Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Status
Not open for further replies.
NI kweli awa jamaa wa zeutamu hawatufai katika jamii ya maadili ya jamii yetu, ni kweli kwamba watu wengi wamechafuliwa na mambo aya yapo katika jamii yetu ila hayajafikia kiasi icho wao zeutamu wanachokiamini! Kwa maoni tu mie ningependa web hii ifungwe na wote wanaohusika nayo wafikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa uchafuzi wa jamii
 
Swala la maadili ni swala la nafsi ya mtu. Kuna siku jamaa alisema, "Siku hizi muda wa vipindi vya Dini mashuleni ni muda wa michezo". Nilitafakari sana hilo jambo, sasa naona maana yake. Watu wamekuwa hawamuogopi Mungu ndio chanzo cha haya yote.

Ze utamu ni sawa na porn site zingine, watu mmeenda huko kutafuta nini? Kama watu wanasema wamezipata hizo picha kwenye mail hapo naweza kuwaelewa. Nadhani alichofanya huyu jamaa ni "broadcasting" kwa hiyo lawama zote ni vyema zingeenda kwa aliyeitengeneza hiyo picha.

Watanzania tuamke, hii ni ishara ya kwamba watu wanamuda mwingi wa kufanya kazi lakini kazi hamna. Kuna jamaa mmoja alisema, "In Tanzania Human is not a resource". Watu mpo tuu kazi kufuatilia umbea.

Naomba kuwasilisha kwenye jamvi wakuu.
 
nimeiona hiyo picha ni mbaya na ni chafu,hajamdhalilisha mh.Rais tu bali watanzania wote walio wastaarabu na wanaojiheshimu,NAMLAANI huyo aliyetengeneza hiyo picha,imeniumiza na imeniogopesha ,amewezaje kuthubutu kufanya jambo la aina hiyo,Watanzania wenzangu tunaenda wapi?hii new technology mbona tunamisuse namna hii?huu uhuru na mani tuliyonayo mbona tunaipaka matope tena kwa bila huruma wala haya tena bila kumuogopa Mungu,jamani hata vitabu vya Mungu imeandikwa HESHIMUNI MAMLAKA MLIYOPEWA NA MUNGU,kweli leo hii imefikia kutengeneza picha ya kumchafua Rais wa nchi ,?

Wewe uliyetengeneza picha hiyo JK amekukosea nini kikubwa hata ufikie hatu uliyofikia?imagine ingekuwa wewe ungejisikiaje?Tanzania nchi inayosifika kote ulimwenguni kwa amani na utulivu,eti watanzania ni wakarimu na wana upendo,kweli?

Nimeumia roho kupita kiasi,huu uhuru tulionao sasa tunautumia vibaya.Huyu aliyetoa picha hiyo ALAANIWE YEYE NA KIZAZI CHAKE!!!!!!!!!NA UKOO WAKE WOTE NA WALA ASIPATE BARAKA ZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKE YOTE!!!!!!!!!!
 
Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchngu, watu kibao wamechafuliwa kule. Ila siku itakapokuwa zamu yako ama ya ndugu wako wa karibu ndio utajua kuwa ile web haifai.
Give me a break.
We are talking about THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA for christ sake.
Huyu si mtu tu ,hata kama anamapungufu.

RAIS NI TAASISI.

UKIMTUKANA RAIS,UMELITUKANA TAIFA.

Huyu si kama Insia,Mengi au wengineo unawajua wewe.

TUNALAANI.
 
