Je, Rais wa Tanzania aweza kuitwa Mahakamani kama Shahidi wa Utetezi kwenye kesi ya Mbowe na Wenzake watatu?

Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?

Naomba kuwasilisha .

View attachment 2123826
Mkuu jibu ni MOJA hakuna aliejuu ya SHERIA, lazima akafike safari hii, tatizo CCM humuona Rais ni Mungu, kumbe ni kiongozi wa nchi tena KWa mda tu , yule ni binadam Kama Mie na wewe sema ana heshima yake
 
Rais ana kinga ya kutokushtakiwa tu, ila hana kinga ya kutokuitwa mahakamani kama shahidi.

Kwa ufupi, anaweza kuitwa kama shahidi wa upande wa utetezi either kwa;

1) Kupewa wito na mawakili wa upande wa utetezi afike kama shahidi.

2) Mawakili wa upande wa utetezi kuiomba mahakama imuite kwq lazima kama shahidi wao wa upande wa utetezi (Kama atagoma kuitikia wito wa mawakili wa utetezi #1).

NOTE; Naona kabisa hawa wakiitwa kama mashahidi wa upande wa utetezi, na naona watakataa wito wa kistaarabu kutoka kwa Adv Kibatala then watafanya maombi mahakama iwaite kwa nguvu;

● Rais SSH.

● IGP Sirro.

● Lengai Ole Sabaaya (Huyu hana umuhimu sana kwasababu ni Mhalifu - Convicted Criminal).

● DCI (Anaweza kuitwa kwa mara ya pili mahakamani, ila safari hii kwa maombi ya mawakili wa upande wa utetezi na atatambulika kama shahidi wa upande wa utetezi. Ataitwa ili akavunjwe vunjwe mbavu)
Nimekuelewa Sana yapo majitu humuona Rais kwamba sio binadam wa kawaida ,
Rais ana heshima yake nakubali,ila Hana Cha ziada kuliko binadam yoyote nje ya cheo chake Cha kidunia, anahitaji takwa lile lile Kama binadam mwingine Ili kuishi, CCM acheni ushamba ,Sasa tutamtaka mahakamani atake au asitake ,ukimwaga mboga sie Ugali
 
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?

Naomba kuwasilisha .

View attachment 2123826
Watu wa CHADEMA punguzeni makelele mitandaoni, nyinyi hamna Siri? Mkoje nyinyi mnatoa siraha zote kabla ya pambano?? Inafikilisha sana Ujue mnapaswa kuwa na Siri sijui kama mtanielewa ,
 
Rais ana kinga ya kutokushtakiwa tu, ila hana kinga ya kutokuitwa mahakamani kama shahidi.

Kwa ufupi, anaweza kuitwa kama shahidi wa upande wa utetezi either kwa;

1) Kupewa wito na mawakili wa upande wa utetezi afike kama shahidi.

2) Mawakili wa upande wa utetezi kuiomba mahakama imuite kwq lazima kama shahidi wao wa upande wa utetezi (Kama atagoma kuitikia wito wa mawakili wa utetezi #1).

NOTE; Naona kabisa hawa wakiitwa kama mashahidi wa upande wa utetezi, na naona watakataa wito wa kistaarabu kutoka kwa Adv Kibatala then watafanya maombi mahakama iwaite kwa nguvu;

● Rais SSH.

● IGP Sirro.

● Lengai Ole Sabaaya (Huyu hana umuhimu sana kwasababu ni Mhalifu - Convicted Criminal).

● DCI (Anaweza kuitwa kwa mara ya pili mahakamani, ila safari hii kwa maombi ya mawakili wa upande wa utetezi na atatambulika kama shahidi wa upande wa utetezi. Ataitwa ili akavunjwe vunjwe mbavu)
Kindly enlighten me on this matter, umeitoa kwenye Sheria gani? Kama ni Katiba inakuwa Ibara ipi mkuu? Just for reference nikawanyooshe sehemu
 
Umemaliza kuandika uchafu wako??? Acha kuongea vitu usivyokua na elimu navyo mdudu wewe!!!

Rais Benjamin Mkapa alikwenda kutoa ushahidi mahakamani kwa upande wa utetezi kwenye kesi iliokua inamkabili Balozi wa zamani Prof Costa Mahalu.

Alikwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, na mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi aliokua akimuongoza Rais Mkapa alikua Wakili Alex Mngongolwa.

