Je umaarufu wa Mzee Lowassa umeporomoka au umeongezeka??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,116
Baada ya mkutano mkuu wa chama cha ccm kumalizika hapo jana kuna maneno mengi yameibuka ya kuwasema Lowassa na Sumaye. Kwa leo nitamwongelea Lowassa tu.

Je mzee Lowassa angebaki ccm baada ya kukatwa angekuwa maarufu kisiasa kama sasa au angeporomoka?
Je kwa sasa ni maarufu kisiasa kuliko hata kabla hajakatwa au kipindi kile alikua maarufu kuliko sasa??
Haya ni baadhi ya maswali unayopaswa kujiuliza kabla ya kumsema mzee lowassa kwa uzuri au kwa ubaya. Mm nina haya ya kumsema Lowassa.
Kwanza naanza kwa kusema Lowassa ndiye mwanasiasa maarufu kuliko yeyote hapa TZ kwa sasa. Na umaarufu umeongezeka baada ya kuhama kutoka ccm na kujiunga na ukawa. Sababu za ni nyingi lakn kubwa ni kuwaunganisha maadui zake wa awali na kuwafanya marafiki. Hata kule alikohama ameacha marafiki. Waliomkataa ni viongozi wa juu lakn wanachama bado wanamkubali lejea baada ya kukatwa ukumbi mzima zilisikika nyimbo za kumkubali. Hata kwenye kampeni tumemsikia JPM akilalamika kuhujumiwa na wenzao na kudiliki kuwasema hadharan kwamba usiku wako ukawa mchana ccm.

Ukitaka kuhakiki nisemayo ombea utawala huu uruhusu usawa katika ulingo wa siasa utakubali bado ni kipenzi cha wengi na bado watanzania hawajapata kile wanachohitaji hivyo bado wanamtafuta mtu wa kuwatatulia shida zao zilizo letwa na ccm kwa zaid ya miaka 50. JPM bado hana umaarufu kisiasa kumzid Lowasa na ndio maana serikali inafanya kila mbinu kuhakikisha upinzani haupati uwanja mpana wa kujieleza. maana kukiwa na ulingo huru wa siasa serikali itaumbuka na kujiondelea sifa inazojinadi kwamba inakubalika.maana nina uhakika 100% viongozi wanafaham upinzani unakubalika na watu wengi na ndio maana wanawaminya maana watapelekea kushuka kwa hadhi ya serikali. Pale mikutano ya upinzani itakapo jaa watu wengi na mikutano ya kiccm au kiserikali kukosa watu.

Mkutano wote wa jana ulitawaliwa na yeye Lowasa. Kwann wasimjadili mwingine? Hakuna mjumbe au mwalikwa ambaye alipewa wasaa wa kuongea alikosa kumsema lowassa. Kila mtu alimsema. Nikimnukuu mwalimu mmoja wa dini aliwahi kusema yamtokayo mwanadamu ndio yaliomjaa kichwani. Hivyo bado lowassa kawajaa kichwani. Wapinzani wengine wamehamisha vita yao sasa adui yao mkubwa ni ukawa.badala ya Ccm. Hiyo ni dalili ya nguvu iliopo upinzani baada ya Lowassa kuhamia huko imekua kubwa hadi kupelekea vyama vingine kupotea kabisa. Namnukuu cheyo anaombea ccm isipasuke tena maana kupasuka kwao mwaka jana kumewaathiri hata wao. akasema ccm ni kama mti mkubwa ukipasuka unaumiza viumbe wangine waliochini yake.

Nimalizie kwa kusema angebaki ccm baada ya kukatwa asingekua na umaarufu wowote maana asingekua na nafasi ya kusema chochote. Asingekua na ulingo mpana wa kuongea chochote, angebaki bubu. Maana tumeshuhudia makada kadhaa wakikosoa chochote, wana ccm huwasema wanamhujumu raisi wa sasa.ushahidi uko kwa Membe alipojaribu kukosoa tu lundo la maneno lilimwendea. Pia tujiulize ni nani aliyebaki ccm baada ya kushindwa katka uchaguzi ambaye amekua maarufu kuliko Lowassa au umaarufu wake umeongezeka kuliko wa awali.binafsi sijamwona.

