Je, wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni batili? Ni mvinyo wa zamani, kwenye chupa mpya? Why ubatili huu?

Mkuu Tate Mkuu , nyinyi mnaomsusia ngedere shamba la mahindi ndio mnao sababisha kila mwaka tunavuna mabua!.
Numbers don't lie! Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

Watu wote wenye umri wa kupiga kura wasipo jiandikisha na kujitokeza kupiga kura, hawa ndio wanao ipa CCM ushindi kwasababu majina yao yataandikishwa na kura zao watapigiwa na zote zitaichagua CCM!.

P
Hiki unachosema nadhani kinaweza kuwa na ukweli kwa 100%. Maana kuna mtu wangu wa karibu alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi wa 2020, aliwahi kuniambia hivi hivi.

Eti baada ya watu kuondoka kituoni, walijifungia na kupiga kura za kuwapa ushindi mgombea wa urais wa kipindi hicho kupitia chama tawala, mbunge wa chama tawala, na pia diwani.

Na alisema kabla ya kupiga hizo kura, mgombea urais wa upinzani na mgombea ubunge wake na yule wa udiwani; ndiyo waliokuwa wakiongoza kwa kura nyingi tu.

NB:- Bado msimamo wangu hautabadilika. Maana inauma kushiriki hayo maigizo yanayoitwa uchaguzi. Mambo yakibadilika walau kama ilivyokuwa 2015 kurudi nyuma, nitashawishika.
 
Nimesema na ninasema tena, numbers don't lie. Uchaguzi wa 2020 tulikuwa milioni 50 eligible voters ni milioni 30 wakaandikisha milioni 29!.

Do you see the game people play?. Eligible voters wote waliandikishwa!, wakapigiwa kura zao na zikahesabiwa!.

Hii iliwezekana kwasababu ya watu kama nyinyi ambao hamjiandikishi na mkijiandikisha hamjitokezi kupiga kura!.

Uchaguzi wa 2025 tutakuwa na eligible voters 40 million!. Kama wote watajitokeza kujiandikisha na wote wakajitokeza kupiga kura, na wakachagua viongozi wanaowataka, there will be no one wa kupigiwa kura and no game to play!.

Kususa kupiga kura ni kumsusia ngedere shamba la mahindi, utayavuna mabua!.
P
Hiyo tu out of 60m kuwa eti 29m waliojiandikisha kupiga kura , ni wendawazimu mwanaume unayesimamisha vizuri kwenda kusomama kwenye mstari wa kura ukisema unachagua viongozi.
 
Nimesema na ninasema tena, numbers don't lie. Uchaguzi wa 2020 tulikuwa milioni 50 eligible voters ni milioni 30 wakaandikisha milioni 29!.

Do you see the game people play?. Eligible voters wote waliandikishwa!, wakapigiwa kura zao na zikahesabiwa!.

Hii iliwezekana kwasababu ya watu kama nyinyi ambao hamjiandikishi na mkijiandikisha hamjitokezi kupiga kura!.

Uchaguzi wa 2025 tutakuwa na eligible voters 40 million!. Kama wote watajitokeza kujiandikisha na wote wakajitokeza kupiga kura, na wakachagua viongozi wanaowataka, there will be no one wa kupigiwa kura and no game to play!.

Kususa kupiga kura ni kumsusia ngedere shamba la mahindi, utayavuna mabua!.
P
Uwe na wananchi 60m kisha wapiga kura wawe 40m, yaani watu wenye 18+ wawe wengi kuliko waliochini kisha useme kuna uchaguzi?!
 
Mungu ataingilia kati kama Kwa yule.....
No, kuna baadhi ya mambo ya Kaisari Mungu humwachia Kaisari mwenyewe!, dhulma hii imekuwepo toka 1992, hivyo Mwinyi kaitumia Mungu hakuingilia, Mkapa kaitumia, Mungu hakuingilia, JK kaitumia, Mungu hakuingiliwa, JPM kaitumia, Mungu hakuingilia na hata Samia akiitumia, Mungu hataingilia, ila Samia akiiondoa dhulma hii, atabarikiwa sana!. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
P
 
Hiki unachosema nadhani kinaweza kuwa na ukweli kwa 100%. Maana kuna mtu wangu wa karibu alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi wa 2020, aliwahi kuniambia hivi hivi.

