Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,225
- 219,401
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .
Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?
Naomba kuwasilisha .