Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Big Lady

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
546
75
Wakuu wa Jukwaa,

Heri ya Mwaka Mpya 2012.

Kuna Mwanaume ambaye ametokea kunipenda sana, nami nampenda sana ingawa hatujafikia hatua ya mahusiano ya kimwili. Napenda kumwita A.

Kinachonitatiza ni kuwa enzi za ujana wao, Baba yake A (Namwita B) na Mama yangu walizaa binti ambaye tumpe jina C. Sasa mimi na C tunashare Mama lakini Baba zetu tofauti. C ni dada yangu, yeye ni mkubwa mimi ni mdogo. Wazazi wangu wote walifariki. A na C hawajawahi kufahahamiana hadi walipokutana hivi karibuni na kutambulishwa na baba yake yaani B katika harusi ya Binti mwingine wa baba yake A (yaani baba B) ambaye alizaa na Mwanamke mwingine tena.

Kwa upande wa A, yaani Mwanaume tunayependana amelelewa na familia nyingine toka utotoni ambayo mama yake Mzazi na A aliolewa na Baba mwingine. A ana ndugu zake huko waliolelewa pamoja. Hii ndiyo familia yake ya sasa.

Sasa swali langu kwenu wana MMU, je mimi naweza kuolewa na Mwanaume huyu yaani A?

Naomba kuwakilisha.
 
Halafu mtoto mtakae mzaa wewe na huyo kaka huyo mdogo wako atamuitaje huyo mwanao? Tafakari Chukua hatua

Je, tatizo ni hilo tu? Tafadhali nieleweshe, Kijamii, Kimaadili, Kidini au Kisayansi ili nichukue hatua.
 
Mhhhh! hapo busara inahitajika,
Je mila zenu zinaruhusu?

Best ni kweli busara inahitajika ndo maana nakuja kwenu.

Kuhusu Mila ni mchanganyiko mtupu wa makabila na hata sijui ni mila ipi ya kufuata.

Huyu Mwanaume anayenipenda ni kabila XY. Baba wa Kumzaa kabila X. Baba aliyemlea toka mdogo kabila Y. Mwama yake ni kabila Z.

Mimi baba yangu ni kabila Q na ni mchanganyiko wa makabila mawili. Mama yangu kabila lake ni W.

Nimelewa na ndugu wengine so hata mila sizijui. Same kwa huyo Mwanaume A. labda nianze kuulizia. Ila kabla ya hapo ngoja nipate ushauri kwanza.
 
Rukhusa kwetu sisi kimila unakata undugu kwa kuchinja mbuzi au kondoo.
So kama umemdondokea endelea
 
incest
Mume wa mama yako ni Baba yako, na mke wa baba yako ni Mama. Watoto zao ni kaka ua dada zako period.

Mkuu hawajawahi kuoana ni walizaa tu enzi za ujana wao. Na je, hilo unaloliongelea unaweza ukanipa source yake? Bi bible au Kimaadili au Kijamii tu?
 
Kwa kabisa futa hiyo kitu mawazoni kwako. Huwezi kupima 'kupenda sana'?

Ungeniuliza kwa nini ningekueleza kisha uamue kama ni kweli ananipenda sana au la.

Anyway usijali naona pia umetoka nje ya mada. Ushauri wako ukoje katika mada husika?
 
jibu unalo mwenyewe nauamuzi niwako. kwanini nasema hivyo mapenzi ni siri ya watu wawili sidhani kama mtu baki anweza kuingilia maana mapenzi naweza kufananisha na kidonda ambacho huacha kovu mwilini ambalo halisahauliki maishani kila la heri
 
Back
Top Bottom