Picha zimetumwa kwenye e-,ail tangu jana na watu walioona tumezikuta asubuhi kwenye email address zetu

Imekuwaje ze utamu akakutumia email? Kama si ze utamu aliyetuma basi kuna tatizo pia kwa wale wanaotoa picha kwenye globu ya ze utamu na kuanza kuzisambaza. Mwambie huyo aliyekutumia picha hiyo/hizo kwamba si halali kufanya hivyo na pia ni kinyume na maadili ya kitanzania!
 
nimeiona hiyo picha ni mbaya na ni chafu,hajamdhalilisha mh.Rais tu bali watanzania wote walio wastaarabu na wanaojiheshimu,NAMLAANI huyo aliyetengeneza hiyo picha,imeniumiza na imeniogopesha ,amewezaje kuthubutu kufanya jambo la aina hiyo,Watanzania wenzangu tunaenda wapi?hii new technology mbona tunamisuse namna hii?huu uhuru na mani tuliyonayo mbona tunaipaka matope tena kwa bila huruma wala haya tena bila kumuogopa Mungu,jamani hata vitabu vya Mungu imeandikwa HESHIMUNI MAMLAKA MLIYOPEWA NA MUNGU,kweli leo hii imefikia kutengeneza picha ya kumchafua Rais wa nchi ,???????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wewe uliyetengeneza picha hiyo JK amekukosea nini kikubwa hata ufikie hatu uliyofikia?imagine ingekuwa wewe ungejisikiaje?Tanzania nchi inayosifika kote ulimwenguni kwa amani na utulivu,eti watanzania ni wakarimu na wana upendo,kweli????????????????nimeumia roho kupita kiasi,huu uhuru tulionao sasa tunautumia vibaya.Huyu aliyetoa picha hiyo ALAANIWE YEYE NA KIZAZI CHAKE!!!!!!!!!NA UKOO WAKE WOTE NA WALA ASIPATE BARAKA ZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKE YOTE!!!!!!!!!!


Acha ukute huyo aliyeweka ni ndugu yako na wewe utalaaniwa.kama kulaaaniwa Alaaniwe yeye aliyeweka na wala sio mtu mwingine.Kweli utandawazi unatupeleka pabaya.SIJUI JK ATAKUWA AMESHAIONA AU ATAKUWA AMEAMBIWA.ILA UTASHANGAA NAE NI MPENZI MKUBWA WA HIYO BLOG,watu wanaichukia wakishatolewa huko.
 
Give me a break.
We are talking about THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA for christ sake.
Huyu si mtu tu ,hata kama anamapungufu.

RAIS NI TAASISI.

UKIMTUKANA RAIS,UMELITUKANA TAIFA.

Huyu si kama Insia,Mengi au wengineo unawajua wewe.

TUNALAANI.

Please! Kwa watu wengine wanauchafuliwa sio binadamu? Hawana familia? hawana baba na mama? Kushabikia ujinga ndo matokeo yake haya! Eti chombo cha kurekebisha tabia! Aya sasa!
 
Ni kweli nami nimeona hii picha si nzuri kwa raisi wa nchi kama binadamu mwingine. Watu wengi wamewekwa mle bila wao kujua lakini hakuna lililosemwa! SASA AMEWEKWA MKULU WATU WANAPIGA KELELE. Lazima kuwa na maadili kwa watu wote situ eti kwakuwa huyu ni kiongozi na huyu ni mtu wa kawaida.
 
nimeshasema hili na kuandika kwenye Cheche na hata Tanzania daima; huwezi kuwa na standards tofauti ndio maana watu wanapush the envelope. Ile habari ya kusagana iliyoandikwa kwenye Ijumaa endapo ingekuwa na kichwa cha habari "Waziri x afumwa Geto akisagana au Akiliwa uroda" na ikawa describe vile nadhani serikali ingechukua hatua.

Kuna mtu haelewi maana ya uhuru wa maoni.
Sikiliza Mwanakijiji

Nakubaliana na wewe kimsingi,lakini imefika wakati sasa watawala waamke na kufanya sehemu yao.

WATUNGA SERA NA SHERIA ,THEY SHOULD DO THE SAME.

SHERIA ZIENDE NA WAKATI,tusibaki kutumia sheria za 1970s au 1980s kwa kipindi hiki cha 2000s,

Swali: Je huyu mtu akipatikana atashitakiwa kwa sheria ipi? NA KUWA CONVICTED.

Ni kawaida kwa jamii nyingi, mpaka pale jambo kubwa linapotokea ,then mabadiliko hufuata.Jambo kubwa limetutokea leo sisi kama taifa.