Eti baada ya watu kuondoka kituoni, walijifungia na kupiga kura za kuwapa ushindi mgombea wa urais wa kipindi hicho kupitia chama tawala, mbunge wa chama tawala, na pia diwani.

Na alisema kabla ya kupiga hizo kura, mgombea urais wa upinzani na mgombea ubunge wake na yule wa udiwani; ndiyo waliokuwa wakiongoza kwa kura nyingi tu.

NB:- Bado msimamo wangu hautabadilika. Maana inauma kushiriki hayo maigizo yanayoitwa uchaguzi. Mambo yakibadilika walau kama ilivyokuwa 2015 kurudi nyuma, nitashawishika.
Huo ni uongo, kura zenu nyinyi msiojiandikisha na msiopiga kura zilipigwa usiku kucha kabla ya uchaguzi, kesho yake ilikuwa ni kazi ya kuziunganisha tuu ili kuzijazilizia tuu kwenye balot boxes !. Kura zote zinahesabiwa hapo kituoni baada ya kupiga kura na matokeo yanabandikwa kituoni usiku huo huo hivyo hiyo ya kupiga kura baada ya uchaguzi ni uongo!. Kama eligible voters mngejiandikisha na wote mkajitokeza, then hizo mlizopigiwa zisinge pigika!. The game is played kwenye daftari la kupiga kura.
P
 
Wanabodi,

Kama kawa, leo nimepata fursa kuwaletea makala elimishi ya uchambuzi wangu wa muswada huu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, kwa swali Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Je muswada huu ni mvinyo ule ule wa zamani, kwenye chupa mpya?. Muswada huu una nini kipya?, nini kilichobadilika tofauti na zamani?. Huu ni ubatili mtupu, ila ndani ya ubatili huu pia kuna baadhi ya mambo ni mambo mazuri!

Naomba nianze bandiko hili kwa utambulisho
Mwandishi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea na Wakili wa kujitegemea, ambaye japo ni mhitimu wa LL.B (Hons) ya UDSM, yeye sio wakili msomi, kwasababu haendi mahakamani, huyu ni wakili mtangazaji na muelimishaji umma kuhusu katiba, sheria na haki, kupitia makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" zinazotoka humu JF, baadhi ya magazeti na kipindi cha TV na oline
View: https://youtu.be/b67jqx0GWd8?si=ucNR1r5_kd7rZShI

Nimeanza na utambulisho huo, kwasababu kitendo cha wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, wa serikali wametunga muswada, wamejiridhisha uko ok ndio maana wakauwasilisha Bungeni, ambako nako kuna mabingwa wa sheria, wabobezi na wabobevu nao wakaoona uko sawa na ndio maana wakaruhusu uwasilishwe Bungeni na umeisha somwa kwa mara ya kwanza, halafu akaibuka mtu tuu kuukosoa kwa kuwaambia watu muswada huu ni batili!, lazima watu watajiuliza huyu ni nani?, hivyo huu ni uthibitisho kuwa Tanzania tuna wanasheria wa ajabu sana!. Jambo limeishatamkwa na Mahakama Kuu kuwa ni batili, serikali yetu sikivu inawezaje tena kutuletea ubatili huo huo kwenye hii sheria mpya?!. Hii sio mara ya kwanza kwa serikali yetu kututungia sheria batili, na niliwahi kuuliza Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?, hivyo zinapokea fursa za kubadili sheria, tuzibe kwanza paa letu, tuzibe matobo ili tuwe salama.