Kesi iliokua ikimkabili Prof Costa Mahalu ni ya kuisababishia hasara serikali ya Tanzania USD Million 3.098 mnamo mwezi february 2003, wakati akiwa Balozi wa Tanzania nchini Italy.

Nina amini, umejiona juha hamna mfano wake humu JamiiForums kwa kukurupuka kwako.
Mkapa alikuwa amestaafu. The issue at hand is whether a sitting president can be summoned by the Court which he is supreme over it as a witness.

Akishastaafu pia anaweza kuwa shahidi, kushtakiwa kwa criminal matters alizofanya binafsi kama alipigana nk Ila Kama Magufuli alivyoua watu angeshtakiwa Kama kawaida.
 
Hii issue ipo hapa imeelezewa vizuri sana Rais Jakaya na waziri wake Magufuli waliitwa pia kama mashahidi upande wa utetezi lakini hawakutokea

Kuna kesi nyingi kubwa zinazohusisha watu maarufu zilizowahi kufunguliwa na kuamuliwa kwa nyakati tofauti katika historia ya mahakama Tanzania.
Moja ya kesi hizo ni ile ya uhujumu uchumi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Ricky Costa Mahalu, mtaalamu nguli wa sheria na anayetajwa kuwa rafiki wa aliyekuwa Rais wa Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamini William Mkapa.
Profesa Mahalu pamoja na aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin walishitakiwa mwaka 2007, wakidaiwa kula njama, kutumia nyaraka za manunuzi ya jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia ili kumdanganya mwajiri wao (Serikali).
Walishitakiwa pia kwa wizi wa Euro 2,065,827 (zaidi ya Sh2.5 bilioni wakati huo) na kuisababishia Serikali hasara. Kushitakiwa kwa Profesa Mahalu ambaye aliwahi kuwa Mhadhiri na Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuliwasitua wengi. Watu wa karibu yake waliamini kesi ile ilitokana na figisu figisu za kisiasa.
Waliomshitaki walidai wamejiridhisha kuwa walikuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha mashitaka dhidi ya watumishi hao wa umma.
Moja ya tukio kubwa katika kesi hiyo ni pale Rais Mkapa alipoamua kuweka kando ukuu na heshima iliyoambatana na kuwahi kuwa Rais kwenda kusimama kizimbani kumtetea Profesa Mahalu.
Ni miaka 12 imepita sasa tangu kumalizika kwa kesi hiyo na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumwachia huru Profesa Mahalu na mwenzake. Pamoja na kuwa kesi hiyo iliisha miaka mingi iliyopita, kumbukumbu yake imebakia kwenye vichwa vya wengi na kuacha rekodi ya pekee katika historia ya mahakama Tanzania.
Moja ya jambo la kipekee katika kesi hiyo ni aina ya mashahidi waliotajwa katika kesi hiyo, hasa upande wa utetezi.
Mbali ya Rais Mkapa, mashahidi wengine waliotajwa kuja kusimama kizimbani kama mashahidi wa utetezi ni pamoja na Rais aliyekuwa madarakani wakati huo, Jakaya Kikwete na hayati John Magufuli ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Ujenzi.
Kinachoipa kesi hiyo upekee mkubwa ni pale Rais Mkapa aliposimama kizimbani na kutoa ushahidi uliokinzana na ule wa Jamhuri, akiamini Profesa Mahalu na wenzake hawakuwa na hatia.
Uamuzi wa Rais Mkapa uliweka rekodi mbili kwa wakati mmoja. Kwanza, uliifanya kesi hiyo kuwa ya kwanza nchini kuwa na shahidi aliyewahi kushika nafasi ya ukuu wa nchi. Pili, ni kitendo cha aliyewahi kuwa mkuu wa nchi kutoa ushahidi uliokinzana na Serikali aliyowahi kuiongoza.
Hadi kesi hiyo inakwisha, si Kikwete wala Magufuli walifika mahakamani kutoa ushahidi kama walivyotajwa awali na upande wa utetezi.

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Kama wanataka Haki itendeke, itabidi apokee huo wito na ahudhurie hiyo Kesi.

Kinyume cha hapo Haki haiwezi kutendeka.

Kumbuka mahojiano ya Rais Samia na Kikeke wa BBC, alithibitisha kuwa washirika wake Mbowe walishafungwa na yeye Mbowe alikimbilia Nairobi kujificha!