Tunashauri,hili lifanyiwe kazi.Na vyombo vyote husika.

LEO NCHI IMEAMKA ASUBUHI, NA KUKUTANA NA MOJA YA AIBU KUBWA KUWEZA KUTUTOKEA KATIKA HISTORIA YETU KAMA TAIFA.
 
Acha ukute huyo aliyeweka ni ndugu yako na wewe utalaaniwa.kama kulaaaniwa Alaaniwe yeye aliyeweka na wala sio mtu mwingine.Kweli utandawazi unatupeleka pabaya.SIJUI JK ATAKUWA AMESHAIONA AU ATAKUWA AMEAMBIWA.ILA UTASHANGAA NAE NI MPENZI MKUBWA WA HIYO BLOG,watu wanaichukia wakishatolewa huko.

kisale,unasema JK ni mpenzi mkubwa wa hiyo blog,mimi naona weye mwenzetu si bure umekunywa maji ya choo
 
Please! Kwa watu wengine wanauchafuliwa sio binadamu? Hawana familia? hawana baba na mama? Kushabikia ujinga ndo matokeo yake haya! Eti chombo cha kurekebisha tabia! Aya sasa!
Where is your patriotism my brother.

Let us not argue for the sake of kubishana tu.

Tulia CHUKUA MUDA kulitafakari hili.
 
All ya grow up, mbona masela kibao tu wanatolewa kule tokea kajamba nani mpaka mawaziri wa serikali, so itakuwa president? Ile ni site ya kikubwa anayeona inamzingua aache kuitembelea.

Ni mtazamo tu.
 
imekuwaje ze utamu akakutumia email? Kama si ze utamu aliyetuma basi kuna tatizo pia kwa wale wanaotoa picha kwenye globu ya ze utamu na kuanza kuzisambaza. Mwambie huyo aliyekutumia picha hiyo/hizo kwamba si halali kufanya hivyo na pia ni kinyume na maadili ya kitanzania!
asante mkulu.
 
All ya grow up, mbona masela kibao tu wanatolewa kule tokea kajamba nani mpaka mawaziri wa serikali, so itakuwa president? Ile ni site ya kikubwa anayeona inamzingua aache kuitembelea.

Ni mtazamo tu.
Avatar yako inajieleza wewe ni mtu wa namna gani.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
heshima mbele!tusiige utamaduni ambao hatukuwa nao hapo mwanzo.Inasikitisha kuona hii blog ya ze utamu inaendeleza libeneke la kuchafua watu sasa mpaka wamefikia hatua ya kumchafua Rais wa nchi!!!!!najiuliza maswali mengi ni kwamba hakuna wa kuzuia hili ?hakuna sheria yoyote ya nchi inayokataza uchafuzi unaofanywa na media!!!???Nampa pole mh.Rais pamoja na familia yake,lakini ni wakati muafaka sasa serikali kufatilia hili jambo na kufika muafaka!!

mkuu sheria zipo ila wafuatiliaji ndio hamna na watu wanasubiri iundwe tume ya kumtafuta zeutamu hakuna anaye jua majukumu yake mpaka kufuatana nyumanyuma. kwa hali hii tuna kazi haswa!
 
Usalama wa Taifa bwwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiii, usingizi. Leo tuwaamshe kwa kupeleka habari Dar Leo na Alasiri na kichwa cha habari "Rais Kikwete achafulia katika mtandao wa Ze utamu" ili waende kuchungulia huko na kuanza kumsaka mmiliki.
 
Waheshimiwa,

Hii thread zaidi sana ina promote hiyo site na watu wengi zaidi ambao walikuwa hawajaiona hiyo picha wanashawishika kuifuatilia ili waione. Wenzetu walioendelea hawazungumzii kabisa vitu kama hivyo, yako masaiti mengi tu ya ajabu ajabu huko kwenye mtandao. Why visit a site whose content is all negative?? Kumbuka njia ya kummaliza mtu na biashara yake ni kukaa kimya na siyo kushabikia eti saiti fulani ina hiki ina kile. Hiyo site inaendelea kukua maana inapata wateja (visitors) na wenye biashara zao wataweka matangazo pale maana wanajua chances za kuonekana ni kubwa. Say NO to this site by not visiting it and even if you receive a dirty picture by email/sms why forward it or talk about it instead of just deleting it and control your spam settings?