Jee inakuwaje madudu haya yakafanywa na wanasheria wetu?. Jibu ni moja tuu, sheria ni fani bahari, eneo ngumu kuliko yote kwenye sheria ni eneo la kutafsiri sheria, kwa Tanzania mamlaka pekee ya kutafsiri sheria ni Mahakama Kuu ya Tanzania, ila naomba kusema wazi hata Mahakama zetu zimekosea kutafsiri baadhi ya sheria zinazokwenda kinyume cha katiba. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?

Ubatili wa muswada huu, sio ubatili mwingine wowote, zaidi ya ubatili ule ule ninaoupigia kelele humu jukwaani kila uchao, wa serikali yetu kutunga muswada wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Bunge letu Tukufu kuupokea huo muswada batili na ubatili wake na waheshimiwa wabunge wetu kujadili kutunga sheria batili kama mazuzu!
Ubatili huu nimeuzungumza hapa

Kwa vile Mkuu wa nchi ni rais wa nchi, hivyo likitokea tatizo lolote, analaumiwa mkuu wa nchi, na madudu yote hayo yalitokea kabla Rais Samia hajaingia madarakani, hivyo nimemjengea indemnity Rais Samia asilaumiwe kwa madudu haya Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.

Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii iyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.

Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.

Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu

Kwenye mada hii pia ninaainisha kwa mukhtaasari, sura zote 10 za sheria hii, ili kuwaelimisha elimu ya uraia, sheria na haki ili tuitumie kikamilifu hii miezi 3 ya kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ya sheria hii.

Muswada huu unatunga Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka, 2023. Kwa ujumla, Sheria hii inaunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292. Hivyo sasa masharti ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani ni sheria moja na kutekelezwa na mamlaka moja ambayo ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hapa ninapendekeza chaguzi zote nchini, uchaguzi wa Rais na Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa, ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume moja Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hili ni jambo jema!.

Muswada huu umegawanyika katika Sura Kumi.
Uchambuzi wangu wa sura kwa sura na maoni yangu
Karibu

Hitimisho
Maadam sheria batili hii imeisha somwa kwa mara ya kwanza, nashauri tutoe maoni yetu, pili hoja hizi zizingatiwe

Hivyo Bunge la February lije na mabadiliko madogo ya katiba kwa hati ya dharura, tuondoe kwanza ubatili huu ndani ya katiba yetu na sheria zetu ndipo tusome kwa mara ya pili muswada huu!.

Hayamambo ya serikali yetu kututungia ubatili, na kulipelekea Bunge letu likaubariki ubatili huu kuwa sheria, tutaendelea nayo hadi
lini? Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
na nikasema Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Hivyo mambo haya yakiendelea, kiukweli kabisa we'll be left with no option but to do something! (ambacho naomba nisikitaje)!.

Mungu ibariki Tanzania

Paskali

Mkuu Pascali
Imenichukua nusu kutwa ya leo kusoma na kuchakata hoja hii uliyotuwekea hapa.

Kimsingi nakubaliana nawe kwenye huu ukweli kwamba muswada wa sheria hii ya uchaguzi una kasoro laanifu zinazohitajj kutakaswa kwa kubatilishwa ili zirejewe na kubadilishwa ziendane na maudhui mazima ya hitaji la demokrasia nchini.

Katika issue ya mgombea kudhaminiwa na Chama ninaona siyo sawa.

Je unaonaje mimi na wewe na yeyote yule tukiungana kwenda huko mahakamani kuzuia ama kupinga kupitishwa kwa muswada huu kuwa sheria.

Je Katiba inatulinda kiasi gani kwenye kutetea demokrasia?
 
Mkuu Msanii, kwanza naunga mkono hoja, kwenda Mahakamani, ila sio kupinga kupitishwa kwa muswada huu kuwa sheria, bali kuiomba Mahakama Kuu kutoa tafsiri ya ubatili wa muswada huu. Mfumo wetu wa mihimili kutoingiliana, Mahakama haiwezi kuliingilia Bunge kwenye utungaji sheria, hivyo kwa vile muswada huu bado sio sheria, ni muswada tuu, huwezi kufungua shauri kuushitaki muswada ila ukiisha pitishwa na Bunge kuwa sheria, unaweza kufungua shauri kuupinga sheria hiyo.