Hivyo nampongeza mzee Lowassa na namtia moyo aendelee na mipango yake. Kuhama kutoka ccm kwa mtu kama yeye yataka mtu mwenye moyo sana. Maana serikali hii ukiwa ccm wewe ni msafi. Lakn ukihama tu ww ni fisadi. Ukiwa ccm mali zote unazomiliki ni halali ardhi yote unayomiliki ni halali ila ukihama tu sio halali.

Je wewe binafsi unamsemaje Lowassa.
 
Yaaa the Man is at work!!! he made the etra -ordinary meeting to end in his own power as every person touched him in anyway around!!! Not only him but Mzee Sumaye as well!!!these TWO are GIANTS IN TZ POLITICS! asikwambie mtu coz wanapeana matumaini lakini miyoni mwao wanatafakari kwa kini ni namna gani wawazime kabisaaa wasisikike...MUNGU akimnyanyua mtu kwa mkono wake hakuna kiumbe chochote kitachoushusha chini!!! kama wameinuliwa wataendelea kuonekana kwa watanzania tu hata iweje!! enzi ikifika imefika haizuiliwi kwa mkono wa dola wala maneno BALI Mungu anafanya pasipo njia na kuwa na njia!!
 
kwa jana tuu imethiirisha mkutano wa ccm kuwa lowasa yupo ndani ya vichwa vyao kwa asilimia nyingi wakilala wakishinda wanamuwaza na ndio maana wanazuia mikutano yake maana akianza huo umati na serikali haitaki kuabika live
 
Tukizingatia jinsi alivyotawala vikao vya ccm mwanzo mwisho, kwa wiki nzima na headlines za magazeti, ni dhahiri Lowassa ndie mwanasiasa mwenye "mguso" mkubwa sana kwa sasa hapa Tanzania baada ya JPM, nafikiri umaarufu wake umedumu na kuhimili vishindo vyote. (Nachelea kusema umeongezeka pasipo kuwa na takwimu za kitafiti!)
 
Kama kila anayesimama kwenye mkutano mkuu Wa chama Fulani anamuongelea au kumfanyia reference mtu Hugo Huyo, na kila mmoja anahisi bila ya kumtaja huyo hotuba yake au uanachama wake utakua hujakamilika, unadhani mtu huyo anayetajwa anakua na nguvu au dhaifu?
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Lowasa n mwanasiasa wa karne
Ameanza kujijenge zaidi ya muaka 20
Hivo ccm wasitegemee kuwa edo atapoteza umaarufu
Ukizingatia watanzania walimpa kura za kutosha
Amebaki kwenye vichwa na mioyo ya watu wengi
Viva lowasa
 

Unaweza uka fikiria kuwa umaarufu wake unapungua, ila ukifikiria jinsi Mkutano mkuu wa CCM walivyomshambulia hapo ndipo nafsi inapingana na mafikirio
 
  • Thanks
Reactions: MTK
LOWASA YUPO JUU SANA HUWEZI KUA MWANASIASA BILA KUMTAJA NGOYAE HUYU JAMAA BALAA KWA SIASA ZA TANZANIA. YAANI AKIPEWA NAFASI KIDOGO KUONGEA CCM WANATETEMEKA.
 
Umaarufu wa Edo unazidi kuongezeka kila jua linapochomoza, hata maadui zake wanalijua hili vizuri sana......mpk kushindwa kujizuia kwenye mkutano mkuu kama vile na kuanza kulipopoa mawe jina LA mheshimiwa ni wazi wakiwa mwenyewe kwenye corido zao huko Lumumba hali ni zaidi.......Lowasa ni MTU wa watu na kwangu Mimi yeye ndio mwanasiasa bora zaidi katika kipindi hichi.
 
Back
Top Bottom