Ni lazima aje kuyathibitisha hayo aliyoyasema BBC
Nahisi shahidi mwingine anaweza kuwa Uhuru Kenyatta kuja kuthibitisha kama kweli alimoa hifadhi ya ukimbizi ndg Mbowe huko inakosemekana alitorokea.😄😃😀
Natania TU jamani
 
Asante kwa vielelezo
Ha ha haa naanza kucheka kwanza 😀😃😄
Pengine Rias wa nchi jirani nae akatimba ku Mahakama kuja kushuhudia kama kweli Mbowe alitorokea Kwenye nchi yake ama lah!
Maana mtu mzito kama Mbowe akiingia kwenye nchi ya watu kwa namna ya kutafuta hifadhi kwa kukimbia mikono ya dola ya nchi jirani Raisi wa nchi hiyo hawezi kutopewa taarifa.
 
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?

Naomba kuwasilisha .

View attachment 2123826

1.Acheni kibatala na wenzake waendelee kuvuna fedha za wajinga kwenye michango kwa kuwaingiza king msiojua lolote kwenye taratibu za adversarial proceeding

2. Tangu lini shahidi ambaye hayupo willing kukutetea au ni mmoja kati ya wanaokushtaki unamwita ili aijenge kesi yako kama sio umemwita ili aibomoe kabisa kesi yako?

3.Najua lengo ni sheria za commedy ili ipatikane mada ya kujadiliwa kwenye space usiku na nadhani lengo sio kuwanasua wateja wao kwenye kesi hapana ni kutaka kuwauliza maswali chechefu ya kudhalilisha ili kurefusha kesi waendelee kuvuna mabilioni ya mabeberu wanaofuatilia kesi hiyo na kupata michango kwa wajinga wakati mwenzao anateseka mahabusu

4.Kumbuka kama hao watakuja kwa mujibu wa sheria za ushahidi kazi ya kibatala na wenzake itakuwa ni
EXAMINATION IN CHIEF , ambayo haruhusiwi kuuliza leading questions.

5.Kwa shahidi mjanja anaweza kuitumia hiyo nafasi kuubomoa ushahidi wote wa utetezi maana wakili wa serikali ambao wapo kitu kimoja ndio mwenye nafasi ya CROSS EXAMINATION hapa watakuwa wametengenezewa jukwaa la bure tena huru la kuishawishi mahakama kile kilichotokea

6.Kibatala na wenzake watakuwa na kanafasi narrow sana cha RE EXAMINATION IN CHIEF ambacho ni cha ufafanuzi tuu wa yale yaliyotokea kwenye CROSS EXAMINATION

7. Kwa ninavyowaona hawa ni kwamba wanataka kutumia hii nafasi kama ya cross examination lakini rule za evidence zitawa guide

8. Haitawezekana taratibu za HOSTILE WITNESS zitumike kuwa cross examine kwa sababu wao sio mashahidi walioandaliwa na deffence na wala hskuna previous statement ambazo wameandika

9. Wakitaka jamaa yao aozee jela mika 30 wafanye huo ujinga wa kuwalazimisha upande wa jamhuri kuwa mashaidi wao itawagarimu
 
Mkapa alikuwa amestaafu. The issue at hand is whether a sitting president can be summoned by the Court which he is supreme over it as a witness.

Akishastaafu pia anaweza kuwa shahidi, kushtakiwa kwa criminal matters alizofanya binafsi kama alipigana nk Ila Kama Magufuli alivyoua watu angeshtakiwa Kama kawaida.
Nipe kifungu cha sheria kimoja ambacho kinatamka kwamba;

1) Rais yupo juu ya mahakama kama unavyosema.

2) Rais hawezi kuitwa kama shahidi mbele ya mahakama.

3) Excemption of Summoning a Witness Kwasababu ya cheo au position ya shahidi.

Babu pitia sheria zote za tanzania, case law zote za tanzania na common law zote then uje na hoja yako.

"NASEMA HAKUNA KASORO (EXCEMPTION) HIO KWAMBA RAIS HAWEZI KUITWA KAMA SHAHIDI MAHAKAMANI (LABDA MAHAKAMA ZA CCM NDIO HAWEZI KUITWA)", as far as upande wowote unaweza kui-move mahakama ili aitwe atakapogoma, basi ataitwa kwa wito wa mahakama (summons).
 
Hakuna cha mungu-mtu Katika shughuli za kimahakama.

Si wameyataka wenyewe??