Kwa kiasi kikubwa namlaumu mwanzishaji wa thread hii maana ameamsha awareness ya wana JF wengi kwa site hii. Wengi wameenda kuiangalia picha baada ya kuisoma thread hii, kweli wongo? Isn't that a marketing strategy? Hii site iko huko kwenye cyber space na most likely haijawa registered in Tz, so hakuna sheria ya Tz ya kufanya lolote hapa. Kama ameiregister kwenye nchi liberal isiyokuwa na matatizo na mambo hayo je? Kwani hamjafika nchi kama Holland ambako hivyo mnavyoita vitu vya ajabu vinafanyika mitaani legally? Mkimfungia si ataenda kuiregister huko tu? Kama kweli tuna nia ya dhati ya kuipinga, na tusiitembelee - nukta. Hata mtu akiizungumzia mwabie shutup.

Unajua sisi wenye magazeti hapa Tz, kiongozi fulani akituudhi tunafanya nini - tunagoma kuandika chochote au kutangaza chochote juu yake wala kutaja jina lake kwenye vyombo vyetu vya habari. Doesn't this strategy work? Hali kadhalika mafisadi tukishawatambua tunasusia bidhaa na huduma zao wanazotoa kwenye biashara zao! subutu! wabongo hawana hizo. Wao ndio kwaaaaanza wanajitokeza kwa maelfu kusupport. Sasa unategemea nini in that case?

mimi nasita kuichukulia hii kama ni class struggle, ya kwamba eti raisi ana privacy ya tofauti na binadamu MTz mwingine yeyote. Kelele zoooote hizi ni kwa sababu raisi anafanyiwa shughuli? Hiyo site ina nyingi kweli ya watoto wa masikini waliochorwa kama ambavyo hii inadaiwa. Hakuna mwenye uhakika though kama hii imechorwa au la and that's beside the point. Nachosema ni kwamba if we believe this site is not serving our interest, tusingoje mpaka wenye haki zaidi ya wengine wachorwe ndio tuibuke njozini. Tuanze kuukataa ushenzi wa aina zote tangu jana bila kujali kafanyiwa nani. Mimi naona hili ndio somo kubwa kwetu.
 
That is too much!!!! Haipendezi sio kwa mkuu wa nchi tu kwa mtu yeyote decent. Pls pls pls, tujiulize mara mbili mbili kabla ya kuweka picha za ajabu mtandaoni. God forbid.
 
Ni kweli nami nimeona hii picha si nzuri kwa raisi wa nchi kama binadamu mwingine. Watu wengi wamewekwa mle bila wao kujua lakini hakuna lililosemwa! SASA AMEWEKWA MKULU WATU WANAPIGA KELELE. Lazima kuwa na maadili kwa watu wote situ eti kwakuwa huyu ni kiongozi na huyu ni mtu wa kawaida.
Nimekosa la kuandika.
Sijui wapi tulikosea kama taifa, kuhusu suala zima la kujenga uzalendo pale heshima ya taifa letu inapokuwa mashakani.
 
kisale,unasema JK ni mpenzi mkubwa wa hiyo blog,mimi naona weye mwenzetu si bure umekunywa maji ya choo

Son of Alaska!kwani ni nani wasomaji wa hiyo Blog?...kwani JK hawezi isoma?na nini kinacho kufanya ufikiri hawezi kuwa na yeye anaicheki?mimi naamini inawezekana kwa sababu nina mheshimiwa mmoja rafiki yangu ni jina kubwa mno serikalini na anipenda hiyo Blog ajabu.watu wangekuwa wanaandikwa majina yao ungekuibaliana na mimi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom