Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,753
- 218,340
Taarifa kutoka Mbeya zinadokeza kwamba Wakili Msomi Peter Kibatala , anatarajiwa kuwa miongoni mwa Mawakili wa Utetezi kwenye kesi ya uongo ya uhaini iliyobadilishwa kutoka kwenye Uchochezi , inayowakabili Boniface Kajunjumele Mwabukusi na Mdude Nyagali , Labda na wengine wanaotarajiwa kukamatwa kama polisi itakavyotaka .
Ikumbukwe kwamba Msemaji wa Polisi Kamanda Misiime Aliudanganya Umma kwamba Mwabukusi na Mdude wamekamatwa kwa Tuhuma za uchochezi , kumbe kinachowakabili ni Uhaini , bado haijajulikana sababu ya kamanda Misiime kudanganya .
Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania , Mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani baada ya masaa 24 tangu kukamatwa kwake , hawa walikamatwa Jumamosi basi tunatarajia kesho Jumatatu watasomewa Uhaini wao Mahakamani .