawatendaji wa uchaguzi na maafisa waandikishaji, makosa yanayohusu fomu za uteuzi au karatasi za kura, vitendo vya ushawishi na rushwa, kutotunza siri katika uchaguzi kwa watu wanao ruhusiwa kuwa katika kituo cha kupigia kura au kuhesabia kura na kuingilia mikutano halali ya hadhara. Sambamba na kuainisha makosa mbalimbali, Sehemu hii inaweka pia adhabu kwa mtu atakayetenda makosa hayo.
Sura ya Nane ya Muswada inaweka masharti kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi kwa njia ya shauri la uchaguzi. Kwa mujibu wa Sura hii, mashauri ya uchaguzi kupinga matokeo ya ubunge yatasikilizwa katika Mahakama Kuu na mashauri ya uchaguzi kupinga matokeo ya udiwani yatasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi. Miongoni mwa taratibuzilizoainishwa katika Sura hii ambazo mtu aliyefungua shauri atapaswakuzingatia ni utaratibu wa kuweka dhamana ya gharama. Aidha Sehemu hii inaweka pia masharti ya mamlaka ya Jaji Mkuu kutengeneza kanuni zitakazosimamia usikilizwaji wa mashauri ya kupinga matokeo ya uchaguzi. Ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa kanuni hizo, inapendeekzwa kuwa kanuni hizo zitengenezwe kwa kushauriana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Sura ya Tisa ya Muswada inahusu masharti ya jumla ambayo yanajumuisha mamlaka ya Mkurugenzi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi kupata taarifa, malipo ya watendaji wa uchaguzi, mamlaka yaTume ya Taifa ya Uchaguzi kutengeneza kanuni kwa ajili ya utekelezaji bora wa Sheria na matumizi ya teknolojia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Tume.
Sura ya Kumi ya Muswada inaweka masharti kuhusu kufutwa kwa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 1979 na kuweka utaratibu kwa masharti yatakayoendelea kutumika hata baada ya kufutwa kwa Sheria hizo.
Maadam sheria batili hii imeisha somwa kwa mara ya kwanza, nashauri tutoe maoni yetu, pili hoja hizi zizingatiwe
Hivyo Bunge la February lije na mabadiliko madogo ya katiba kwa hati ya dharura, tuondoe kwanza ubatili huu ndani ya katiba yetu na sheria zetu ndipo tusome kwa mara ya pili muswada huu!.
- Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
- Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?
- Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.