Mfumo wetu wa haki hauko vizuri kabisa!, katiba yetu ina matobo kibao!, ni serikali tuu ndio pekee inaweza kushitakiwa Mahakamani isipo tenda haki, lakini Bunge na Mahakama zisipo tenda haki, haziwezi kushitakiwa popote! Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?

P
 
Ubatili wa muswada huu, sio ubatili mwingine wowote, zaidi ya ubatili ule ule ninaoupigia kelele humu jukwaani kila uchao, wa serikali yetu kutunga muswada wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Bunge letu Tukufu kuupokea huo muswada batili na ubatili wake na waheshimiwa wabunge wetu kujadili kutunga sheria batili kama mazuzu!
Paskali
Hapa nauliza tuu swali, Je inawezekana baadhi ya Wabunge wetu wa Bunge la JMT ni mazuzu?, wanajadilije muswada wa sheria ya uchaguzi wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT bila kujijua kuwa kuna ubatili?, huu sio uzuzu?. Nauliza tuu!.
P
 
Wanabodi,

Kama kawa, leo nimepata fursa kuwaletea makala elimishi ya uchambuzi wangu wa muswada huu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, kwa swali Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Je muswada huu ni mvinyo ule ule wa zamani, kwenye chupa mpya?. Muswada huu una nini kipya?, nini kilichobadilika tofauti na zamani?. Huu ni ubatili mtupu, ila ndani ya ubatili huu pia kuna baadhi ya mambo ni mambo mazuri!

Naomba nianze bandiko hili kwa utambulisho
Mwandishi ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea na Wakili wa kujitegemea, ambaye japo ni mhitimu wa LL.B (Hons) ya UDSM, yeye sio wakili msomi, kwasababu haendi mahakamani, huyu ni wakili mtangazaji na muelimishaji umma kuhusu katiba, sheria na haki, kupitia makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" zinazotoka humu JF, baadhi ya magazeti na kipindi cha TV na oline
View: https://youtu.be/b67jqx0GWd8?si=ucNR1r5_kd7rZShI

Nimeanza na utambulisho huo, kwasababu kitendo cha wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, wa serikali wametunga muswada, wamejiridhisha uko ok ndio maana wakauwasilisha Bungeni, ambako nako kuna mabingwa wa sheria, wabobezi na wabobevu nao wakaoona uko sawa na ndio maana wakaruhusu uwasilishwe Bungeni na umeisha somwa kwa mara ya kwanza, halafu akaibuka mtu tuu kuukosoa kwa kuwaambia watu muswada huu ni batili!, lazima watu watajiuliza huyu ni nani?, hivyo huu ni uthibitisho kuwa Tanzania tuna wanasheria wa ajabu sana!. Jambo limeishatamkwa na Mahakama Kuu kuwa ni batili, serikali yetu sikivu inawezaje tena kutuletea ubatili huo huo kwenye hii sheria mpya?!. Hii sio mara ya kwanza kwa serikali yetu kututungia sheria batili, na niliwahi kuuliza Katiba Yetu Ina Matobo: Serikali Ikikosea, Inashitakika. Je, Bunge na Mahakama Zinapowakosea Watanzania Kama Makosa Haya Tunawashitaki Wapi?, hivyo zinapokea fursa za kubadili sheria, tuzibe kwanza paa letu, tuzibe matobo ili tuwe salama.

Jee inakuwaje madudu haya yakafanywa na wanasheria wetu?. Jibu ni moja tuu, sheria ni fani bahari, eneo ngumu kuliko yote kwenye sheria ni eneo la kutafsiri sheria, kwa Tanzania mamlaka pekee ya kutafsiri sheria ni Mahakama Kuu ya Tanzania, ila naomba kusema wazi hata Mahakama zetu zimekosea kutafsiri baadhi ya sheria zinazokwenda kinyume cha katiba. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?

