Je, Rais wa Tanzania aweza kuitwa Mahakamani kama Shahidi wa Utetezi kwenye kesi ya Mbowe na Wenzake watatu?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,729
218,291
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?


Naomba kuwasilisha .


Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
 
CCM ya Sasa na Serikali yake wamemtengeneza Rais kua mungu mtu wao..

Hilo haliwezi kutokea
Hakuna cha mungu-mtu Katika shughuli za kimahakama.

Si wameyataka wenyewe??

Kwa sheria za kimahakama, Rais akiandikiwa "Samansi" ya kuitwa kuja kutoa ushahidi, inabidi aititikie wito huo na kuhudhuria vikao hivyo vya kimahakama na vile vile awe tayari kuulizwa maswali na mawakili wa upande wa utetezi, akina Kibatala😁

Hapo ndipo ulipo mtihani wenyewe
 
Kwa sheria za kimahakama, Rais akiandikiwa "Samansi" ya kuitwa kuja kutoa ushahidi, inabidi aititikie wito huo na kuhudhuria vikao hivyo vya kimahakama na vile vile awe tayari kuulizwa maswali na mawakili wa upande wa utetezi, akina Kibatala

Hapo ndipo ulipo mtihani wenyewe
Mkuu kwa jinsi unavyoona, mahakama hizi wanaweza kumuandikia wito?
Bashite tu kuwa karibu nae wameshindwa, ije kuwa yeye mwenyewe
 
Mkuu kwa jinsi unavyoona, mahakama hizi wanaweza kumuandikia wito?
Bashite tu kuwa karibu nae wameshindwa, ije kuwa yeye mwenyewe
Kama wanataka Haki itendeke, itabidi apokee huo wito na ahudhurie hiyo Kesi.

Kinyume cha hapo Haki haiwezi kutendeka.

Kumbuka mahojiano ya Rais Samia na Kikeke wa BBC, alithibitisha kuwa washirika wake Mbowe walishafungwa na yeye Mbowe alikimbilia Nairobi kujificha!

Ni lazima aje kuyathibitisha hayo aliyoyasema BBC
 
Kama wanataka Haki itendeke, itabidi apokee huo wito na ahudhurie hiyo Kesi.

Kinyume cha hapo Haki haiwezi kutendeka.

Kumbuka mahojiano ya Rais Samia na Kikeke wa BBC, alithibitisha kuwa washirika wake Mbowe walishafungwa na yeye Mbowe alikimbilia Nairobi kujificha!

Ni lazima aje kuyathibitisha hayo aliyoyasema BBC
Kimenuka !
 
Suala la Mzee Mkapa ni tofauti na hili yeye alishakuwa ameshastaafu! Ila Kwa hili la sasa kuna utata huenda tupate maelezo ya kisheria!
 
Back
Top Bottom