Kwa sheria za kimahakama, Rais akiandikiwa "Samansi" ya kuitwa kuja kutoa ushahidi, inabidi aititikie wito huo na kuhudhuria vikao hivyo vya kimahakama na vile vile awe tayari kuulizwa maswali na mawakili wa upande wa utetezi, akina Kibatala😁

Hapo ndipo ulipo mtihani wenyewe
Ndoto ya mchana hiyo..
 
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?

Naomba kuwasilisha .

View attachment 2123826
Mkuu nko tayar kurekebishwa ila nnachojua tayar majina ya upande wa utetezi yalijulikana na hoja ilikuwa hlo jina 1 ambalo lilifichwa kwa masilahi ya kisheria, na wameweka makusudi ili kutokuibia mtihani, maana unaweza kuleta mtu ambae hukuwa umemuasigh itakuwa shida, na mahakama ina taratibu zake,

Kwa hyo naona Kama haliwezekani maana kwayo Ni hoja mfu..
 
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?

Naomba kuwasilisha .

View attachment 2123826
Katika kutafuta haki pale inapopatikana, sijawahi kukutana na kifungu cha sheria kinachozuia/kataza Rais asiweze kutoa ushahidi mahakamani. Chukulia kama ndiyo pekee ya kumfanya mshtakiwa atendewe haki katka kesi inayomkabili. Kwa kutozoea kuona Rais akitoa ushahidi mahakamani (isipokuwa Rais Benjamin Mkapa) na kwa madaraka makubwa ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa Rais, tunaogopa hata kusikia anaitwa mahakamani. Hili si tatizo lake, ni letu. Kwa mantiki hii, tunaona heri mtu akose haki yake mahakamani kuliko kusikia au kuona Rais akiitwa atoe ushahidi mahakamani. Sisi, au watu wanaofikiria hivyo, ni watu wa ajabu kabisa!
 
Rais hawezi kwenda kutoa ushahidi, wale walio upande wa serikali wote wanamwakilisha raisi.

Hata hao wanaotetea upinzani wote ni mawakili wa serikali na wana viapo, huwa wanajua mwisho wa kesi hawawezi pia kuharibu cv zao.
 
Hakuna cha mungu-mtu Katika shughuli za kimahakama.

Si wameyataka wenyewe??

Kwa sheria za kimahakama, Rais akiandikiwa "Samansi" ya kuitwa kuja kutoa ushahidi, inabidi aititikie wito huo na kuhudhuria vikao hivyo vya kimahakama na vile vile awe tayari kuulizwa maswali na mawakili wa upande wa utetezi, akina Kibatala

Hapo ndipo ulipo mtihani wenyewe
Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea prof Mahalu.
 
Baada ya Washitakiwa hawa kuonekana wanayo kesi ya kujibu , kuna juhudi kubwa kutoka kwa upande wa serikali kutaka kujua na kuwafahamu Mashahidi wa Utetezi (Haifahamiki malengo ya jambo hili) , Bali lililo wazi ni kwamba Aliyekuwa DCI Robert Boaz na IGP Simon Sirro ni miongoni mwa mashahidi wa mwanzo kabisa watakaoitwa na Mahakama kama mashahidi wa Utetezi .

Swali langu ni hili , Je Rais Samia aweza kuitwa kutoa ushahidi wake Mahakamani kuhusiana na kesi hii ? Maana ipo minong"ono kwenye upande wa utetezi kwamba miongoni mwa mashahidi wao muhimu ni pamoja na Mama Samia , na Je sheria zinaruhusu Rais kuwa Shahidi akihitajika mahakamani ? Nakumbuka Banjamin Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kama Shahidi , kwenye kesi iliyomkabili Costa Mahalu , tulimuona na kumsikia akitoa ushahidi wake huku akitandikwa maswali kadhaa na mawakili wa mshitakiwa , Je kwa sasa mambo haya bado yanawezekana ?

Naomba kuwasilisha .

View attachment 2123826
Kama mahakama ikaridhia waje hamna namna labda wao sasa wagone.
Ila sheria kama inavyoataka wakihitajika hamna namba lazma waifuate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais hawezi kwenda kutoa ushahidi, wale walio upande wa serikali wote wanamwakilisha raisi.

Hata hao wanaotetea upinzani wote ni mawakili wa serikali na wana viapo, huwa wanajua mwisho wa kesi hawawezi pia kuharibu cv zao.
Umenakili kifungu chochote cha katiba ya nchi kwenye hoja yako ?
 
Back
Top Bottom