Ubatili wa muswada huu, sio ubatili mwingine wowote, zaidi ya ubatili ule ule ninaoupigia kelele humu jukwaani kila uchao, wa serikali yetu kutunga muswada wenye vipengele batili vinavyokwenda kinyume cha katiba ya JMT na Bunge letu Tukufu kuupokea huo muswada batili na ubatili wake na waheshimiwa wabunge wetu kujadili kutunga sheria batili kama mazuzu!
Ubatili huu nimeuzungumza hapa

Kwa vile Mkuu wa nchi ni rais wa nchi, hivyo likitokea tatizo lolote, analaumiwa mkuu wa nchi, na madudu yote hayo yalitokea kabla Rais Samia hajaingia madarakani, hivyo nimemjengea indemnity Rais Samia asilaumiwe kwa madudu haya Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.

Kwa maoni yangu, dhulma kuu ya kwanza na ya msingi ni haki ya kupiga kura na haki ya kupigiwa kura, haki hii iyotolewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, ikaja kuporwa kwa sheria batili ya uchaguzi, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ya Mwaka 1979.

Mchungaji Mtikila akapinga sheria hiyo mahakani, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kukibatilisha kifungu hicho batili, kwa kwenda kinyume cha katiba, serikali yetu ikafanya jambo moja kubwa la ajabu sana, au kitu cha ajabu sana!, ikapeleka bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, ikakichomekea kipengele batili ndani ya katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo ubatili huo ukachomekewa ndani ya katiba!. Kwanini tutunge sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule?. Kwanini tutunge sheria mpya yenye dhulma ile ile ya haki kwa Watanzania?!.

Rais Samia baada ya kuingia madarakani, tumemlilia sana kuhusu ubatili huu

Kwenye mada hii pia ninaainisha kwa mukhtaasari, sura zote 10 za sheria hii, ili kuwaelimisha elimu ya uraia, sheria na haki ili tuitumie kikamilifu hii miezi 3 ya kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ya sheria hii.

Muswada huu unatunga Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka, 2023. Kwa ujumla, Sheria hii inaunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292. Hivyo sasa masharti ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na Madiwani ni sheria moja na kutekelezwa na mamlaka moja ambayo ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hapa ninapendekeza chaguzi zote nchini, uchaguzi wa Rais na Wabunge, Madiwani na Serikali za Mitaa, ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume moja Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Hili ni jambo jema!.

Muswada huu umegawanyika katika Sura Kumi.
Uchambuzi wangu wa sura kwa sura na maoni yangu
Karibu

Hitimisho
Maadam sheria batili hii imeisha somwa kwa mara ya kwanza, nashauri tutoe maoni yetu, pili hoja hizi zizingatiwe

Hivyo Bunge la February lije na mabadiliko madogo ya katiba kwa hati ya dharura, tuondoe kwanza ubatili huu ndani ya katiba yetu na sheria zetu ndipo tusome kwa mara ya pili muswada huu!.

Hayamambo ya serikali yetu kututungia ubatili, na kulipelekea Bunge letu likaubariki ubatili huu kuwa sheria, tutaendelea nayo hadi
lini? Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?
na nikasema Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Hivyo mambo haya yakiendelea, kiukweli kabisa we'll be left with no option but to do something! (ambacho naomba nisikitaje)!.

Mungu ibariki Tanzania

Paskali

Mkuu, huko juu zaidi ni wapi?
 
Nalipeleka jambo lako kule juu zaidi, top of the top ambako huko lazima haki ipatikane!.
P
Acha tu nicheke kwa sababu, duh!

Nimeupenda uchambuzi wako, na inaonesha uko vizuri sana kwenye uelewa wa Katiba.

Jambo moja ambalo huwa unaniudhi sana ni wewe kujifanya huelewi kuwa Zanzibar ni nchi na huku Katiba ya Zanzibar imeliweka hilo peupe kabisa kuwa Zanzibar ni nchi na Taifa.
 
Back
Top Bottom